Gamboshi: Makao makuu ya wachawi Kanda ya Ziwa

Gamboshi ni moja ya vijiji vilivyopo wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu. Kwa Wanyantuzu huko.

Kijiji hiki kinasifika kwa kuwa na wachawi wakali sana hadi baadhi ya watu kukiita kuwa ndo makao makuu ya wachawi na uchawi kwa kanda ya ziwa.

Kama video hii ya kwanza inavyoeleze, Gamboshi kipo kama kilometa 44 hivi kutoka Bariadi mjini.

Mimi natokea Ikungulyabashashi [hapo kwenye video dakika 1:56 sikia jinsi Ikungulyabashashi inavotamkwa], ambapo si mbali kivile na Gamboshi.



Gamboshi nimeshafika mara nyingi tu. Nina ndugu wengi tu huko. Habari na sifa za Gamboshi hekaya tu.

Hazina ukweli wowote. Kuna watu ukiwakuta wanaiongelea Gamboshi unaweza kudhani Gamboshi ni NYC.

Wapo ambao huwa wanadai huko Gamboshi kuna magorofa makali sana, kuna mabarabara mazuri kama ya Marekani, na mengineyo mengi mazuri lakini eti kwa wengine ambao sio wachawi hawawezi kuyaona.

Huo ni uongo. Gamboshi ni kijiji cha kawaida mno na hakina tofauti na vijiji vingine vya Tanzania.

Tatizo kubwa la Gamboshi ni ujinga tu. Na ndo maana hata maendeleo [kwa viwango vya Tanzania] ni madogo mno.


Kwa mfano, zahanati ipo lakini idadi ya watu wanaoenda kutibiwa hapo ni chache mno. Watu wakiumwa wanaenda kwa 'Nfumu' [Wasukuma wenzangu mtakua mnajua nfumu ni nini].

Shule ya msingi ipo, ya sekondari ipo, lakini ndo hivyo tena. Imani potofu zishawapotosha watu kiasi cha kutokuona umuhimu wa elimu ya darasani.

Halafu inadaiwa eti karibu kila mwana-Gamboshi ni mganga wa kienyeji:D. Binafsi sidhani kama watu wapatao 4,000 waishio huko wanaweza karibu wote kuwa waganga/ wachawi.

Jionee mwenyewe mazingira ya Gamboshi na wasikie wasikie kwa masikio yako wana-Gamboshi.



hapo kwenye bold ndo ingekuwa hitimisho langu....
 
Nilifika bariadi kikazi hivi karibuni....kunamambo ambayo yalinidhangaza sana
1.siku ya mnada....ukichelewa kutoka mnadani au ukienda mnadani majira ya saa 1 usiku.... utakuta fisi kibao na utajiuliza wametoka wapi ilihali eneo la mnada lipo bariadi mjini
2.mwanzoni nilibisha sana mauza uza ya gamboshi believe me nilipotea na msafara wangu hapo....lengo lilikua ni kuitembelea zahanati hiyo...sikufanikiwa....nilipofika maeneo ya gamboshi tulizunguka na gari letu kuitafuta zahanati kwa dk kama 40....tukashitukia hilo chezo tukaamua kurudi na nilipanga kesho yake nirudi tena....baada ya kutafakari kwa kina sikurudi......gamboshi is real
 
Nilifika bariadi kikazi hivi karibuni....kunamambo ambayo yalinidhangaza sana
1.siku ya mnada....ukichelewa kutoka mnadani au ukienda mnadani majira ya saa 1 usiku.... utakuta fisi kibao na utajiuliza wametoka wapi ilihali eneo la mnada lipo bariadi mjini

Unazungumzia ule mnada wa kila Jumanne pale Bariadi mjini?

Hao fisi mimi sijawahi kuwaona hata siku moja na huwa nikiwa Bariadi sikose kwenda mnadani kula nyama choma na kunywa Balimi.
 
Duh, mi nilikuwa najua gamboshi ipo kuzimu. Kumbe ipo Tz hapahapa. Natamani nikutane na mtu anayetokea gamboshi ili nimhoji vizuri maswali
 
Duh, mi nilikuwa najua gamboshi ipo kuzimu. Kumbe ipo Tz hapahapa. Natamani nikutane na mtu anayetokea gamboshi ili nimhoji vizuri maswali

Si rahisi kukutana na mtu wa Gamboshi kwa sababu hata kama ukikutana naye, yeye kusema anatoka huko inaweza kuwa mgogoro.
 
Hicho kijiji kimenikumbusha miaka Ya utotoni nilienda kwenye msiba kijiji kimoja kinaitwa isulilo huko usukumani kuna mambo sana,kilichonifurahisha kuna matunda fulani Ya misituni yanaitwa ngubaru niliyapenda sana sikutaka hata kurudi mjini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom