Namtumbo: Mtoto wa darasa la nne apigwa risasi akiwa anavua samaki kwa ndoano

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,095
4,059
Mtoto wa darasa la nne katika shule ya msingi Songambele iliyopo kata ya Mchomoro wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma Ashalaf Saidi amepigwa risasi kipindi akivua samaki na watoto wenzake.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa tisa mchana, baada ya askari polisi kusambaa katika pori lililosadikika kuwepo kwa mtuhumiwa wa Ugaidi Mbaraka Ibadi Maleka.

Tukio hili ni mwendelezo wa operesheni ya kusaka kikundi kinachosadikika kuwa ni cha Kigaidi kilichokuwa kinaongozwa na Ibadi Rashidi Maleka. Watuhumiwa wa kuu ni Ibadi R Maleka pamoja na watoto wake wawili, Antwiya pamoja na Baraka.

Watu kadhaa hadi sasa wamekamatiwa na baadhi wameachiwa na jeshi la polisi ikiwa kama wahisiwa au undugu na urafiki wa karibu na Ibadi.
Ibadi ni miongoni mwa mashekhe wakubwa sana katika wilaya na Mkoa kwa ujumla.

Taarifa za chinichini zinadaiwa ni baada ya Antwiya kuuwawa katika mapango ya Kibiti, kikundi kiliamua kujipanga tena upya chinichini ili kulipiza kisasi. Ndipo Baba pamoja na watoto wake hao wawili wakaanzisha chuo maalumu cha mafunzo ya ngumi huko Mchomoro katika pori la Namawala.

CHANZO CHA KUJULIKANA KUNDI

Inadaiwa ubabe na ukatili wa wanafunzi hao ilichangia kujulikana kwa kundi hilo. Aidha kundi hilo lilikuwa na ubabe wa kuingia shambani kwa mtu na kuchukua chochote kwa kuwa tu mtu huyo haswali swala tano au hawaendani kiitikadi. Kero zilifikishwa katika serikali ya kijiji na kikundi kiliamuliwa kisitishe masomo yao. Kikundi hiki awali kilikuja kwa sura ya madrasatu ila ajabu wageni walikuwa wanamiminika.

Baada ya amri hiyo kikundi hicho kiliondika na kwenda kujichimbia ndani zaidi bila ya mtu kujua. Wakiwa huko wakaweka sheria kali ya mtu yeyote atakae pita au kuona makazi yao basi auwawe ili kutunza siri. Siku moja wanawake wawili walienda polini kukata nyasi na bahati mbaya walipita jirani na kambi hiyo. Mtu mmoja asiyejulikana aliwaona na akaenda kuwatishia wale wanawake kuwa wasije tena eneo lile kwani watauwawa.

Baada ya kufanya hivyo, akawa amevunja masheri ya kambi hivyo yule mtu alichinjwa na kufukiwa karibu na kambi hiyo.

PILISI KUVAMIA KAMBI

Baada ya wale wanawake kuondoka walitoa taarifa kwenye serikali ya kijiji kwa kusimulia yaliyowakuta. Serikali ya kijiji ikatoa taarifa kituo cha polisi na wakaenda kuvamia kambi.

Makabiliano yalikuwa, huku washukiwa wa ugaidi wakitumia silaa za jadi na polisi silaa za moto. Baadhi walikimbia na baadhi waliuwawa na wengine kushikiliwa na jeshi la polisi. Katika pekua pekua polisi waliona mahala pamefukiwa kitu maana kuna shimo kubwa. Huku wakidhani ni handaki la silaa, Kumbe kiwiliwili cha mtu aliyechinjwa.

TUKIO LA KUUAWA MTOTO

Jana kulikuwa na taarifa ya kuwa Baraka ameonekanika porini na anamhitaji baba yake mdogo Abi Rashidi Maleka. Akiwa porini(Baraka) alimtuma mtoto na kumwambia kuwa Abi anaitwa na Baraka.

Kundi hili liliapa lazima litamuua Abi bila ya sababu kuwa wazi. Ila Abi ni mkali wa Martial Arts(Ngumi) na hii labda ilipelekea kwa kuwa yy (Abi) ni mwamba wa ngumi.

Baada ya Abi kutalifiwa juu ya kuhitajika na Baraka, alienda serikali ya kijiji na kueleza juu ya kuitwa kwake na Baraka. Uongozi wa kijiji bila ya kukawia wakatoa taarifa polisi.

Jana majira ya saa nane mchana polisi wakiwa na gari tatu wakiambatana na wanausalama wa mkoa walitinga kijijini. Walivamia sehemu ambayo inasemekana Baraka alikuwepo, katika uvamizi huu ndipo Mtoto (RIP) alikuwa huko polini akivua samaki na akawa amepigwa risasi.

NANI ALIYEUA POLISI AU BARAKA?

Hapa kuna taarifa mbili tofauti kwani raia wanasema polisi ndio walioua na polisi wanasema Baraka ndiye aliyeua. Taarifa za kuaminika ni kuwa Kijana Baraka anatembea na upanga pamoja na silaa za jadi. Ila Baraka bado hajapatika hadi leo na polisi wanaendelea na kazi yao ya kuhakikisha kijana anapatikanika.

RAI: Naomba uchunguzi ufanyike juu ya kuuwawa kwa mtoto hata kama Namtumbo hakuna wafuatiliaji na vyombo vya habari vya kushinikiza haki ya familia ipatikane hata kwa uchache.

Kesho mchana mazishi ya Kijana.

Ahsante.
 
sijui nisemeje lakin watu wanaangalia makosa tu ya polisi umeambiwa ni bahati mbaya mbona hakuna aliesifia polisi kwa kazi mzur yakuwasambalatisha hao wapuuzi ila kila mtu analaumu polisi yaan ningekuwa IGP ao askari ningewapa maelekezo waache iyo operations Mara moja waende kwao maana wanainchi hawana shukran
 
Hebu tupe experience, na iwe based kwa white people.. usituletee za latin America maana unataka kutuona sisi wehu kwamba raia wa marekani afanyiwe brutality na polisi kama wa huku.
Bora mara 100 polisi wa bongo kuliko wa USA! Tatizo hamfatilii
 
sijui nisemeje lakin watu wanaangalia makosa tu ya polisi umeambiwa ni bahati mbaya mbona hakuna aliesifia polisi kwa kazi mzur yakuwasambalatisha hao wapuuzi ila kila mtu analaumu polisi yaan ningekuwa IGP ao askari ningewapa maelekezo waache iyo operations Mara moja waende kwao maana wanainchi hawana shukran
Mkuu hawajui madhara ya kuwaacha hawa imani kali wastawi, hawa imani kali sio wa kuonea huruma hata kidogo
 
Back
Top Bottom