Gazeti la Uhuru lammaliza Lowassa

Watu wengine. Tunatumika adha kwa kujia au kwa kulipwa Chama changu nakubaliana kimeshindwa na ni wote kuanzia mkubwa mpaka ndogo ufisadi mkubwa upo juu na report ambayo inafichwa mpaka Leo pesa iliyoibiwa kwa muda wa miaka Sita ni bilion 870 nchi imefilisika na ni viongozi wa juu na pesa zipo kwenye baadhi ya nchi za kiafirika awapeleki Tena ulaya. Wanafichiana wakibwa ni Azimio la umoja wao
 
Kumbe mpo wengi humu... Haya jioni njema, nilidhani tunajadili mustakabali wa taifa letu kumbe wengine mpo kazini... Au revoire!
Inatisha sana. Siamini kwamba sasa watu wameanza kumtetea EL kiaina, siamini kwamba sasa EL anaonekana anweza kuwa Rais wa nchi hii tena humu ndani ya JF, siamini mambo mengi tu na kwa kweli siamini kabisa kuwa jukwaa limeanza kumuona EL shujaa na soon RA atakua mfadhili na si fisadi tena, siamini kwamba tumeshasahau zile thread zote zinazomuita EL mwizi zimesahaulika. MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Makala ya gazeti la uhuru kama yamelenga Lowasa nafikiri huo ndio mwanzo wa mwisho wa chama cha Mwl Nyerere.Kwani walio wengi tena wenye nyadhifa kubwa kubwa si wasafi.Hatujui Lowasa amejipanga vipi? Sio mtu wa kudharau,ni moto mkali ambao hao wanaojipitisha pitisha na kampeini za kuvua gamba hawawezi kumsogelea.Siku tisini sio nyingi tusubiri hayo mapambano ,sisi watazamaji.
 
EL anapata sympathisers kwavile mnataka mumtoe tena kafara ilhali kuna wanachama wengi tu huko wasi safi!
 
Pale Uhuru wanapotoboa Jahazi ambalo nao wanasafiria. Tehe eee tehe nilikuwa sijaiona Logo ya gazeti la uhuru siku nyingi, kumbe bado lipo...
 
Hawo wanaomsakama lowassa watuambie nani msafi ndani ya ccm mmoja tu Kama wote ni wachafu basi woote awafai Kama baraza limepitisha kitu wote wanausika je nani I msafi tuambieni si kutumika kumchafua Mtu mmoja jamaa bado wengi wanamkubali hakuna wakumfikia kwa kwa uchapakazi. Na kuhamisisha kazi na alipita kila wilaya na tulipewa nafasi ya kuwahoji watendaji wazembe vijijini na wanasImaama na kujibu tuhuma hapo ka hapo
 
Jamani mjadala mwema maana hapa kwa EL patamu ila na mimi nasubiri siku atakapofungua mdomo wake kuhusu Richmond Teh teh labda kuna watu wataomba ardhi iwameze akiwemo JK
 
hilo ndio gazeti kongwe la chama cha mapinduzi..my take; wanambip EL akiwapigia wasijeshindwa kupokea tu
Hakika CCM ni Kinda mbele ya Lowassa, na ni kiongozi mwenye msimamo kuliko wote ccm. Hata kama aliiba yeye alianza kuwa mtafutaji siku nyingi tofauti na waliotajirika mara tu waliposhinda urais. Lowassa anaweza kukipa discipline chama na anaowaongoza. Bora mwizi anayeweza kuilinda nyumba yake kuliko anayeiba kwa kujificha lakini hawezi kuionyesha njia familia. Bora Lowassa kuliko Kikwete na wengine ccm maana ni waoga
 
Huyu jamaa hawamjui,mapigo yake ni ANGUKO LA CCM.
Mimi namwomba Mungu ampe roho ya Toba Lowassa na asahau tu ajushushe aombe watanzania msamaha kwa yote aliyokosea na aliyochafuliwa nayo! Hakika tutamwamini na kumkabidhi Ikulu.Tunajua mema yake mengi kuliko huyu Kikwete. Kikwete mchonganishi tu, kawachonganisha akina Sitta na akina Lowassa ili akae kati na afaulu mipango yake, Divide and Rule.
 
Lowassa apunguze upole sasa, alipue na yeye yoote kuhusu jk. Jinsi alivyopata uraisi kwa njia ya rushwa, alivyochonga dili la Richmond n.k_
 
Mie yangu macho waache waumane tuone nani atatokwa gamba then tujue .Ila najua kwa matamshi ya Mukama kuna kivumbi kinakuja wait and see CCM inavyo kufa .
 
Nani sio fisadi CCM? Si umeona jana Kafulila kaongeza list ya wavua gamba? For sure Lowassa yuko clean kuliko JK na Sitta aliyejenga kasri la mil 500 Urambo miezi 6 kabla ya kuvuliwa Uspika.
Hakika pamoja na kwamba naipenda Cdm. ILA LOWASSA ni msafi kuliko hao wote sema tu anajaribu kuepusha shari maana akitaka kufanya chochote ccm anaweza na anaungwa mkono na asilimia kubwa halafu mtandao wake ni kila mahali kwenye ccm. Subiri atoboe ukweli muda ukifika, muumbue Kikwete maana ni mnafiki sana
 
[h=2]Tangu Juni 11 niliweka post hii humu kwenye Jukwaa la Siasa, ila moderators wakaificha kwenye folder ya Hoja na Habari Mchanganyiko ambayo zaidi ni kwa ajili na masuala yasiyo serious... Nyie moderators nao mnatia mashaka sasa!

Lowassa afuata upako kwa 'Nabii' wa Nigeria[/h]
Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu mwaka 2008 kwa kashfa kubwa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa, ametuma ujumbe wa watu wawili waende Nijeria kukutana na Pastor TemitopeBalogun Joshua a.k.a. Prophet T.B. Joshua ambaye 'alimtabiria' Mbunge Beatrice Shellukindo kuwa Lowassa atakuwa Rais wa Tanzania baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Wajumbe hao wa Lowassa ni mtoto wake Frederick Lowassa na mshauri wake mkuu wa masuala ya vyombo vya habari, Absalom Kibanda, ambaye ni mhariri wa gazeti la Tanzania Daima linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Frederick na Kibanda wako safarini Nijeria kwenda kuchukua 'upako' ili wamletee Lowassa asafishe nyota na kuepuka na dhoruba kubwa ya kisiasa katika kipindi hiki kigumu ambacho wajumbe wa NEC ya CCM wamedhamiria kuwafukuza mafisadi kwenye chama, akiwemo Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz.

Wajumbe hawa wa Lowassa wanatarajiwa kukutana na TB Joshua siku ya Jumapili Juni 12, 2011, ambayo mchungaji huyo atakuwa anasherehekea birthday yake na atawapa "dawa" wamletee Lowassa Tanzania ili asafishe nyota yake.

Ikumbukwe kuwa 'nabii' huyu wa Nijeria aliwahi kumwambia Mbunge wa CCM, Beatrice Shellukindo, kuwa anatabiri Lowassa atakuwa Rais ajaye wa Tanzania.

Beatrice, ambaye mume wake William Shellukindo, aling'olewa ubunge kwenye jimbo la Bumbuli na kina Lowassa-Rostam-Chenge na kisha wakamuweka January Makamba, sasa amehamia kwenye kambi ya kumpigia debe Lowassa awe Rais pamoja tuhuma kubwa za ufisadi dhidi yake, ikiwemo kujilimbikizia sana mali, ufisadi wa Richmond, kununua hekaru la sh bilioni 1 London na mengine mengi.

Siri ya Edward Lowassa nje | Gazeti la MwanaHalisi

Eti huyu fisadi kweli anadhani atakuwa Rais wa Tanzania?

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom