Gari iliyobeba bangi yapata ajali Pwani

Gari iliyobeba bangi yapata ajali Pwani

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
Majeruhi wawili wa ajali ya gari wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Pwani wakihusishwa na usafirishaji wa bangi magunia 7 yenye uzito unaodaiwa kuwa Kg 7,500.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shana ameiomba mahakama kutoa adhabu kwali kwa watuhumiwa hao ikiwemo kutaifisha gari hiyo iliyotumika kusafirisha magunia hayo

Gari hiyo yenye namba za usajili T847 DHD aina ya IST ilikamatwa majira ya saa 5 asubuhi Kwa Mathias Wilayani Kibaha askari wakiwa doria walipata taarifa za gari kupata ajali kwa gari hiyo na kuwakoa majeruhi, walipoikagua gari hiyo waliikuta na magunia 7 ya bangi.

Chanzo: Mwananchi
 
Majeruhi wawili wa ajali ya gari wanashikiliwa na jeshila polisi mkoani Pwani wakihusishwa na usafirishaji wa bangi magunia 7 yenye uzito wa Kg 7,500

Kmanda wa Polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shana ameiomba mahakama kutoa adhabu kwali kwa watuhumiwa hao ikiwepo kutaifisha gari

Yaani tani 7.5 kweli? Alikusudia kilo 750??
 
bahati mbaya ilikuwa upande wao, alafu utaifishe gari kisa bangi mambo gani hayo? je basi likibeba mzg huo mtalitaifisha pia
 
RPC kuiomba mahakama itoe adhabu kali kwa "watuhumiwa" tafsiri yake naitafuta. Alikuwa mahakamani au alikuwa anaongea na wanahabari? Maombi hayo kwa nini asisubiri mahakama ili awasilishe?
 
Magunia saba (7) ndani ya IST ni habari ya kutilia shaka sembuse tani 7.
Kuna makosa mengi ktk uwasilishaji taarifa hii kwa umma.
 
Majeruhi wawili wa ajali ya gari wanashikiliwa na jeshila polisi mkoani Pwani wakihusishwa na usafirishaji wa bangi magunia 7 yenye uzito wa Kg 7,500

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shana ameiomba mahakama kutoa adhabu kwali kwa watuhumiwa hao ikiwemo kutaifisha gari hiyo iliyotumika kusafirisha magunia hayo

Gari hiyo yenye namba za usajili T847 DHD aina ya IST ilikamatwa majira ya saa 5 asubuhi Kwa Mathias Wilayani Kibaha askari wakiwa doria walipata taarifa za gari kupata ajali kwa gari hiyo na kuwakoa majeruhi, walipoikagua gari hiyo waliikuta na magunia 7 ya bangi yenye uzito wa Kg 7,500

Chanzo: Mwananchi

Ist inabeba mzigo kg 7500 which is equal to 7.5tones?? Humamayuuu nyieee
 
Majeruhi wawili wa ajali ya gari wanashikiliwa na jeshila polisi mkoani Pwani wakihusishwa na usafirishaji wa bangi magunia 7 yenye uzito wa Kg 7,500

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shana ameiomba mahakama kutoa adhabu kwali kwa watuhumiwa hao ikiwemo kutaifisha gari hiyo iliyotumika kusafirisha magunia hayo

Gari hiyo yenye namba za usajili T847 DHD aina ya IST ilikamatwa majira ya saa 5 asubuhi Kwa Mathias Wilayani Kibaha askari wakiwa doria walipata taarifa za gari kupata ajali kwa gari hiyo na kuwakoa majeruhi, walipoikagua gari hiyo waliikuta na magunia 7 ya bangi yenye uzito wa Kg 7,500

Chanzo: Mwananchi

7,500kg yaani Tani 7.5, Dah hiyo IST kiboko. Kuna data imepikwa hapa.
 
mleta taarifa kwa nini usitulie ukaleta vitu vilivyoshiba/kamilika wakati mwingine huwa mnakera sana japo mnatuhabarisha mambo mengi.

sasa ni lini IST imeanza kubeba magunia saba 7!!!
 
Mi shida yangu ni hao wanahabari walikuwa kwenye hiyo press conference, hivi hawawezi kuhoji details wanazopewa?? wanachukuwa kila detail bila kuitafakari??? Hivi katika hesabu ya kawaida kabisa, gunia moja lina weza kuwa na kilo 1000+ kweli?? Shame on you...😡😡
 
Aiyaa, huyu bwege nilishamfunza jinsi ya kufunga mzigo yeye kapuuza muongozo, ona sasa gari imelewa imeanguka[emoji35] [emoji35]
 
Back
Top Bottom