Abul Aaliyah
JF-Expert Member
- Nov 8, 2016
- 7,339
- 5,553
Hiv upo serius kweli????Ni lini mayahudi yalikuwa na njema zaidi ya kuendelea.kuchukua ardhi kila kukichaSiungi mkono kuuawa kwa mtu yeyote asiye na hatia, au hata mwenye hatia lakini hatia yake haina hatari kwa maisha ya watu wengine.
Kila nikitizama vifo, hasa vifo vya wale watoto wadogo wa kule Gaza, naumia sana moyoni, maana angalao una uhakika kuwa watoto wale hawana hatia yoyote. Hali kadhalika wale wapalestina wasio na mafungamano yoyote na Hamas.
Lakini kuna tofauti kati ya hawa magaidi wa Hamas na askari wa Israel. Askari wa Israel wanawatafuta Hamas, lakini katika kutafuta huko ndiko kunasababisha hata wasio Hamas kuuawa, ama kwa kukosa umakini ama kwa sababu ya mbinu za magaidi ya Hamas kujichanganya na raia.
Siamini kuwa bila ya shambulio la Hamas, Israel wangeenda kuwaua Wapalestina. Hata maisha ya Wapalestina yamekuwa kama ya gereza kutokana na vitendo vya hawa magaidi. Hapo mwanzo haikuwa hivyo.
Wapalestina, hata kama kuna haki wanaidai au kuitafuta, kuna njia sahihi za kuidai ambazo zingewapa mafanikio kuliko kuamini eti hawa magaidi wanapigania haki ya Wapalestina. Mbona uongozi wa Ramallah chini ya Arafat ulipofikia makubaliano na Israel juu ya kuundwa kwa taifa la Palestina, haya magaidi ya Hamas yakapinga na kuanzisha vita dhidi ya uongozi wa Ramallah, kwa madai kuwa kwa nini wanafanya mazungumzo na wayahudi? Kwa hiyo magaidi ya Hamas, hayataki mazungumzo, yanatafuta tu kuua watu wasio na hatia.