soskeneth
JF-Expert Member
- Jul 2, 2016
- 583
- 235
Kijiji cha Gamboshi, ambacho kwa miongo mingi kimekuwa kikiogopwa kama makao makuu ya wachawi na uchawi wa kutisha.
Kimekuwa ni kijiji kinachotafutwa na watu
wanaotaka utajiri na uongozi kwa njia ya mkato.
Mwandishi wa habari hii amejikuta akipata wakati mgumu kutoka kwa wasakamali na uongozi tangu alipoandika habari za kijiji hicho katika vyombo vya habari.
Haileweki ni vipi watu hao waliweza kupata
namba yake ya simu kwani kati ya March 12 hadi May 28, aliweza kupigiwa simu na
watu 19, na 11 kati ya hao wakitaka awapeleke au awatajie majina ya ‘Wazee’ maarufu watakaowawezesha kufanikisha malengo yao wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
Huku 8 waliobaki wakiwa ni wachimba madini ambao wanaamini
wazee wa Gamboshi wanaweza kuwaonesha madini yalipo.
“Nasikia wewe ndiye unawapeleka watu
Gamboshi, tafadhali nisaidie nikawaone ili
waninyoshee mambo yangu. Mimi niko Mererani Arusha,” alisema mmoja wa watu hao katika simu aliyompigia Mwandishi wa habari hii.
Mwingine aliyejitambulisha kuwa ni mkazi wa Dodoma alisema: ” Bwana naomba nisaidie nifike Gamboshi ili wataalam hao wanisaidie katika uchaguzi ujao, kuna jimbo la uchaguzi nalowania".
Kwa mujibu wa wakazi wa kanda ya ziwa, Gamboshi si mahali pa kupakimbilia kwani kijiji hiki kimetajwa kuwa na mengi ya kutisha kiasi cha kuitwa ni ‘jiji
la miujiza’.
Moja ya visa vilivyowahi kuripotiwa na ambavyo viliwaogopesha sana watu ni pamoja na viongozi wa kiserikali na kichama kunyolewa nywele
sehemu za siri, kujikuta wamelazwa nje.
“Gamboshi si mahala pa kutembea kwa sababu ukienda kamwe hutarudi, nawafahamu vema wakazi wa huko si rafiki kabisa na watu wengine,” alinionya Epaphra Swai, mkaguzi wa
viwanda vya kuchambua pamba mkoani Simiyu.
Kijiji hicho ambacho ni nadra sana kutembelewa, kimepata umaaurufu mkubwa ndani na nje ya
nchi kama kama kitovu cha uchawi na
wachawi wanaoweza kufanya miujuza, hali
ambayo imekifanya kijiji hicho kupitwa na
mkondo wa kimaendeleo kitaifa.
Hata hivyo baada ya kukitembelea kijiji hicho, wakazi wake walidai kuwa mengi
mabaya yanayosemwa dhidi yao ni ya kuzusha tu, na chumvi nyingi kuongezwa, hali ambayo imeathiri maendeleo ya kijiji chao.
“Sisi ni wakulima wakarimu wa pamba, mahindi na mpunga. Yote mnayoyasikia kwamba sisi ni magwiji wa uchawi ni uvumi uliotiwa chumvi nyingi. Tunamuomba Rais wetu kwa kushirikiana
na mbunge wetu, Andrew Chenge atusadie
kulisafisha jina letu,” alisihi Zephania Maduhu, afisamtendaji wa kijiji cha Gamboshi.
Maduhu pamoja na wanakijiji wenzake walidai kuwa hofu iliyoenezwa kitaifa na kimataifa juu ya uchawi uliovuka mipaka wa kijiji cha Gamboshi umesababisha madhara makubwa kwa kijiji hicho
kiasi cha kutengwa na jamii yote ya Watanzania.
“Hakuna aliyetembelea kijiji hiki kwa miaka mingi sana. Hata sisi tunapotoka nje ya kijiji wengi hawataki kutusogelea wakiamini
tuwadhuru, ” alisema Musa Deus, 26, mmoja wa wakulima walionufaika sana kilimo cha mkataba kijijini Gamboshi.
Kwa mujibu wa afisa mtendaji,
tangu Uhuru hakuna kiongozi yoyote wa kitaifa aliyewahi kukanyaga kijijini hapo. Mtu wa pekee aliyewahi kuzuru kijijini hapo ni mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge, ambaye alifika kijijini hapo mwaka 2010 wakati akifanya kampeni
za ubunge.
“Tume ya katiba ilitupita, mwenge wa Uhuru nao haujawahi kupita hapa. Tuko kisiwani mbali na Watanzania wengine,” aliseman afisa mtendaji.
Mijini na vijijini, kumekwepo na ubishani mkali kuhusu ni mkoa gani unaokimiliki kijiji hicho ambacho baadhi ya wakazi wake wanadai kuwa miongoni mwa vioja vyake ni mauzauza yanayoweza kuifanya Gamboshi ionekane kama jiji la New York au London wakati wa usiku.
Wakazi wa Shinyanga wanadai kuwa Gamboshi iko wilayani Magu, mkoa wa Mwanza, wakati wale Mwanza wakidai kuwa iko mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa afisa mtendaji, Gamboshi iko katika wilaya Bariadi, karibu na mpaka
unaotenganisha na wilaya ya Magu iliyoko
mkoani Mwanza.
“Tunaomba sana ndugu mwandishi waambie Watanzania kuwa mengi wanayoyasikia kuhusu Gamboshi si kweli kabisa, tunawakaribisha wote
hapa waje kufanya biashara na sisi, waoleane na vijana wa Gamboshi kama wafanyavyo katika vijiji vingine. Sisi ni binadamu wema,” alidai mkulima Malimi Kidimi.
Lakini si wananchi tu wanaogopa kufika hapo hata baadhi ya makampuni ya ununuzi wa pamba.
“Kampuni Billlchard, moja ya mawakala wa kilimo cha mkatabaka alishindwa kutuletea mbolea hapa na badala yake akaenda kuibwaga katika kituo cha Polisi Bariadi kwa kile ambacho wafanyakazi wake walidai ni kuhofia usalama
wao,” alidai afisa mtendaji na kulaumu watu.
Wanaoneza hofu hiyo kuwa ina athari kubwa kwa kijiji na watu wake.
Kwa mujibu wa afisa mtendaji si kweli kabisa kila mtu ajaye Gamboshi hupotea moja kwa moja, huuliwa au kugeuzwa nyoka au fisi kama wengi wanavovumisha.
“Pigo tulilopata kutokana sifa mbaya
tuliyobambikiziwa haisemeki ila ni madhara
makubwa tunayapata kutokana na kutengwa na jamii. Wanakijiji wa Gamboshi ni masikini kwa sababu mkondo wa maendeleo na mageuzi umepita mbali sana nao,” alidai mtendaji huyo.
Akifafanua kiini cha chuki na hofu waliyonanayo wananchi juu ya kijiji cha Gamboshi, afisa mtendaji huyo alidai kuwa
"hapo zamani ilitokea
kijana mmoja kutoka kijiji jirani cha Ngasamwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana mzaliwa wa Gamboshi. Siku moja kijana huyo alikuja kijijini hapo akimsandikiza mpenziwe na kisha kushindwa kurudi kijijini mwake. Juhudi za kumsaka kijina huyo hazikuweza kuzaa matunda hadi aliponekana kichakani baada ya siku saba huku ngozi yake imebadilika na kuwa nyeupe.
Alipouliza alifikaje kichakani hapo, kijana huyo alijibu kuwa ameteremshwa na ndege ya JET kutoka Ulaya na baada ya hapo kijana huyo alirukwa na akili kiasi cha kushindwa kuuongea. Ilibidi achukuliwe na kupelekwa kutibiwa na waganga wa jadi na akapona baada ya matibabu ya zaidi ya mwezi mmoja,” alisimulia
afisa huyo, na kudai kuwa, kisa hicho
inawezekana kuwa na ukweli kidogo sana, lakini kuongezwa chumvi nyingi kupita kiasi.
Kwa mujibu wa Maduhu, tangu siku hiyo
Gamboshi ikatangazwa uadui na vijiji vingine kiasi cha kukifanya kuogopwa na kuchukiwa mno.
“Uvumi kama Gamboshi inaweza kuonekana kama Ulaya au Marekani ilianzia hapo na umendelea kurudiwa kwa namna ambayo imekifanya kijiji hiki kiitwe jiji la maajabu,” alidai afisa huyo.
Kwa maoni ya Malimi Kidima, Wana Gamboshi wangeweza kuitangazia dunia kuwa wao ni wasafi lakini, kwa miaka mingi wamekosa jinsi ya kuifanya sauti yao isikike.
“Redio ndiyo njia ya pekee inayotufanya sisi tuwe karibu na dunia. Hakuna mwenye luninga hapa kwa sababu hakuna umeme. Tunasoma magezeti kupitia vichwa vya habari vinavyosomwa kila siku redioni,” alidai Maduhu.