Kutenguliwa na kuvuliwa hadhi ya Ubalozi kwa Alphayo Kidata. Ufafanuzi wake kidiplomasia

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
KUTENGULIWA NA KUVULIWA HADHI YA UBALOZI KWA ALPHAYO KIDATA. UFAFANUZI WAKE KIDIPLOMASIA.

Alhamisi tarehe 08 Novemba, 2018 kulitolewa taarifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe juu ya kutenguliwa kwa uteuzi wa aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Canada, Alphayo Japani Kidata.

Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje ilisomeka hivi:

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli ametengua uteuzi na kumrejesha nchini aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada Bw. Alphayo Japani Kidata. Uamuzi huo umeanza tarehe 05 Novemba, 2018. Aidha Bw. Kidata ameondolewa hadhi ya Ubalozi."

Mwisho wa kunukuu.

Makala hii inaelezea sababu mbalimbali ambazo huweza kupelekea balozi kurejeshwa nyumbani,kutenguliwa na hata kuvuliwa hadhi ya Ubalozi.

Ili kuweza kuelewa kwa kina sababu zinazoweza kupelekea Balozi kurejeshwa nyumbani, kutenguliwa au kuvuliwa hadhi yake turejee kidogo kueleza kuhusu kazi za mabalozi na kile kilichowahi kumtokea Balozi Mstaafu Costa Ricky Mahalu mwaka 2007.

Kwa mujibu wa ibara ya tatu ya VCDR 1961 kazi za balozi zimeainishwa kama ifuatavyo:

(a) Kuiwakilisha nchi iliyomtuma (Sending State) ndani ya nchi husika itakayompokea (Receiving State).

(b) Kulinda maslahi ya nchi (dola) iliyomtuma ndani ya nchi iliyompokea pamoja na ya raia wake, bila ya kuathiri mipaka aliyowekewa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

(c) Kujadiliana (negotiating) na serikali ya nchi iliyompokea (katika mambo mbalimbali yenye maslahi baina yao).

Kifungu hiki kinawapa uwezo mabalozi kuingia na kusaini mikataba mbalimbali kwa niaba ya Marais wa nchi husika ama taasisi.

(d) Kuenenda na taratibu zote za kisheria katika kufuatilia yanayojitokeza ndani ya nchi iliyompokea na kutolea taarifa yale yanayojiri kwa nchi iliyomtuma.

Kanuni hii inawakataza mabalozi kujihusisha na masuala ya siasa ya ndani ya nchi.

(e) Kuendeleza mahusiano ya kirafiki kati ya nchi iliyomtuma (Sending State) na nchi na inayompokea, kuendeleza mahusiano ya kiuchumi, kiutamaduni na kisayansi.

KUITWA NYUMBANI/KUREJESHWA (RECALL) HUWAJE?

Katika muktadha wa diplomasia kurejeshwa ama kuitwa hutumika kuelezea balozi anapomaliza muda wake kule alipopelekwa au anapohitajiwa na Mkuu wa Nchi ama serikali kwa ajili ya mashauriano au kwa mashitaka yanayomkabili nchini mwake.

NI KWA SABABU ZIPI NA KATIKA MAZINGIRA GANI BALOZI HUWEZA KUITWA NCHINI MWAKE?

Kuna mazingira kadhaa ambayo huweza kupelekea balozi kuitwa au kurejeshwa nyumbani na nchi yake.

Hapa nitaeleza mazingira machache kwa lengo la kupeana elimu tu.

(1) KUHARIBIKA KWA HALI YA USALAMA WA NCHI HUSIKA.

Kwa mfano hali ya usalama katika nchi ya Libya iliwahi kupelekea nchi ya Uingereza kumwita nyumbani balozi wake kutokana na kuharibika kwa hali ya usalama Libya kwa kiasi kikubwa miaka ya 2011-2012.

Wengi tunakumbuka kuwa mnamo tarehe 11 Septemba, 2012 ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi ulilipuliwa na kusababisha kifo cha Balozi J. Christopher Stevens na maafisa watatu wa ubalozi huo.

Katika kuelezea tukio hilo la kuuawa kwa balozi Stevens ndani ya kitabu chake "How the South Won the Civil War. And How it Affects us Today (2013), Frank R. Barreca ameeleza:

"Just previous to this incident, the British recalled their ambassador because of a shooting incident" (Barreca, 2013:52).

Kwa tafsiri yangu:

"Wakati mfupi uliopita kabla ya tukio hili, Uingereza 'ilimwita' nyumbani balozi wao kutokana na tukio la mtu kupigwa risasi."

Hapa tunaona kuwa kuharibika kwa hali ya usalama wa nchi husika huweza kusababisha balozi kuitwa nyumbani kwa mashauriano.

(2) BALOZI KUMALIZA MUDA WAKE AU KUPANGIWA MAJUKUMU MENGINE NA NCHI YAKE.

Kuna wakati balozi anaweza kuitwa nyumbani kutokana na kumaliza muda wake wa kuhudumu katika nchi husika au kubadilishiwa majukumu au kwa suala lingine lolote kwa mujibu wa katiba ya nchi husika.

Tufahamu kwamba hati (Letter of Credence /Credentials) ambazo mabalozi huwa wanakabidhi kwa marais au wakuu wa taasisi na serikali husika licha ya kujumuisha taarifa zote muhimu kama majina yake,umri na weledi lakini pia huwa zinaonesha mwanzo wa kufanya majukumu yao katika nchi husika kwa maana ya tarehe ya kuanza hadi kumaliza majukumu yao.

(3) KUZOROTA/KUHARIBIKA KWA UHUSIANO BAINA YA NCHI NA NCHI

Kumbukumbu nzuri katika hili ni kurudishwa nyumbani kwa wanadiplomasia 23 wa Urusi waliokuwa Uingereza kufuatia tukio la kupewa sumu kwa Sergei Skripal (66) na bintiye Yulia Skripal (33) kule Salisbury mapema mwezi Machi mwaka huu.

(4) BALOZI KUSHINDWA KUFIKIA MATARAJIO YA NCHI AU TAASISI

Mabalozi wote hutakiwa kufanya kazi walizotumwa na nchi zao na kufikia malengo yaliyowekwa na dola husika.

Kwa mfano, serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imejikita katika sera ya viwanda.

Hapa mabalozi wetu wanatarajiwa wakaiuze sera hii ya viwanda kwa kuiunganisha na sera ya Mambo ya Nje ya sasa ya uchumi wa Kidiplomasia.

Tunatarajia kuona wawekezaji na wafanyabiashara wengi wakija kuwekeza katika maeneo ya viwanda vya aina mbalimbali kutegemea na rasilimali ilizo nazo Tanzania.

Balozi kushindwa kufanya jukumu hili tayari atakuwa amemuangusha Rais Magufuli ambaye amemteua.

Kushindwa kwa balozi kufikia viwango au matarajio huweza kusababisha mwakilishi huyo kuitwa kwa mashaurino au hata kutenguliwa katika nafasi hiyo.

Holmes na Rofe (2012: 230) waliandika katika kitabu chao, "The Embassy in Grosvenor Square. American Ambassadors to the United Kingdom 1938-2008" wakielezea kuitwa nyumbani kwa balozi John J. Louis Jr na Rais wa wakati huo Ronald Reagan kutoka ubalozi wa Marekani London, Uingereza alikokuwa akihudumu kuanzia mwaka 1981 hadi 1983.

Balozi John J. Louis Jr aliyefariki tarehe 15 February, 1995 akiwa nchini Uingereza alipewa maelekezo ya kutumia "Public diplomacy" ili kuyafikia maslahi ya taifa.

Holmes na Rofe (2012) wanasema:

"The problem for Louis was that this was a form of diplomatic representation of an old age."

Kwa tafsiri yangu:

"Tatizo la Balozi Louis lilikuwa kwamba hii (public diplomacy) ilikuwa ni aina ya uwakilishi wa kibalozi ya kizamani".

Kwa ufupi hapa public diplomacy ni aina ya diplomasia ambayo hutumia zaidi mawasiliano ya kirafiki na ya karibu na jamii aliyopo balozi kupitia kukutana, redio, luninga na hata magazeti kuweza kuiathiri jamii na kufikia maslahi ya taifa kwa kueneza propaganda mbalimbali.

Holmes na Rofe waliendelea kueleza:

"Assertive public diplomacy of this sort was a task that Louis found very difficult to perform and it became one of the main reasons for his recall as Ambassador in September, 1983" (Holmes na Rofe, 2012: 230).

Kwa tafsiri yangu:

"Msimamo wa diplomasia ya jamii wa aina hii ilikuwa ni kazi ambayo Louis aliiona ngumu sana kuifanya na ikawa miongoni mwa sababu kuu ya yeye kuitwa mwezi Septemba, 1983".

(5) MASHITAKA

Ili kufahamu kwa kina kuhusu namna mashitaka yanavyoweza kupelekea Balozi kuvuliwa hadhi ya Ubalozi ni vema kuelezea mashitaka yaliyowahi kumkabili Balozi Profesa Costa Ricky Mahalu aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa Jumamosi tarehe 17/Machi/2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alimrudishia hadhi ya Ubalozi Profesa Costa Ricky Mahalu baada ya kuwa amevuliwa mwaka 2007 kufuatia kufunguliwa mashitaka ya Jinai na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivyo tangu siku hadhi yake ilirejea na ataendelea kuitwa Balozi Profesa Costa Ricky Mahalu kama ilivyokuwa kabla ya mwaka 2007.

Kurejeshewa hadhi hii ya Ubalozi kwa Profesa Mahalu kulizua mijadala mingi ya watu kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii hapa nchini huku wengi wao wakitaka kufahamu uhalali wa kuvuliwa kwake hadhi hiyo mwaka 2007 na hatimaye kurejeshewa siku ile Jumamosi.

Profesa Costa Ricky Mahalu aliteuliwa kuwa balozi na aliyekuwa Rais wa awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Benjamin William Mkapa mwaka 1999 na mwaka 2000 alipangiwa kuiwakilisha Tanzania nchini Italia.

Balozi Profesa Mahalu alihudumu kama balozi wa Tanzania (Sending State) Rome, nchini Italia (Receiving State) kuanzia mwaka 2000 mpaka 2006 na baadae kufunguliwa mashitaka ya jinai na uhujumu uchumi sambamba na mfanyakazi mwingine wa Ubalozi Bi.Grace Alfred Martin katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mwaka 2007 kufuatia manunuzi ya Ofisi ya Balozi (Chancellery) tarehe 1/Octoba/2002.

Ilidaiwa kuwa Balozi Profesa Mahalu na Bi. Grace walituhumiwa kula njama na hatimaye kutumia nyaraka feki ili kuidanganya mamlaka na kuiingizia serikali hasara ya Euro 2,065,827.60 sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 2.5 za Tanzania.

Balozi Profesa Costa Mahalu na Bi.Grace walifunguliwa mashitaka sita tofauti kwa kile kilichoelezwa kuwa walikiuka Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2002 [Cap.329. R.E.2002], Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 [Cap. 16.R.E.2002] na Sheria ya Kupambana na Uhujumu Uchumi ya mwaka 2002 [Cap. 200.R.E.2002]

Ilidaiwa kuwa manunuzi ya jengo la ofisi hiyo ya balozi yalifanyika kwa mikataba miwili tofauti iliyotekelezwa siku moja lakini ikiwa na bei tofauti na pia kutohusisha baadhi ya taratibu za manunuzi za Serikali jambo ambalo lilielezwa kuwa ni kinyume na utaratibu halali wa manunuzi wa Serikali.

Katika utetezi wake Balozi Profesa Mahalu alielezea Mahakama kuwa alimjulisha Katibu Mkuu Kiongozi kipindi hicho Ndugu Martin Lumbanga juu ya manunuzi ya jengo hilo sambamba na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo Mheshimiwa Benjamin William Mkapa juu ya masharti ya mkataba wa manunuzi.

Alipoitwa Mahakamani kutoa ushahidi wake kwa upande wa utetezi Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa aliithibitisha Mahakama kuwa
alifahamishwa na Balozi Profesa Costa Ricky Mahalu kuhusiana na masharti yaliyowekwa na muuzaji kuhusu kulipwa pesa kupitia akaunti mbili tofauti za benki nae Rais Mkapa alitoa ruhusa ya manunuzi kufanyika kutokana na hitajio la haraka la ofisi ya ubalozi nchini Italia.

Hatimaye baada ya miaka mitano ya kuunguruma kwa kesi hiyo ilipofika tarehe 09/8/2012 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Ilvin Claud Mugeta (baadae alikuja kuwa Jaji) aliyekuwa akiendesha kesi hiyo wakati huo alimuachia huru Profesa Costa Ricky Mahalu na mshitakiwa mwingine Bi. Grace Alfred Martin baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa utetezi na hivyo kumkuta Profesa Costa Ricky Mahalu hana hatia yoyote kuhusiana na ununuzi wa jengo la Ubalozi pale Rome, Italia.

SABABU ILIYOPELEKEA BALOZI PROF. MAHALU KUVULIWA HADHI YA UBALOZI MWAKA 2007.

Kikubwa kilichopelea Balozi Profesa Mahalu kuvuliwa hadhi yake ya ubalozi mwaka 2007 ilikuwa ni kuruhusu taratibu za kimahakama kufuata mkondo wake.

Tunapaswa kufahamu kuwa mabalozi huwa na kinga dhidi ya mashitaka katika zile nchi zilizowapokea (Receiving States) na ambazo wanazofanyia majukumu yao.

Kwa mujibu wa Ibara ya 31 ya Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961 Balozi ana kinga dhidi ya mashitaka ya ndani ya nchi anapofanyia majukumu yake yaani Receiving State.

Ibara hii ya 31 (Article 31) ya Mkataba wa Vienna unaohusu Mahusiano ya Kidiplomasia (VCDR-1961) inaeleza hivi;

Balozi atakuwa na kinga dhidi ya mashitaka yote ya jinai katika nchi iliyompokea (Receiving State).

Pia, Balozi atakuwa na kinga dhidi ya mashitaka ya madai ama ya kiutawala katika nchi hiyo anayofanyia kazi isipokuwa kwa:

(a) Suala linalohusu mali binafsi ya balozi isiyohamishika ambayo ipo ndani ya mipaka ya nchi iliyompokea (Receiving State).

Isipokuwa kama balozi ataishikilia mali hiyo kwa niaba ya nchi iliyomtuma (Sending State) kwa malengo ya ubalozi.

(b) Jambo linalohusiana na balozi kumiliki kutoka kwa mtu mwingine/balozi ambalo ni la binafsi na halihusiani na nchi iliyomtuma.

(c) Jambo linalohusiana na weledi au masuala ya biashara ambalo balozi amelifanya nje ya majukumu yake ya kibalozi.

Ibara ya 37 (2) imeeleza waziwazi kuwa balozi hana wajibu wa kutoa ushahidi mahakamani, hivyo Mahakama za nchini Italia ama vyombo vya usalama vya nchi hiyo visingeweza kumuhoji ili kupelekea kushitakiwa kwake akiwa nchini humo.

Ibara hiyo hiyo ya 37 (3) imeendelea kueleza kuwa, balozi anaweza kuchukuliwa hatua kwa mambo binafsi ambayo niliyaeleza hapo juu katika (a), (b) na (c) ya paragrafu ya kwanza ya ibara hii.

Kwa msingi huo wa maelezo ya vifungu vya Mkataba wa Vienna tunaona kuwa isingekuwa rahisi kwa Balozi Profesa Costa Mahalu kushitakiwa pasina kuondolewa kinga dhidi ya mshitaka na hasa akiwa katika mipaka ya nchi anayofanyia majukumu yake.

JE KINGA ZA MABALOZI ZINA MIPAKA?

Kwa mujibu wa Ibara ya 37 ibara ndogo ya 4 ya Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961 inaeleza kuwa kinga ya mashitaka ndani ya mamlaka iliyompokea (Receiving State) hazimfanyi balozi kutoshitakiwa na mamlaka iliyomtuma (Sending State).

Kwa muongozo wa mkataba wa VCDR wa 1961 kinga na upendeleo wa mabalozi vinaishia katika mipaka ya nchi wanapofanyia kazi zao (Receiving States) tu na si pale wanapokuwa ndani ya mipaka ya nchi zao (Sending States) , hivyo mahakama za ndani za nchi wanapotoka mabalozi zina uwezo wa kuwashitaki kufuatia kuondolewa kinga zao.

NANI MWENYE MAMLAKA YA KUMVUA BALOZI HADHI YAKE?

Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961 umetoa muongozo wa nani mwenye mamlaka ya kumvua balozi hadhi yake.

Ibara ya 32 ibara ndogo ya kwanza ya mkataba huu inaeleza kuwa kinga ya mashitaka ambayo balozi hupewa huweza kuondolewa na nchi iliyomtuma (Sending State) tu.

Kwa mujibu wa maelezo ya ibara hiyo tunaona kuwa nchi iliyomtuma balozi kwenda kuwakilisha ndiyo yenye haki ya kuweza kumvua balozi hadhi yake.

Sasa swali hapa linakuja kuwa ni nani katika nchi iliyomtuma balozi ana mamlaka ya kumvua hadhi balozi?

Ili kufahamau nani mwenye mamlaka ya kumvua balozi hadhi yake ni vema kuitazama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa mujibu wa Ibara ya 36 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inaeleza ifuatavyo...

36 (2) Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu kushika nafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za idara na taasisi za Serikali, na watendaji wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa sera za idara na taasisi hizo katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, nafasi ambazo zimetajwa katika sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge kwamba zitajazwa na uteuzi unaofanywa na Rais.

Kutokana na ibara hii ya 36 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaona kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye mwenye Mamlaka ya kumteua mtu yeyote kuwa Balozi kuiwakilisha nchi na pia kama mwakilishi wa Rais katika nchi na vivyo hivyo ana haki ya kumvua hadhi ya ubalozi na hata kutengua uteuzi wa mtu yeyote endapo kutakuwa na hitajio la kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa hivyo basi, Ibara ya 36 Ibara ndogo ya pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajibu swali la nani mwenye mamlaka ya kumvua hadhi ya ubalozi na kutengua uteuzi wa balozi yeyote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililotokana na maelezo yaliyopo kwenye Ibara ya 32 Ibara ndogo ya Kwanza ya Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961 unaohusu Mahusiano ya Kidiplomasia iliyoeleza kuwa kinga na hadhi ya ubalozi huweza kuondolewa na nchi iliyomtuma balozi (Sending State).

Hivyo tunapaswa kufahamu kuwa kidiplomasia inapozungumzwa Sending State kimsingi huwa anazungumziwa mkuu wa Dola husika ambalo lilimteua balozi mtajwa na hivyo kwa mamlaka aliyo nayo kikatiba anaweza kumuondoa balozi huyo ama kumvua hadhi.

Baada ya kuthibitishwa na Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni muhimili mmojawapo wa Serikali kuwa hakuwa na hatia (Proven Innocent) Profesa Costa Ricky Mahalu alistahili kurejeshewa hadhi yake hiyo ambayo imeelezwa kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Uma kwamba mtu anakayehudumu katika cheo cha balozi ataendelea kuwa na hadhi ya kuitwa Balozi hata baada ya kustaafu utumishi wake Serikalini katika kipindi chote cha maisha yake.

Kwa kuangalia mfano huu wa Balozi Profesa Costa Ricky Mahalu tunaweza kuona kuwa mashitaka huweza kuwa sababu ya balozi kuvuliwa hadhi ili utaratibu wa kawaida wa kisheria uweze kufuata mkondo wake.

Kwa ujumla hizo ndiyo sababu ambazo huweza kusababisha balozi kurejeshwa nyumbani,kutenguliwa na hata kuvuliwa hadhi yake pale inapohitajika kama ilivyokuwa kwa Bw. Alphayo Japani Kidata aliyetenguliwa hadhi tarehe 05 Novemba, 2018.

*Abbas Mwalimu.*

*+255 719 258 484*

*Uwanja wa Diplomasia.*
 
Nashukuru kwa ufafanuzi mzuri tusubiri mbeleni
 
Kwa ufafanuzi huu ni dhahiri kuna mashtaka yanamsubiri atakokanyaga ardhi ya Tz
 
Aliitwa kitambo......ana wiki nzima yuko hapa labda atarudi Canada kwenda kukabidhi ofisi na kusafirisha familia yake
 
Back
Top Bottom