Gazeti Raia Mwema nalo mfukoni?

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,524
13,099
Nimekuwa muumini mkubwa wa gazeti la Raia Mwema kutokana na ukweli kwamba ni moja ya magazeti yanayoandika habari kwa weledi mkubwa.

Waandishi wa gazeti hili nimekuwa nikiwaona ni miongoni mwa waandishi wenye weledi mkubwa na wasioyumbishwa. Hata waandishi wa kujitegemea wanaotuma taarifa kwenye gazeti hili ni wa kutiliwa mfano.

Nimeanza kuwa na mashaka baada ya kufanya tathmini kwa muda wa miezi kama mitatu hivi kama bado baadhi ya waandishi wa gazeti hili wanatilia maanani kiapo chao cha uandishi.

Nakumbuka Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye alitembelea vyombo karibu vyote vya habari na gazeti Raia mwema likiwa mojawapo. Tangu wakati huo nimekuwa siridhishwi na habari zinazoongoza kwenye gazeti hilo ukurasa wa mbele. Ni habari ambazo ni tofauti sana na zilivyokuwa zinaripotiwa mwanzo.

Wadau mtanisaidia lakini mwenye kufanya tathmini alinganishe habari zinazoongoza ukurasa wa mbele kwa muda niliotaja na jinsi ilivyokuwa inaripotiwa kabla.

Utafiti wangu umejionyesha dhahiri baada ya hekaheka za kampeni za Igunga kuanza.Gazeti hili likiripoti habari ya Igunga limekuwa likionyesha waziwazi kwamba CCM itashinda. Tafuta nakala ya wiki iliyopita.

Gazeti la leo limetoa taarifa kwamba Chadema na CUF watashindwa kwa sababu watagawana kura za upinzani,na habari hii imewekwa ukurasa wa mbele kwa makusudi na naamini imepangwa.

Sasa nikajiuliza kwanini gazeti hili liseme eti CUF na Chadema watagawana kura? Ina maana kura za kugawanyika ni za CUF na Chadema tu?

Ningependa kuwashauri wahariri wa gazeti hili watambue kwamba imani kubwa wananchi waliyokuwa wanaonyesha kwa gazeti hili inaanza kufifia na hakika mimi ni miongoni mwa watu watakaokuwa wanafikiri mara mbilimbili wakati wa kununua gazeti hili.

Nawasilisha.
 
Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,882
1,124
Ni maoni yao tu sioni shida kwanza igunga magazeti mijini yanasomwa kesho yake na vijijini hayafiki mimi nashauri chadema wagonge kampeni usiku na mchana mpaka kieleweke.
Mbinu chafu za ccm zinajulikana chadema kaza buti.
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,395
RaiaMwema kama kawaida yao wameandika ukweli tu. Baadhi yetu tulishayaandika hayo humu JF. CHADEMA na CUF wana wagombea wazuri kwa Igunga. Watagawana kura zisizoitaka CCM na mgombea wake.
 
Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Nimekuwa muumini mkubwa wa gazeti la Raia Mwema kutokana na ukweli kwamba ni moja ya magazeti yanayoandika habari kwa weledi mkubwa.

Waandishi wa gazeti hili nimekuwa nikiwaona ni miongoni mwa waandishi wenye weledi mkubwa na wasioyumbishwa. Hata waandishi wa kujitegemea wanaotuma taarifa kwenye gazeti hili ni wa kutiliwa mfano.

Nimeanza kuwa na mashaka baada ya kufanya tathmini kwa muda wa miezi kama mitatu hivi kama bado baadhi ya waandishi wa gazeti hili wanatilia maanani kiapo chao cha uandishi.

Nakumbuka Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye alitembelea vyombo karibu vyote vya habari na gazeti Raia mwema likiwa mojawapo. Tangu wakati huo nimekuwa siridhishwi na habari zinazoongoza kwenye gazeti hilo ukurasa wa mbele. Ni habari ambazo ni tofauti sana na zilivyokuwa zinaripotiwa mwanzo.

Wadau mtanisaidia lakini mwenye kufanya tathmini alinganishe habari zinazoongoza ukurasa wa mbele kwa muda niliotaja na jinsi ilivyokuwa inaripotiwa kabla.

Utafiti wangu umejionyesha dhahiri baada ya hekaheka za kampeni za Igunga kuanza.Gazeti hili likiripoti habari ya Igunga limekuwa likionyesha waziwazi kwamba CCM itashinda. Tafuta nakala ya wiki iliyopita.

Gazeti la leo limetoa taarifa kwamba Chadema na CUF watashindwa kwa sababu watagawana kura za upinzani,na habari hii imewekwa ukurasa wa mbele kwa makusudi na naamini imepangwa.

Sasa nikajiuliza kwanini gazeti hili liseme eti CUF na Chadema watagawana kura? Ina maana kura za kugawanyika ni za CUF na Chadema tu?

Ningependa kuwashauri wahariri wa gazeti hili watambue kwamba imani kubwa wananchi waliyokuwa wanaonyesha kwa gazeti hili inaanza kufifia na hakika mimi ni miongoni mwa watu watakaokuwa wanafikiri mara mbilimbili wakati wa kununua gazeti hili.

Nawasilisha.

Uko sahiihi 100% gazeti hili limeshanunuliwa siku nyingi. Si hili tu Nipashe tayari, Mwananchi tayari hawa wamiliki ni makada wa CCM baada ya kutoswa wakina Rostam wamerudishwa kundini ili wasaidie adui wao sio mfumo ni Rostam,ELna Chenge. Badae utaona mengi we subiri.
 
Vin Diesel

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
9,095
6,321
Kwahiyo wewe wataka gazeti liwasifie CDM ndio utaamini kuwa linaandika habari za kweli? CDM hatoki igunga huo ndio ukweli.
 
Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
Yaani we jamaa huna hata chembe ya utu. Kwako wewe habari ya ukweli ni ile inayosifia magwanda lakini nyigine zote ni za uongo. Basi endelea kusoma Tz daima kama unataka aina hiyo ya habari.
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,395
walisema hivyohivyo ubungo kuwa mtatiro atagawana kura na mnyika.....kilichotokea wenyewe mnajua
Kwa Ubungo ni case nyingine kabisa. Mnyika alishajijenga sana tu. CCM nao wakaboronga kwenye uteuzi wa mgombea wao. Wangemteua Nape bado Mnyika angeshinda lakini kwa taabu sana.
 
Kishongo

JF-Expert Member
May 4, 2010
932
64
Gazeti hili lilipokuwa linakandia CCM lilikuwa halijanunuliwa. Sasa linaposema ukweli kuhusu CDM...limenunuliwa. ULIMBUKENI HUU!

Mashabiki wa cdm watakomaa lini na kuachana na uvivu wa kufikiri unaowafanya watoe mawazo ya kipuuzi kama hii pumba iliyomwagwa hapa?
 
timbilimu

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
4,840
1,490
Mimi nilianza kutilia shaka uandishi wa gazeti la Raia Mwema wakati CCM ilipoanzisha ngonjera za kujivua gamba. Mpaka muda mwingine ungedhani pengine kichwa cha habari na habari ameandika Pius Msekwa ama Mukama! Itabidi wajirekebishe kama wanataka kutubakiza kama wasomaji wa gazeti lao ambalo kusema kweli huwa sikosi nakala ya toleo lao la kila wiki.
 
gepema

Member
Mar 25, 2010
97
9
Tuache ushabiki pembeni,kwa muda sasa gazeti la raia mwema limekuwa na main stories ambazo zinaacha maswali kwa wasomaji.
Tena hii kitu tumetoka kuizungumzia hapa ofcn kwetu na jamaa yamgu mmoja ambaye naye ni muumini wa haya magazeti mawili ya jumatano!!!!!
 
Gwota

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
205
92
Naunga mkono hoja, Na si kicha cha habari cha mbele pekee hata makala zake ni za kuonesha wamenunuliwa. Ccm watanunua magazeti yote lakini nguvu ya umma inayoongozwa na chadema still itashinda tu hujuma hizi. Mm kuanzia wiki iliyopita sijalinunua
 
mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,568
185
Sioni tatizo kwa gazeti kuandika ilicho kiandika hata editorial yao ya leo ukiisoma unaweza kuwa na dhana hiyo lkn nafikiri ni maoni yao na utafiti wao si lazima uwe sawa na maon8i na utafiti wako hsa kama unakuwa na majibu yako kabla ya utafiti
 
Mshirazi

JF-Expert Member
Dec 8, 2009
444
159
Mkuu wewe unataka liandike UKWELI au unataka liandike yale yanayokupendeza wewe tu??

Kama unataka UKWELI na UHAKIKA basi ndio huo,, laa kama unataka yale ya kukufurahisha nunua Tanzania Daima, utafuraaaaahi

teh teh teh...
 
Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
126
Sioni tatizo kwa gazeti kuandika ilicho kiandika hata editorial yao ya leo ukiisoma unaweza kuwa na dhana hiyo lkn nafikiri ni maoni yao na utafiti wao si lazima uwe sawa na maon8i na utafiti wako hsa kama unakuwa na majibu yako kabla ya utafiti

amenipunguzia gharama na matumizi ya kununua magazeti leo
 
Makindi N

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
1,067
172
Tena km toleo la leo trh 21-Sept, habari km ya WASTAAFU KUWAKABILI SLAA, LIPUMBA..... nahisi Philip Mangula ndo kaiandika halafu Raia Mwema wakaitoa..... Vichwa vilivyobaki labda ni Msomaji Raia na Johnson Mbwambo? Kulikoni Jenerali siku hz, haonekani? No wonder karibu matangazo yote ya serikali wanayapata wao...........
 
commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,101
1,526
Nimekuwa muumini mkubwa wa gazeti la Raia Mwema kutokana na ukweli kwamba ni moja ya magazeti yanayoandika habari kwa weledi mkubwa.

Waandishi wa gazeti hili nimekuwa nikiwaona ni miongoni mwa waandishi wenye weledi mkubwa na wasioyumbishwa. Hata waandishi wa kujitegemea wanaotuma taarifa kwenye gazeti hili ni wa kutiliwa mfano.

Uko sawa mkuu na kwa uthibitisho soma makali ya mwandishi wa habari mkuu bwana dillunga katika toleo hilohilo ukurasa wa 17,
Nimeanza kuwa na mashaka
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom