Gazeti la serikali ni nini na linauzwa wapi?

Brother Kaka

Member
Jun 11, 2013
90
54
Naomba anayejua maana ya gazeti la serikali ni nini. Naskia skia tu gazeti la serikali lakini sifahamu ni gazeti la HabariLeo au Daily News au ni lipi hilo?Msaada pls.
 
Ni kijarida cha serikali ambacho huchapishwa na mpiga chapa wa serikali, kwa lengo la kutoa taarifa za serikali ikiwemo marekebisho ya sheria mbali mbali na miswada ya sheria mpya zilizopitishwa na bunge na kusainiwa na Rais.. Na matangazo mengineo ya serikali ye sura ya kisheria.
 
Isumbi/Mussolin
Na jee gazeti hili huwa linauzwa kama magazeti mengine au inakuwaje?
 
Naomba anayejua maana ya gazeti la serikali ni nini. Naskia skia tu gazeti la serikali lakini sifahamu ni gazeti la HabariLeo au Daily News au ni lipi hilo?Msaada pls.

ni magazeti yanayomilikiwa na serikali na yapo pia kwa kuandika mema tu ya serikali husika na la kiingereza ni daily news na la kiswahili ni habari leo.
 
Serikali kivuli nayo inagazeti lake hilo!
 
Attachments

  • 1406866899747.jpg
    1406866899747.jpg
    8 KB · Views: 877
Gazeti la serikali ni jarida linalochapishwa na mpiga chapa wa serikali na mara nyingi linalotolewa kila wiki likiwa na taarifa mbali mbali za utendaji wa serikali kama vile kutangaza tarehe za kuanza ajira kwa wafanyakazi wa serikali kuu, tarehe na uteuzi wa viongozi wote wa serikali kuu, kuanza kwa matumizi ya sheria zianzotungwa na bunge, kubatilisha hatimiliki za viwanja, kutoa haki za matumizi ya maji, kutangaza sheria ndogo ( by laws and regulations).

Gezeti la serikali linauzwa kwa kulipia kwa mwaka ( subscription) kwenye ofisi ya mpiga chapa mkuu wa serikali Nyerere Road zamani Pugu Road au ofisi zake zilizopo Jamhuri Street, Dar es salaam na mara nyingi gazeti hilo huletwa kwa njia ya posta au kama una uwezo unaweza kwenda kuchukua mwenyewe kwenye ofisi zao kila wiki au mwezi
 
Naomba anayejua maana ya gazeti la serikali ni nini. Naskia skia tu gazeti la serikali lakini sifahamu ni gazeti la HabariLeo au Daily News au ni lipi hilo?Msaada pls.

nakumbuka siku si nyingi niliuliza kuhusu gazeti la serikali lakini mods waliifutilia mbali thread yangu sijawahi iona mpaka leo ila nashukuru sana Brother Kaka kwa kuuliza
 
Last edited by a moderator:

Wewe uliuliza kijingajinga wakafikiri unampango wa kwenda kulipua ofisi zao ndio maana wakaipotezea. Badilisha jina na msimamo na itikadi ya kidini na utaheshimiwa.
 
kama huna hoja ni bora ukakaa kimya
umejuaje kuwa niliuliza kijingajinga? Ukiambiwa utoe ushahidi wa jinsi nilivyouliza utaweza?
kukaa kimya mara nyingine ni jibu zuri sana
 
Ni kijarida cha serikali ambacho huchapishwa na mpiga chapa wa serikali, kwa lengo la kutoa taarifa za serikali ikiwemo marekebisho ya sheria mbali mbali na miswada ya sheria mpya zilizopitishwa na bunge na kusainiwa na Rais.. Na matangazo mengineo ya serikali ye sura ya kisheria.

Ni Government Gazette ambalo ni tofauti na Daily News na Habari Leo ambayo ni mouthpieces za serikali kipropaganda. Government Gazette haliuzwi through circulation kama magazeti ya kawaida yakiwemo Daily News na Habari Leo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom