Halafu ndiyo mnasema kuna cha kujivua magamba hapo? Kugawa magazeti bure ni nini basi kama si aina nyingine ya ufisadi? Kwa kweoli hii ni aibu kubwa kwa CCM na ni dalili mbaya kabisa kwani sasa inaonekana CHADEMA wamewashika pabaya. Habari zooote zilizomo ndani ya gazeti hilo ni porojo tu na kama wahuni hao walioandika wanabisha wajaribu kuitisha mikutano miwili katika mji mmoja, mkutano mmoja uhutubiwe na Dr. Slaa na mwingine uhutubiwe na JK kisha upime mwenyewe watu watamiminika kwenda msikiliza nani.Hivi ni kwa nini CCM wanakubali kudhalilika namna hii?
CCM bado hawajabaini kwamba vitendo vyao ovyo ovyo vinawapa nguvu wasizotarajia wapinzani. Kwa mfano wamekuwa miaka nenda miaka rudi wakipinga juu ya uwepo wa mafisadi ndani ya CCM wakitamba ati mwenye ushahidi awasilishe. Tena walikuwa wakiimba kila siku kwamba CHADEMA ni waongo, wazushi wakubwa; leo hii wanajinadi ati wanaendesha operesheni ya kujivua magamba kwa kuwatimua mafisadi ndani ya chama chao! Je, hapo ni nani mzushi, mlaghai na mwongo? Kwa kitendo chao hicho cha kukiri hadharani kwamba ni kweli kuna mafisadi miongoni mwao wamedhihirisha kwamba wasema ukweli katika nchi hii ni CHADEMA pekee na walaghai, waongo na wazushi ni CCM.
Sasa ndiyo nakumbuka maneno ya Baba wa Taifa aliposema " Kiongozi aliyeingia madarakani kwa rushwa, hataweza kamwe kupambana na rushwa". Ukweli ni kwamba Rais aliyeingia madarakani awamu ya Kwanza kwa fedha zilizoibiwa toka Benki Kuu (EPA), na kwa kuchakachua katika awamu ya pili na ambaye yumo kwenye "payrol" ya mafisadi wa IPTL, Richmond, Ticts n.k. kamwe hawezi kuongoza mapambano dhidi ya walarushwa. Hivi CCM bado wanadhani kuna nafasi ya cheap propaganda katika siasa za TZ kwa sasa enzi za kizazi cha Dot Com? Kama mwendo ndiyo huu wa kisanii kisanii CCM haitafika hata 2015.