kivyako
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 14,342
- 12,067
Ili kumuonyesha mkubwa kuwa watu wanachapa kazi7,500kg yaani Tani 7.5, Dah hiyo IST kiboko. Kuna data imepikwa hapa.
Ili kumuonyesha mkubwa kuwa watu wanachapa kazi7,500kg yaani Tani 7.5, Dah hiyo IST kiboko. Kuna data imepikwa hapa.
Gari yenyewe ni tani moja kamilindo mjue uandishi kipaji ....tani 7.5 au kilo 7500 za bangi kwenyi IST zitakaa wapi ..... gari yenyewe tani mbili aifiki afu ibebe tani 7.5 .....
Sasa hutaki au izo taarifa zimethibitisha na RPC na kwa mujibu wa nchii RPC akithibitisha jambo basi ni kweli.Yaani IST ibebe mzigo wa tani 7 huu ni utani au?
Hahaha sawa mkuuSasa hutaki au izo taarifa zimethibitisha na RPC na kwa mujibu wa nchii RPC akithibitisha jambo basi ni kweli.
Hivyo hatuna budi kukubaliana na miujiza hiyo
Labda bangi ndio ilikuwa imebeba gari.Kumbe bangi ni nzito kiasi hicho?
Yani magunia saba tu ya na kilo 7,500
Majeruhi wawili wa ajali ya gari wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Pwani wakihusishwa na usafirishaji wa bangi magunia 7 yenye uzito unaodaiwa kuwa Kg 7,500.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shana ameiomba mahakama kutoa adhabu kwali kwa watuhumiwa hao ikiwemo kutaifisha gari hiyo iliyotumika kusafirisha magunia hayo
Gari hiyo yenye namba za usajili T847 DHD aina ya IST ilikamatwa majira ya saa 5 asubuhi Kwa Mathias Wilayani Kibaha askari wakiwa doria walipata taarifa za gari kupata ajali kwa gari hiyo na kuwakoa majeruhi, walipoikagua gari hiyo waliikuta na magunia 7 ya bangi.
Chanzo: Mwananchi
Acha ubishi wewe !IST za Tz zinabeba bhana !huku mbona kawaida tu kubadilisha manamba?trillion 400 =300 bilion.