Geita: Wananchi wafanikiwa kumuua mamba aliyeua wakazi 5 akiwemo mtoto wa darasa la 3

Nina tone moja tuu hapa lete kikombe cha nyagi nikuchanganyie uonje just ni tone tuu usihofu


Huo utakuwa ni ushindani wa kitoto (a childish contest).

Wewe upo wapi na mimi nipo wapi ili tukutane unipe hiyo nyongo???!!😩- it is impossible.

Wenzako hufanya hivi; Chukua hiyo nyongo changanya na unga kisha weka sehemu ambapo kuna panya, kama ni sumu basi maramoja hao panya watakufa na hapo utathibitisha na kuleta ushahidi hapa.

Watu weupe wanatushinda sisi watu weusi katika mambo kama hayo, wao hujibidisha katika tafiti ili kupata ukweli, mtu mweusi tafiti yake ni kuangamiza mwenziye.🤣
 
Ni uzushi uliotapakaa na hasa huku Afrika mashariki na kati kwamba nyongo ya mamba ni sumu.

Na watu ukiwauliza kazi ya nyongo mwilini mwa viumbe hai ni ipi??!!-- wala hawajui.

Nyongo hata Binadamu, kuku, mbuzi nk, wanazo.

Kwanza Kazi ya nyongo ni nini????

watu wanasema nyonyo ya Mamba ni sumu ,wewe unadai hata binadamu anayo hivo hiyo ndio fact yako kwamba nyongo ya mamba sio sumu ? wenzio wamekuwa specific kwamba “nyongo ya mamba “ ni sumu wewe unaongelea story za nyongo ya binadamu dah
 
watu wanasema nyonyo ya Mamba ni sumu ,wewe unadai hata binadamu anayo hivo hiyo ndio fact yako kwamba nyongo ya mamba sio sumu ? wenzio wamekuwa specific kwamba “nyongo ya mamba “ ni sumu wewe unaongelea story za nyongo ya binadamu dah


Venom za nyoka, Nge, Dondola (nyigu), Nyuki nk, zimethibitika kisayansi (kibaiilojia) kwamba ni sumu na kuna maandiko kibao kuhusu hizo venom na mahospitalini kuna dawa za sindano kwa ajili ya watu walioumwa na hao wadudu na kila siku watu wanaumwa na hao wadudu (wanyama).

Sasa lete andiko la kisayansi linalonyesha kwamba nyongo ya mamba ni sumu, kumbuka Mamba hawapo Tanzania au Afrika tu bali wapo Asia wapo America, wapo Australia, wapo latin America--- kote huko tafuta habari au andiko la kisayansi linalosema nyongo ya Mamba ni sumu.

Jifunze jambo hili:- Nyongo katika miili ya wanyama kazi yake ni moja tu nayo ni kuyeyusha (kusaga/digesting) mafuta yanayoingia tumboni mwa mnyama, hata nyongo iliyomo tumboni mwako kazi yake ni hiyohiyo na sio vinginevyo.
 
Back
Top Bottom