Gari iliyobeba bangi yapata ajali Pwani

a0d41517714b11ea4aacdb3244b0215b.jpg
181699e91d8753db2069b73085ea32a4.jpg

Tan 7.5 ziliminywa humo
 
Majeruhi wawili wa ajali ya gari wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Pwani wakihusishwa na usafirishaji wa bangi magunia 7 yenye uzito unaodaiwa kuwa Kg 7,500.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shana ameiomba mahakama kutoa adhabu kwali kwa watuhumiwa hao ikiwemo kutaifisha gari hiyo iliyotumika kusafirisha magunia hayo

Gari hiyo yenye namba za usajili T847 DHD aina ya IST ilikamatwa majira ya saa 5 asubuhi Kwa Mathias Wilayani Kibaha askari wakiwa doria walipata taarifa za gari kupata ajali kwa gari hiyo na kuwakoa majeruhi, walipoikagua gari hiyo waliikuta na magunia 7 ya bangi.



Chanzo: Mwananchi

Asamehewe bure kwa kweli hata fuso nyingine nyingi ni tani 7 tu maximum
 
Acha ubishi wewe !IST za Tz zinabeba bhana !huku mbona kawaida tu kubadilisha manamba?trillion 400 =300 bilion.
mwingine kaingia inyumba ikuu sugar kaikuta 5000 tzs per kg yeye kaishusha mpaka 2400per kg ina maana 5000 = 1600
kwa tz namba hazina maana
Ohoo
 
Pamoja na mapungufu ya kiuandishi yaliyojitokeza, hoja yangu ni hii, hivi mpaka nyakati hizi kuna watu wanathubutu kufanya madudu hayo, kama kubeba bangi, mimba watoto wa shule, meno ya nani yule kweli mchana kweupe peeee?
 
Muandishi hana kosa mana somo la hesabu kwake na vipimo avipo sawa tatizo limeanzia kwa aliemuandikia report polisi na polisi mwenye mana ndo wenye kushuudia ajali na kupima nilikua nataka kununua fuso basi tena bora ist cheap na mzigo ubeba sawa na fuso
 
Mtu ukishapakia ile kitu bangi, unafanya chochote. Kwahiyo ninaamini kabisa hiyo ist kubeba 7 ton.
 
Daah hapo mchawi ajali tu lakini mzigo ulikua ushafika mjini daslam. Enewei nahisi dereva alisinzia baada ya uchovu wa safari usiku kucha kutoboa toka musoma mpaka daslam si mchezo.
 
Hii habari imekaa kimkurupukomkurupuko.
Sawa tuchukulie Sio'Tani 7,500' kama ilivyonukuliwa.

Na usahihi Iwe ni Gunia Saba,

Jamani hivi kweli unaweza kuweka Gunia Saba kwenye IST, Kweli?
Au hiyo Gari walikongoroa viti?
Tutumie Akili wakati mwingine.

Chanzo bangi, Habari bangi, Mhabarishaji bangi
Mnukuu habari bangi, Bangi bangi bangi inakuwa BANGIIIIII.
 
Ndio matatizo ya kutesti vizibiti,huyu RPC inaelekea alishtua kidogo kitu cha musoma
 
Pamoja na mapungufu ya kiuandishi yaliyojitokeza, hoja yangu ni hii, hivi mpaka nyakati hizi kuna watu wanathubutu kufanya madudu hayo, kama kubeba bangi, mimba watoto wa shule, meno ya nani yule kweli mchana kweupe peeee?
Jasiri haachi asili mkuu,Mimi juzi tu nimebeba fuko la ganja kutoka dakawa hadi bongo,tena bila wasiwasi na nimepishana na polisi kibao barabarani
 
Gunia au viroba? Hata nyasi za ngombe kunia saba hazitoshi kwenye ist, achulia uzito tajwa!
 
"Walipokagua wakaona bangi" hahaha. Hawa jamaa bwn hua ni watu wa kada flan ivi ya kipekee sana.
Unahutaji kukagua IST ili uone Bangi 7,500kg teh
 
Najilaumu sana kwanini sikusoma hesabu, Kuna siku nitadanganywa hivi hivi Tani 7.5 kwenye IST?

Yaani ina maana ungeweka Tembo wawili size ya Kati kwenye hilo gari lingeondoka?

Tani Saba IST? Yaani ina Maana ingebeba watu wa kilo 100 kila mmoja ingebeba watu 70? Tani 7.5?
 
Back
Top Bottom