Gazeti la MwanaHALISI kufungiwa tena!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la MwanaHALISI kufungiwa tena!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Jan 28, 2009.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Gazeti la Mwanahalisi huenda likajikuta tena matatani kwa kufungiwa kama ilivyokuwa awali baada ya toleo jipya la 28 Jan.-Feb.3, 2009 kuchapisha habari kama zile za awali kuhusu baadhi ya Wanachama wa CCM kutaka kuunda chama kingine (kumeguka).

  Waziri Mkuchika alipokuwa akitafuta kulifungia aliwataka Mwanahalisi wathibitishe habari hizo ndani ya saa 24 na waliposhindwa wakalifungia.

  Habari kama zile za awali zimechapishwa katika Mwanahalisi la leo. Je, Waziri Mkuchika atalifungia tena? Au atalifuta kabisa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 28, 2009
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ni vigumu kutabiri.Lakini kwa staili ya Mkuchika sio ajabu kabisa.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huenda this time Mwanahalisi wanauthibitisho. Sidhani kama watakuwa wajinga wapende kufungiwa kila mara.
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Huyo Mwanahalisi hana jipya zaidi ya CCM?
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Lolote linaweza kutokea; Kama Mkuchika atakuwa kichwa maji na kunasa kwenye mtego kama wa awali, anaweza kuwafungia. Anaweza pia kuwafungia kwa kutaka kuonyesha tu kuwa ile safari ya kwanza haikuwa nguvu za soda. I hope, MwanaHalisi hawajamjaribu Mkuchika ay serikali
   
 6. m

  muasisi Member

  #6
  Jan 28, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uhuru wa vyombo vya habari haupo hapa tz ingawa wananchi wasiojua hilo wanadanganywa kila siku,watz inabidi waamke nafasi pekee iliyo baki ni 2010,sio lazima iwe urais hata tukiwanyima hawa mafisadi viti vya ubunge itatusaidia sana maana ndio wanaamua kufungia magazeti kiholelaholela kwa kuhofia nafasi zao kwani hawajiamini kabisa!
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Suala la kulifungia Mwanahalisi halipo labda kwa kutumia sheria ile ile ya kikandamizaji.Mbona Habari Leo halijafungiwa lilipoongelea Wabunge kutofautiana na Rais,kwani ni siri kuwa kuna mikakati mbalimbali kuelekea uchaguzi wa 2010.Kwanza kwa taarifa kwa wasiojua kile kilichosababisha Mwanahalisi lifungiwe iliisadia Serikali na CCM kwani waliifanyia kazi.Ile kesi ya Wenyeviti wale kudai fidia iko wapi,baadhi ya wenyeviti hao ndio walikuwa nyuma ya Uchaguzi wa UVCCM na UWT na sasa kutaka kuunda chama.Serikali badala ya kukurupuka kuyafungia magazeti iyafanyie kazi yanayoandikwa kwa kutafuta ukweli ili iisaidie katika harakati zake na Rais mwenyewe.Lisemwalo lipo na kama halipo linakuja,mafisadi wanatafuta kila aina na namna ya kuondokana na aibu kwa wizi mkubwa walioufanya uvunguni na sasa ipo juu ya paa.Tabia ya kuziba midomo waandishi wa habari kamwe haisaidii kuficha maovu bali hufichua zaidi.Kazi kwenu watendaji wa Serikali mtafakari na kuchukua hatua.
   
 8. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Tehe tehe tehe! Kho! Acha nicheke kidogo, CCM kumeguka si habari mupya hilyo? Au ndo CCM imeshikilia roho yako kiasi kwamba inaku touch hii mupya (Breaking new).

  MwanaHalisi lete mupyas za CCM tunazingoja. Keep up good job kaka kubenea.
   
 9. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #9
  Jan 28, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete atishia wenzake

  • Wapanga kuhama chama
  • Aliyotabiri Mkapa yaja

  Na Saed Kubenea  BAADHI ya viongozi na wanachama mashuhuri ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wana mpango wa kuanzisha chama cha siasa ili kuweka upinzani mkali kwa Rais Jakaya Kikwete ifikapo 2010, MwanaHALISI limeelezwa.

  Kwa mujibu wa mikakati ya viongozi na wanachama hao, ambayo gazeti hili limepata, chama hicho kinapaswa kuwa kimeanzishwa katika miezi sita ijayo.

  Kwa mujibu wa katiba ya nchi, rais aliyeko madarakani anaruhusiwa kugombea kwa mara ya pili iwapo anapitishwa na chama chake. CCM ina utamaduni wa kumpitisha rais wake kwa kipindi cha pili.

  Sababu kuu ambayo imeelezwa kuwa chanzo cha kuundwa kwa chama cha “waasi” ndani ya CCM ni kile kilichoitwa “kudhalilishwa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi za juu” wa chama hicho.

  Njia tatu zimetajwa kutumika katika kuanzisha chama hicho. Kwanza, kutafuta uwezekano wa kuanzisha chama moja kwa moja. Pili, kujiunga au kununua moja ya vyama vya upinzani vilivyopo ambavyo vimelegalega lakini vina mizizi hasa Tanzania Bara.

  Njia ya tatu ni kwamba iwapo njia mbili za kwanza zitashindikana, basi wapenyeze wafuasi wao katika kura za maoni za CCM na kuwagharimia ili waweze kushinda.

  Mazingira yanayojitokeza katika hili ni kama yale aliyotabiri rais mstaafu Benjamin Mkapa, mwishoni mwa wiki, kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 “utakuwa mgumu na unaweza kuliingiza taifa katika machafuko.”

  Mkapa ametaja siasa za majungu, chuki, fitina, ukabila na udini kuwa mambo yaliyozuka katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na ambayo yatazua ugumu iwapo viongozi hawatajiepusha navyo.

  Miaka miwili na nusu ya utawala wa Rais Kikwete imekuwa ya kimya lakini katika kipindi kuelekea mwaka wa tatu, Kikwete amecharuka na kukamata watuhumiwa wa ufisadi wakiwemo waliokuwa mawaziri katika serikali ya Mkapa.

  Taarifa zinasema baadhi ya viongozi wanaotaka kuanzisha chama ni miongoni mwa watuhumiwa wa ufisadi na ambao wanadai kudhalilishwa na utawala wa Kikwete.

  Kauli ya Mkapa inaonyesha ama anaelewa kinachoendelea kuhusu mkakati wa chama kipya au analilia waliokuwa wasaidizi wake ambao wamekumbwa na zahma sasa.

  Miongoni mwa madai ambayo watuhumiwa wamekuwa wakitoa ni “kuonewa, kufanyiwa fitina na chuki.”

  MwanaHALISI imepewa orodha ya wanachama na viongozi ambao wanatajwa katika mkakati wa kuanzisha chama kipya kwa masharti kwamba wasitajwe kwa sasa.

  Mmoja wao alimwambia mwandishi wa habari hizi, “Nami nimesikia mpango huo, lakini mimi simo kwani mabao yangu siyo magumu.”

  Alisema wale ambao “mambo yao ni magumu kama unavyosema, ndio wanaoweza kujenga mawazo ya kukimbia… Mimi niko kijijini huku nafanya kazi za chama.”

  Mwingine kwenye orodha hiyo ambaye alihojiwa alisema, “Ninavyojua mimi hakuna wabunge wa CCM wanaoweza kuanzisha chama. Hii si kazi ndogo. Kwanza wakianzisha chama sasa hivi watapoteza ubunge na mafao yao.”

  Alipoulizwa juu ya uwezekano wa kujiunga au kununua chama cha upinzani kilichopo alisema, “labda hilo. Hilo linawezekana.”

  Kiongozi wa chama cha NCCR-Mageuzi ambacho kimetajwa kuwa kinaweza kuhamiwa au kununuliwa, amekana kuwa na taarifa zozote juu ya mpango huo.

  Sam Ruhuza, Katibu Mkuu wa chama hicho alimwambia mwandishi wa habari hizi “Mimi sijasikia lolote juu ya hilo.”

  Alipoulizwa huenda hajui kwa akuwa amekuwa kiongozi katika uchaguzi wa mwezi uliopita, alisema “Ni kweli mimi ni mpya kwenye nafasi hii lakini nimekuwa kwenye chama kwa muda mrefu.”

  “Kama mpango huo upo ningeujua, kwa kuwa ni mimi niliyepo ofisini na mwenyekiti wangu yuko nchini Uholanzi kwa masomo,” alisema Ruhuza.

  Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, wanaotaka kuanzisha chama wamelenga kutumia magazeti yaliyopo au kuanzisha mapya ili kuendesha kampeni kubwa ya ushawishi.

  Mmoja wa wamiliki wa magazeti aliyemo katika mpango huo alipoulizwa juu ya mpango wa gazeti lake kutumika, hakijibu bali alikata simu.

  Kumekuwa na taarifa nyingi za kuanzishwa kwa magazeti mengi kuelekea uchaguzi wa 2010 na kwamba ofisi ya Msajili wa Magazeti (MAELEZO) imejaa maombi ambayo hayajashughulikiwa.

  Kaimu Mkurugenzi wa Maelezo, Raphael Hokororo amethibitisha kuwepo maombi mengi ya kuanzisha magazeti.

  Hata hivyo amesema maombi yote yanashughulikiwa. Hakuna agizo lolote la kusita kusajili magazeti.

  “Maombi yapo tunayashughulikia. Hakuna agizo la kusitisha usajili. Kwa hiyo hata mwenye magazeti mia akileta maombi mapya na ametimiza vigezo, tutamsajili,” amesema Hokororo.  [source Mwanahalisi]
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Na siku CCM ikiondoka ndio na Mwanahalisi naye anakufa njaa...
   
 11. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hapa sahau Matokeo ya ubunge ya 2010 CCM wanayajua yote, kwa maana watajikadiria viti vingapi na chama kipi kipewe viti vingapi na wapi. Wasilolijua ni kina nani wawape viti hivyo?, Sasa mtu kama Mkuchika lazima abakiziwe kiti chake na CCM kwa kuwa si vizuri kumtosa waziri aliye madarakani katika kulitetea jimbo lake. Hiyo ndiyo Bongo uchaguzi hasa Tanzania wanao CCM wenyewe katika kutafuta mgombea huku kwa wananchi ni Rubber stamp tu kuonesha dunia kuwa uchaguzi umefanyika.
   
Loading...