Gaidi Hana Rafiki, Dunia Iungane

Siungi mkono kuuawa kwa mtu yeyote asiye na hatia, au hata mwenye hatia lakini hatia yake haina hatari kwa maisha ya watu wengine.

Kila nikitizama vifo, hasa vifo vya wale watoto wadogo wa kule Gaza, naumia sana moyoni, maana angalao una uhakika kuwa watoto wale hawana hatia yoyote. Hali kadhalika wale wapalestina wasio na mafungamano yoyote na Hamas.

Lakini kuna tofauti kati ya hawa magaidi wa Hamas na askari wa Israel. Askari wa Israel wanawatafuta Hamas, lakini katika kutafuta huko ndiko kunasababisha hata wasio Hamas kuuawa, ama kwa kukosa umakini ama kwa sababu ya mbinu za magaidi ya Hamas kujichanganya na raia.

Siamini kuwa bila ya shambulio la Hamas, Israel wangeenda kuwaua Wapalestina. Hata maisha ya Wapalestina yamekuwa kama ya gereza kutokana na vitendo vya hawa magaidi. Hapo mwanzo haikuwa hivyo.

Wapalestina, hata kama kuna haki wanaidai au kuitafuta, kuna njia sahihi za kuidai ambazo zingewapa mafanikio kuliko kuamini eti hawa magaidi wanapigania haki ya Wapalestina. Mbona uongozi wa Ramallah chini ya Arafat ulipofikia makubaliano na Israel juu ya kuundwa kwa taifa la Palestina, haya magaidi ya Hamas yakapinga na kuanzisha vita dhidi ya uongozi wa Ramallah, kwa madai kuwa kwa nini wanafanya mazungumzo na wayahudi? Kwa hiyo magaidi ya Hamas, hayataki mazungumzo, yanatafuta tu kuua watu wasio na hatia.
Hiv upo serius kweli????Ni lini mayahudi yalikuwa na njema zaidi ya kuendelea.kuchukua ardhi kila kukicha
 
Mbona vijana wa kikristo hawashawishiki kwenda kujiunga na hayo makundi?
Hayo makundi hayatawakubali ila mpaka Wasilimu laa sivyo watamuona ni Spy.

Nimeona Video moja kijana wa Kenya amekamatwa akiwa na Magaidi wa Alshababu alisema kwao wote ni Wakristo na nyumbani kwao ni Kisumu, lakini yeye aliamua kujiunga na Dini ya Kiislamu.
 
Nimewaza tu, eti Mandela naye alikuwa Gaidi na wale ANC, hata wale wamakonde wa msumbiji waliitwa Magaidi.

Talebani ni magaidi lakini USA kaondoka kawaachia nchi Magaidi.

Njia ileile anayoitumia Hamas ndio ileile anayoitumia Israel lakini tunamlaani Hamas na kumuona Israel ni mwema, Israel na Palestina zote zimeshakuwa battle ground na lolote hutokea wakati wowote tena tukumbuke mwenye nguvu na mamlaka anapigana na mnyonge asiye nachochote.

Wote tunauchungu kijana wetu Mtanzania mwenzetu ameuwawa, lakini tuangalie intention ya Hamas kuingia Israel ilikuwa ni nini? kuja kumuua huyu kijana na kuondoka? Hapana, bali dhamira ilikuwa kuua na kuteka kila ajaye mbele yao, ndio maana haikuua na kumteka Mtanzania tu bali watu wa mataifa mbalimbali.

Kwanini tunailaani Hamas na si Israeli inayotumia mbinu zilezile za Hamas kutimiza dhamira yake?..,, Ugomvi wa hawa watu wawili ni ardhi na imani, Palestina akidai pale ni kwao na Israel akidai pale ni kwao, Ushahidi wa Israeli ni Bible na ushahidi wa Palestina ni uwepo wao pale na dunia imeshindwa kuprove zaidi ya kumtaka mmoja awe mnyonge na kukubaliana huku yeye akiamini si sawa..

tutafakari sana kabla ya kuandika.
Ndugu yangu nadhani umepitwa na kumbukumbu za kihistoria.

Eneo la Canaan ambalo waisrael na waarabu sasa hivi wapo, ni ardhi ambayo jamii hizi mbili na nyingine ndogondogo ziliishi tangu kale, huku jamii ya Wayahudi ikiwa ndiyo yenye watu wengi. Kusambaa kwa Wayahudi, baadaye kulilifanya eneo hilo liwe na waarabu wengi kuliko Wayahudi. Hakuna watu walioitwa Wapalestina, kwa maana neno palestine au Falastin kwa kiarabu liliashiria eneo la pwani ya bahari, hivyo siyo kabila.

Umoja wa Mataifa kwa kutambua kuwa eneo hilo ziliishi jamii hizi kubwa mbili, mwaka 1947, ililigawa, 60% walipewa Wayahudi, na 40% walipewa Waarabu. Lakini kwa ujinga na kiburi, waarabu walilikataa eneo walilopewa wakidai halina rutuba, na kuamua kuanzisha vita dhidi ya Wayahudi. Na kila waliposhindwa vita, walizidi kulipoteza eneo walilopewa. Eneo la 40% walilopewa walilikataa, leo wanadai eneo dogo kuliko hilo la mwaka 1947. Hivi unaamini haya magaidi ya Hamas hata yakipewa hilo eneo, yatakoma kuua watu. Haya magaidi ni kama jambazi, kwao kuua ni kama ajira yao.
 
Askari wa Israel wanawatafuta Hamas, lakini katika kutafuta huko ndiko kunasababisha hata wasio Hamas kuuawa, ama kwa kukosa umakini ama kwa sababu ya mbinu za magaidi ya Hamas kujichanganya na raia.
Hii ndio double standard, wakiua Hamas ni makusudi ila wakiua IDF ni umakini? Embu niambie kushoot hospitali yenye watoto wadogo waliopo ICU ni bahati mbaya? Kama wanajua hamas wapo kwenye handaki chini ya hospitali kwanini wasivamie hospitali mpaka walipue magorofa ilihali hamas wako chini huko hawawezi athirika na mabomu?
Siamini kuwa bila ya shambulio la Hamas, Israel wangeenda kuwaua Wapalestina. Hata maisha ya Wapalestina yamekuwa kama ya gereza kutokana na vitendo vya hawa magaidi. Hapo mwanzo haikuwa hivyo.
Sio kweli, West Bank haipo ndani ya mipaka ya TAIFA la Israel ila cha ajabu waisraeli laki 5 wamehamia huko na kupora ardhi ya wapalestina huku wakiwatoa kwa nguvu kwa risasi. Ni ajabu sana watu wanadhani mateso yameanza baada ya October 7!! Naomba ukafuatilie issue ya WALOWEZI ndio utaelewa kwanini hamas walivamia vijiji vile ambavyo ni ardhi ya palestina ila vimekaliwa kimabavu. Kama tu Urusi ilivyokalia kimabavu donbass au Kherson je wanakosea kutaka kuyakomboa?. Wakifanya Ukraine ukombozi akifanya Hamas ni ugaidi??
kuna njia sahihi za kuidai ambazo zingewapa mafanikio kuliko kuamini eti hawa magaidi wanapigania haki ya Wapalestina
Njia ipi? Diplomasia imeshafeli, hata Mandela alitumia mbinu za ugaidi kwa kulipua majengo na kuteka wazungu ila waafrika wote na dunia nzima leo hii tunamuita Shujaa. Hata hao Israel walitumia ugaidi kuua na ku revenge kwa askari wa Hitler, viongozi wa arab nations kama Syria, Iran na Lebanon waliokua wanawapinga cha ajabu haiitwi ugaidi ila ujasusi na ukomandoo!! Hakuna lugha Israel anaelewa zaidi ya risasi na October 7 zitajirudia tu kila mwaka.
Mbona uongozi wa Ramallah chini ya Arafat ulipofikia makubaliano na Israel juu ya kuundwa kwa taifa la Palestina, haya magaidi ya Hamas yakapinga na kuanzisha vita dhidi ya uongozi wa Ramallah
Ambacho hujui Israel ndio ilianzisha Hamas ili kudhoofisha PLO na palestina igawanyike. Hata hayo mahandaki ya huko Gaza mengi yalijengwa na Israel huko zamani sielewi kwanini hizi facts hamzijui. Kingine Israel ndio haitaki mazungumzo hasa hardliners maana Yitzakh Rabin waziri mkuu alitaka kuweka amani na palestina na kuondoa walowezi wote waliokalia palestina kimabavu. Ila akauwawa na askari wa Israel maana waliona ana surrender kwa adui. So its Israel isiyotaka mazungumzo sio Hamas.
 
Maana ya Gaidi ni nini?
Gaidi ni neno tulilolitafsiri kutoka kwenye kiingereza, yaani terrorist.

Terrorist ni mtu au kikundi kinachofanyanya terrorism. Terrorism ni noun ya neno terror. Terror ni kutisha, yaani kufanya mauaji kwa nia ya kutisha au kuleta taharuki.

Magaidi ya Hamas, yametamka wazi kuwa yenyewe yaliwaua hata watu wa mataifa mengine ili watu wote Duniani wajue kuwa wakienda Israel wanaweza kuuawa kwa sababu ni kama wanaunga mkono uwepo wa Taifa la Israel. Hivyo vitendo vyote vya Hamas vimelenga kuleta terror, yaani kuwatisha watu.

Magaidi ya Hamas yamewaua raia wa Israel, na kuwabaka mabinti wa Israel kisha kuwaua, yamewakata shingo hata watoto wadogo, lengo lao likiwa moja tu yaani kuleta terror/taharuki. Yaani kupeleka ujumbe wa kitisho kwa waliosalia kuwa kama waisrael hawataridhia matakwa yao hawa magaidi, hayo mauaji yataendelea.

Nimefafanua kwa kirefu kuhusu gaidi na ugaidi.
 
Duniani popote hakuna mtu anayezaliwa kuwa gaidi, gaidi anatengenezwa na kufadhiliwa na wenye pesa kwa maslahi ya wenye pesa. Achana na hao vijana wanaopokea maagizo kutoka kwa mabosi zao, mabosi huwa wanajua ni zipi sababu kuu za kuundwa kwa jeshi na kwa ajili ya maslahi ya nani!.
Huwezi nambia eti Israel pamoja na MOSSAD hawakuweza kutambua kuwa HAMAS anajenga mahandaki chini ya ardhi!, ni uongo wa hali ya juu sana
 
Hakuna mkate mgumu mbele.ya.chai ucpotubu ...utakufa huku mdomo ukiwa wazi na utalipwa kwa yote uliyotenda...

Ila hongera naona mwenzetu una mama wa kiume ambaye hakuwa na bikra...ila yawezekana alikuwa mchanyato
Kaliwe ulipozoea kuliwa
 
Kanuni kuu ya gaidi ni kuua yeyote. Hivyo ujue kuwa gaidi akitaka kuua tajiri, halafu maskini nao wakawepo hapo hapo, na maskini nao watauawa pamoja na huyo tajiri. Ndiyo maana yale magaidi ya September 11 kule US, hayakuuliza wala kuchunguza ndani ya zile ndege kulikuwa na wageni wangapi wala kwenye yale majengo kama kulikuwa na wageni au waislam.

Magaidi ya Hamas, hayajawaua watanzania, Waafrika Kusini, Wamalawi, Wamarekani, Waingereza na wengine wote kwa bahati mbaya. Wamefanya hivyo makusudi, na kwa kujua kabisa kuwa yanawaua watu wa Mataifa mbalimbali. Yaliwaua waafrika huku yakichukua video kwa lengo la kuhakikisha video hizo zinafika kwa Waafrika wenzao ili waogope kwenda Israel, na Israel ikose wafanyakazi wa mashambani.

Magaidi yaliyoshambulia ubalozi wa Kenya pale Nairobi, hayakuuliza humo ndanii kuna waislam wangapi au wakristo wangapi. Yaliua kila ambaye bomu liliweza kumfikia.

Magaidi ya Hamas yamewahi kuwaua wapalestina wenzao kwa madai kwa nini wanafanya mazungumzo na Wayahudi.

Magaidi ya Hizbollah yalimwua Waziri mkuu wao Rafiq Hariri kwa madai kuwa kwa nini alikuwa anawashirikisha wakristo wachache kwenye Serikali yake.

Magaidi ya Hamas, sasa yamefikia kutoa tamko kuwa yamewaua na kuwateka watu wa mataifa mbalimbali Duniani, siyo kwa bahati mbaya, bali kwa kukusudia, ili kuweka tishio kuwa ukienda Israel hupo salama. Yaani watu wote waogope kwenda Israel.

Na ndicho magaidi ya Houthi ya kule Yemen yanachofanya pia. Yanaziteka meli zinazopita kwenye ghuba ya Yemen. Lengo ni kuyafanya makampuni ya meli yaogope kupitisha meli zao eneo hilo; na kama meli hazitapita hapo, basi Israel ikose mizigo.

Ni punguani pekee anayeweza kuunga mkono ugaidi wa Hamas. Haya magaidi yanaweza kuondoa hata uhai wake yeye anayeuyaunga mkono. Chukulia unasafiri, umepanda ndege, ndani ya ndege kuna mtu ambaye haya magaidi yanamtafuta. Yakiamua kuilipua hiyo ndege, haya magaidi hayafikirii kabisa juu ya uhai wa wale abiria wengine nje ya yule wanayemtaka. Yatawaua ninyi nyote pamoja.

Urafiki qetu na mamlaka ya Palestina, haujasaidia chochote kuzuia magaidi haya yasiwaue vijana wetu. Huo ni ujumbe tosha kuwa gaidi hana rafiki, na kwamba tumekuwa wajinga kufanya urafiki na jamii hizi za magaidi.

Magaidi ya Hamas yametenda unyama wa kila aina siku ile ya tarehe 7 Octoba kule Israel. Yaliua bila ubaguzi. Na kuna uthibitisho yaliwabaka wasichama wa Israel maeneo ya mashambani, kisha kuwakata shingo. Na sasa yanajivunia kutekeleza unyama huu.

Dunia isipoungana kuyaangamiza haya magaidi ya Hamas, Hizbollah na mengine yaliyojazana hapo Mashariki ya Kati, kuna siku Dunia itajuta.

Tuombee kampeni ya Israel ya kuyaangamiza haya magaidi, ifanikiwe. La sivyo, Dunia nzima siyo salama. Angalia yalivyotusumbua kule Kibiti na Mkurunga. Fikiria huko jimbo la Cabo Delgado Msumbiji, Somalia, Nigeria, Mali, na maeneo mengine mengi.

Haya magaidi yakipata ushindi ja yakizidi kujijenga, itafika mahali yatakuwa yanashambulia nchi yoyote au kiongozi yeyote kama hayaungi mkono.
Wanao watetea ni marafiki zao.
Waliotaka kuandamana kutoka Jangwani mapaka mnazi mmoja ni marafiki zao.
Unataka kuficha kichwa kwenye mchanga wakati ta** lipo juu kama mbuni, ni aibu ya supporters wa Magaidi ya kiislamu!
 
Sawa Dada tumekusikia , ndio maana ata Israel na yeye anaweza kuua wanawake na watoto wasio na hatia kwa sababu na yeye ni GAIDI MKUBWA KULIKO HAMAS.

HAO DADA ZAKO ISRAEL KWA NINI WANABOMOA MAJUMBA YA RAIA WAKATI WANAUME HAMAS WAKO CHINI YA ARDHI, KWA NINI WASIIINGIE HUKO CHINI YA ARDHI?

HALAFU HAO.DADA ZAKO ISRAEL MBONA WANAPIGA MAHOSPITALI NA MASHULE AMBAYO YAMESHEHENI WAGONJWA ? HOW CAN U KILL A HELPLESS HUMAN BEING IF YOU ARE NOT A TERRORIST ?

TUAMBIE KWA NINI DADA ZAKO ISRAEL WANAWAUA WAANDISHI WA HABARI WANAORIPOTI MADHILA YAO, WANAFICHA NINI?

KAMA HAMAS NI MAGAIDI KWA KUTAKA KUJIKOMBOA KUTOKA KWA DADA ZAKO ISRAEL,.BASI HAO SI ISRAEL SIJUI TUWAITEJE MAANA UOVU WANAOUFANYA NI MARA MIA YA HAMAS

Ignored.

Tunajibu watu wenye healthy brain.
 
Kanuni kuu ya gaidi ni kuua yeyote. Hivyo ujue kuwa gaidi akitaka kuua tajiri, halafu maskini nao wakawepo hapo hapo, na maskini nao watauawa pamoja na huyo tajiri. Ndiyo maana yale magaidi ya September 11 kule US, hayakuuliza wala kuchunguza ndani ya zile ndege kulikuwa na wageni wangapi wala kwenye yale majengo kama kulikuwa na wageni au waislam.

Magaidi ya Hamas, hayajawaua watanzania, Waafrika Kusini, Wamalawi, Wamarekani, Waingereza na wengine wote kwa bahati mbaya. Wamefanya hivyo makusudi, na kwa kujua kabisa kuwa yanawaua watu wa Mataifa mbalimbali. Yaliwaua waafrika huku yakichukua video kwa lengo la kuhakikisha video hizo zinafika kwa Waafrika wenzao ili waogope kwenda Israel, na Israel ikose wafanyakazi wa mashambani.

Magaidi yaliyoshambulia ubalozi wa Kenya pale Nairobi, hayakuuliza humo ndanii kuna waislam wangapi au wakristo wangapi. Yaliua kila ambaye bomu liliweza kumfikia.

Magaidi ya Hamas yamewahi kuwaua wapalestina wenzao kwa madai kwa nini wanafanya mazungumzo na Wayahudi.

Magaidi ya Hizbollah yalimwua Waziri mkuu wao Rafiq Hariri kwa madai kuwa kwa nini alikuwa anawashirikisha wakristo wachache kwenye Serikali yake.

Magaidi ya Hamas, sasa yamefikia kutoa tamko kuwa yamewaua na kuwateka watu wa mataifa mbalimbali Duniani, siyo kwa bahati mbaya, bali kwa kukusudia, ili kuweka tishio kuwa ukienda Israel hupo salama. Yaani watu wote waogope kwenda Israel.

Na ndicho magaidi ya Houthi ya kule Yemen yanachofanya pia. Yanaziteka meli zinazopita kwenye ghuba ya Yemen. Lengo ni kuyafanya makampuni ya meli yaogope kupitisha meli zao eneo hilo; na kama meli hazitapita hapo, basi Israel ikose mizigo.

Ni punguani pekee anayeweza kuunga mkono ugaidi wa Hamas. Haya magaidi yanaweza kuondoa hata uhai wake yeye anayeuyaunga mkono. Chukulia unasafiri, umepanda ndege, ndani ya ndege kuna mtu ambaye haya magaidi yanamtafuta. Yakiamua kuilipua hiyo ndege, haya magaidi hayafikirii kabisa juu ya uhai wa wale abiria wengine nje ya yule wanayemtaka. Yatawaua ninyi nyote pamoja.

Urafiki qetu na mamlaka ya Palestina, haujasaidia chochote kuzuia magaidi haya yasiwaue vijana wetu. Huo ni ujumbe tosha kuwa gaidi hana rafiki, na kwamba tumekuwa wajinga kufanya urafiki na jamii hizi za magaidi.

Magaidi ya Hamas yametenda unyama wa kila aina siku ile ya tarehe 7 Octoba kule Israel. Yaliua bila ubaguzi. Na kuna uthibitisho yaliwabaka wasichama wa Israel maeneo ya mashambani, kisha kuwakata shingo. Na sasa yanajivunia kutekeleza unyama huu.

Dunia isipoungana kuyaangamiza haya magaidi ya Hamas, Hizbollah na mengine yaliyojazana hapo Mashariki ya Kati, kuna siku Dunia itajuta.

Tuombee kampeni ya Israel ya kuyaangamiza haya magaidi, ifanikiwe. La sivyo, Dunia nzima siyo salama. Angalia yalivyotusumbua kule Kibiti na Mkurunga. Fikiria huko jimbo la Cabo Delgado Msumbiji, Somalia, Nigeria, Mali, na maeneo mengine mengi.

