Geita: Ajali yaua 10 Bukombe, gari la Jeshi lilitokea Bukoba kwenda Dar

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,857
2,000
WhatsApp Image 2021-08-18 at 7.38.52 PM.jpeg

Watu kumi wamefariki Dunia katika ajali ya magari mawili katika kijiji cha Ilalwe kata ya Bukombe wilayani Bukombe Mkoani Geita.

Mkuu wa wilaya ya Bukombe Said Nkumba amezungumza na TBC kwa njia ya simu na kuthibitisha tukio hilo na kwamba shughuli ya utambuzi wa maiti hizo bado unaendelea.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa saba mchana ambapo gari la aina ya SCANIA yenye namba ya usajili T130 ERZ ikiwa imebeba mzigo kutoka Dar es Salaam kwenda Rwanda imegongana uso kwa uso na gari ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) yenye namba ya usajili 5964 JW 12 aina ya LEYLAND ASHOCK iliyokuwa inatokea Bukoba kutoka kuzika wakirudi Dar es Salaam .

Maiti zote zimehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Bukombe ambapo katika ajali hiyo kuna majeruhi Wanne wanaendelea na matibabu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom