Gavana Balali Ajiuzulu!

Hata kama hajafanyiwa baya, kuna kila sababu kama binadamu kuweka mahali japo kwa watu wa karibu taarifa zote sahihi ili "WAKATI MWAFAKA" ukweli ujulikane. NAAMINI mambo mengi yana walakini na Watanzania tunajikuta tukiburuzwa bila kufanya utafiti wa kutosha. Upo uwezekano wa kesho kukuta magazeti mengi yakaandika habari ya Ballali, lakini bado najiuliza je, kuna NINI hadi tufikie mahali pa serikali KUPWAYA KIASI CHA KUENDESHWA NA KISANII? MUTAKUJA KUKUBALIANA NA MIMI KWAMBA kutatokea taarifa za KISANII SANA
 
Duh! Kaazi kweli kweli! Utafiti gani tena unaotaka ufanywe vya kutosha!? :confused:
Ushahidi wa kutosha uliandikwa magazeti na hao wahusika walishindwa kuupinga huo ushahidi. Ripoti ya BOT inafanyiwa usanii eti iko kwenye mchakato! Ama kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu! Halafu bado kuna watu wanataka kumtetea yule aliyekuwa kinara wakati $250 millioni zinapotea!
 
Kwanza nashukuru kwa hizi habari.

Lakini Jasusi sijui huo undani wa hii habari yako especially in Red, sijui ulikua karibu kiasi gani hadi ukaweza kupata habari hiyo.

Other´wise kama kwa namna moja ama ingine alikua poisoned na mtu yeyote katika kutaka kumtoa kafara. Ni muda mwafaka kwake kusema yaliyojiri ili hata ikitokea vinginevyo hao wahusika wa BOT waumbuke, vinginevyo na yeye yumo so anataka kufa na tai yake shingoni.

Ugua pole na karibu bongo tena wasikutishe, Bongo bado salama

BowBow, humu ndani mara kwa mara uwe unasubiri kwanza maana hadi mtu anapoamua kuweka hard facts kama hizo, ujue ana uhakika na kwa kuwa humu ndani wengi hatutumii majina halisi (japo mimi ni Halisi) kama linalosemwa unajua zaidi ama unajua kinyume chake toa maelezo yako kupinga ama kuunga mkono lakini si vyema sana kutaka kujua chanzo. Pengine muda si mrefu utaelewa ni kwanini hata yanasemwa. Jambo la msingi uwe na kumbukumbu ama uwe unafuatilia bila kukosa ili usipoteze mtiririko. Kila la kheir
 
Jambo la msingi uwe na kumbukumbu ama uwe unafuatilia bila kukosa ili usipoteze mtiririko.

Halisi
Chumvi, chumvi, chumvi inazidishwa ndio saana, maana kuna vitu vingine lazima uwe karibu especially unapo nukuu maneno ya mtu "nakushauri usirudi tena huko Bongo" maana yake ulikuwepo.

Otherwise msg delivered.
 
Quote: Halisi
Hata kama hajafanyiwa baya, kuna kila sababu kama binadamu kuweka mahali japo kwa watu wa karibu taarifa zote sahihi ili "WAKATI MWAFAKA" ukweli ujulikane. NAAMINI mambo mengi yana walakini na Watanzania tunajikuta tukiburuzwa bila kufanya utafiti wa kutosha. Upo uwezekano wa kesho kukuta magazeti mengi yakaandika habari ya Ballali, lakini bado najiuliza je, kuna NINI hadi tufikie mahali pa serikali KUPWAYA KIASI CHA KUENDESHWA NA KISANII? MUTAKUJA KUKUBALIANA NA MIMI KWAMBA kutatokea taarifa za KISANII SANA

Duh! Kaazi kweli kweli! Utafiti gani tena unaotaka ufanywe vya kutosha!?
Ushahidi wa kutosha uliandikwa magazeti na hao wahusika walishindwa kuupinga huo ushahidi. Ripoti ya BOT inafanyiwa usanii eti iko kwenye mchakato! Ama kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu! Halafu bado kuna watu wanataka kumtetea yule aliyekuwa kinara wakati $250 millioni zinapotea!

Bubu ataka Kusema, Siamini kama kuna mtu anaweza kumtetea mhalifu hata mara moja. Na kama unasoma kwa kufuata mstari, utakuta nimesisitiza utafiti lazima uendelee.

Watupe ripoti ya BoT, watupe ripoti ya PCCB (japo yaweza kuwa kama ya Richmond), watupe ile ya polisi na TIS waliyofanya pamoja, lakini huyu mtu (gavana) naye alikua anafanya kazi chini ya mtu (Mkapa na JK) sasa je, kuna mambo alifanya kwa amri? je, kuna waliomhujumu? Je, kuna siri gani? Je, CCM walichota ngapi kwa uchaguzi? Je kina fulani nao walichota ngapi kwa kusingizia CCM? na walitia ngapi ndani? Je, MWananchi Gold ambayo kina Warioba na CCM (jina) wako ndani BoT, walilazimishwa na nani na sasa ina hali gani? na kadhalika.

Hapo ndipo tunataka kujua ukweli na kama ni majungu pia tuambiwe lakini nayeye asema asiogope. Hapo ndipo tunatakiwa kupata undani.
 
Chumvi, chumvi, chumviinazidishwa ndio maana, maana kuna vitu vingine lazima uwe karibu especially unapo nukuu maneno ya mtu "nakuhsauri usirudi tena huko Bongo" maana yake ulikuwepo otherwise msg delivered.

Kwa taarifa yako HAKUNA CHUMVI... usiwe na haraka.. nimekwambia subiri na ufuatilie. Una haraka ya nini?
 
Habari za kuthibitishwa zinasema kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Daudi Balali amejiuzulu wadhifa wake huo kutokana na sababu za kiafya. Gav. Balali alikuwa ameenda Marekani kwenye jimbo la Massachusetts jiji la Boston ambako alikuwa ameenda kufanya upasuaji. Gav. Balali katika barua yake kwa Rais amesema kuwa kutokana na "sababu za kiafya" hatoweza kuendelea na wadhifa huo. Ikumbukwe kuwa Gav. Balali aliandamwa na tuhuma nyingi katika chombo hicho cha Benki Kuu kwa muda mrefu sasa na watu wengi wakiwemo viongozi wa upinzani wamekuwa wakimtaka Rais amwajibishe.

Hata hivyo wachunguzi wa mambo ya kisiasa na wale waliokuwa wanafuatilia suala hilo la tuhuma za ufisadi wanatambua kuwa katika sakata hilo Bw. Balali hakuwa peke yake na kuna dalili za vyombo na watu wengine mashuhuri kuhusika katika ufisadi huo na hivyo yeye Balali kuwa ni mtolewa kafara wa kwanza.

Kufuatia habari za kujiuzulu kwake ambazo KLH News ilianza kuzisikia tangu jana, kuna uwezekano mkubwa kabisa wa Gavana huyo kutoweza kurudi nyumbani kabisa kutokana na sababu "mbalimbali" ambazo hazitaweza kuzuilika.

M. M.
 
hamna lolote aje atueleze vyema kuhusu mabilioni yetu sio kutuletea habari zisizo kuwa kabisaaaa?
kwanza hatujui wala hatujaambiwa hayo matatizo yake ya kiafyani yapi waweza kuta ni...........
 
BowBow, humu ndani mara kwa mara uwe unasubiri kwanza maana hadi mtu anapoamua kuweka hard facts kama hizo, ujue ana uhakika na kwa kuwa humu ndani wengi hatutumii majina halisi (japo mimi ni Halisi) kama linalosemwa unajua zaidi ama unajua kinyume chake toa maelezo yako kupinga ama kuunga mkono lakini si vyema sana kutaka kujua chanzo. Pengine muda si mrefu utaelewa ni kwanini hata yanasemwa. Jambo la msingi uwe na kumbukumbu ama uwe unafuatilia bila kukosa ili usipoteze mtiririko. Kila la kheir

Halisi, tumekupata barabara tokea mwanzo, na hasa baada ya yale yaliyoongezwa na Mkjj na kiranja, mambo yalianza kunyooka vizuri.
 
Bowbow,
Huhitaji kujua ukaribu au umbali wangu. Kama nilichosema ni uongo kamwulize RO, anisute Tena kuna mengi tu aliyosema ambayo nitayasitiri kwa sasa. Halisi, thanks!
 
Huyu Bwana hata akifa ni sawa tu

Maana tangu alipoondoka Tz alisema anaumwa na ni routine checkup
alizokuwa anafanyiwa But ghafla akasema atafanyiwa operation na sasa tunaambiwa mahututi pamoja na kuresign.

Cha kushangaza sio serikali, BoT wala familia yake inayosema chochote kuhusiana na ugonjwa unaomsumbua. Je sio danganya toto ya kukwepa kujibu tuhuma?

Kuna mahali kwenye thread moja walisema huyu bwana ndio kakimbia nchi na sasa tunaanza kuona ukweli.

Je kwa nini tusiamini kwamba yeye ni mmoja wapo wa mamafia wanaotumiwa na WB, IMF na mamafia wengine kuibia nchi masikini

Nitamuombea Dua Afe kabisa
 
Hapana, hatutaki afe kabla hajatoa ukweli wote ulivyo. Atupe 'details' zote za madeal yalivyofanywa na wahusika wote, bila kuficha kitu. Akifanya hivyo tutamsamehe, na kumtukuza kwa ujasiri wake huo.
 
Bowbow,
Kama unazo kumbukumbu sahihi, hata wakati Mwalimu anaelekea London 1999 serikali ilitangaza kuwa anakwenda "routine medical check up." Hata pale hali yake ilipokuwa inazidi kuwa mbaya Ikulu ya Mkapa ilikuwa inatuambia kuwa anaendelea vizuri na matibabu. Hiyo inaitwa "lugha ya kiserikali." You have to read between the lines.
 
Habari za kuthibitishwa zinasema kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Daudi Balali amejiuzulu wadhifa wake huo kutokana na sababu za kiafya.

Je taarifa ya uchunguzi itatoka tena baada ya Ballali kujiuzulu? Au ndio imefagiliwa chini ya zulia?
 
Bowbow,
Kama unazo kumbukumbu sahihi, hata wakati Mwalimu anaelekea London 1999 serikali ilitangaza kuwa anakwenda "routine medical check up." Hata pale hali yake ilipokuwa inazidi kuwa mbaya Ikulu ya Mkapa ilikuwa inatuambia kuwa anaendelea vizuri na matibabu. Hiyo inaitwa "lugha ya kiserikali." You have to read between the lines.

Nasikiliza

Maana Jana alianza Hasara, baadae leo akaja Halisi, muda si Mrefu akaja M. Mkijiji. Nasubiri huo mririko wa "lugha ya kiserikali" kama Xmass itafika au laa ili neno la HASARA litimie
 
Back
Top Bottom