Haya magaidi yakipata ushindi ja yakizidi kujijenga, itafika mahali yatakuwa yanashambulia nchi yoyote au kiongozi yeyote kama hayaungi mkono.
Mm gaidi akinipiga bomu likamuua na netanyahu .aje nimpe.na hela kabisa
 
Duniani popote hakuna mtu anayezaliwa kuwa gaidi, gaidi anatengenezwa na kufadhiliwa na wenye pesa kwa maslahi ya wenye pesa. Achana na hao vijana wanaopokea maagizo kutoka kwa mabosi zao, mabosi huwa wanajua ni zipi sababu kuu za kuundwa kwa jeshi na kwa ajili ya maslahi ya nani!.
Huwezi nambia eti Israel pamoja na MOSSAD hawakuweza kutambua kuwa HAMAS anajenga mahandaki chini ya ardhi!, ni uongo wa hali ya juu sana!

Mfadhili mkuu wa ugaidi Duniani, anafahamika. Ni IRAN. Iran ilianzisha na inafadhili makundi mengi ya kigaidi kama vile Hamas, Hizibollah, Harakat al Nujaba.
 
Kanuni kuu ya gaidi ni kuua yeyote. Hivyo ujue kuwa gaidi akitaka kuua tajiri, halafu maskini nao wakawepo hapo hapo, na maskini nao watauawa pamoja na huyo tajiri. Ndiyo maana yale magaidi ya September 11 kule US, hayakuuliza wala kuchunguza ndani ya zile ndege kulikuwa na wageni wangapi wala kwenye yale majengo kama kulikuwa na wageni au waislam.

Magaidi ya Hamas, hayajawaua watanzania, Waafrika Kusini, Wamalawi, Wamarekani, Waingereza na wengine wote kwa bahati mbaya. Wamefanya hivyo makusudi, na kwa kujua kabisa kuwa yanawaua watu wa Mataifa mbalimbali. Yaliwaua waafrika huku yakichukua video kwa lengo la kuhakikisha video hizo zinafika kwa Waafrika wenzao ili waogope kwenda Israel, na Israel ikose wafanyakazi wa mashambani.

Magaidi yaliyoshambulia ubalozi wa Kenya pale Nairobi, hayakuuliza humo ndanii kuna waislam wangapi au wakristo wangapi. Yaliua kila ambaye bomu liliweza kumfikia.

Magaidi ya Hamas yamewahi kuwaua wapalestina wenzao kwa madai kwa nini wanafanya mazungumzo na Wayahudi.

Magaidi ya Hizbollah yalimwua Waziri mkuu wao Rafiq Hariri kwa madai kuwa kwa nini alikuwa anawashirikisha wakristo wachache kwenye Serikali yake.

Magaidi ya Hamas, sasa yamefikia kutoa tamko kuwa yamewaua na kuwateka watu wa mataifa mbalimbali Duniani, siyo kwa bahati mbaya, bali kwa kukusudia, ili kuweka tishio kuwa ukienda Israel hupo salama. Yaani watu wote waogope kwenda Israel.

Na ndicho magaidi ya Houthi ya kule Yemen yanachofanya pia. Yanaziteka meli zinazopita kwenye ghuba ya Yemen. Lengo ni kuyafanya makampuni ya meli yaogope kupitisha meli zao eneo hilo; na kama meli hazitapita hapo, basi Israel ikose mizigo.

Ni punguani pekee anayeweza kuunga mkono ugaidi wa Hamas. Haya magaidi yanaweza kuondoa hata uhai wake yeye anayeuyaunga mkono. Chukulia unasafiri, umepanda ndege, ndani ya ndege kuna mtu ambaye haya magaidi yanamtafuta. Yakiamua kuilipua hiyo ndege, haya magaidi hayafikirii kabisa juu ya uhai wa wale abiria wengine nje ya yule wanayemtaka. Yatawaua ninyi nyote pamoja.

Urafiki qetu na mamlaka ya Palestina, haujasaidia chochote kuzuia magaidi haya yasiwaue vijana wetu. Huo ni ujumbe tosha kuwa gaidi hana rafiki, na kwamba tumekuwa wajinga kufanya urafiki na jamii hizi za magaidi.

Magaidi ya Hamas yametenda unyama wa kila aina siku ile ya tarehe 7 Octoba kule Israel. Yaliua bila ubaguzi. Na kuna uthibitisho yaliwabaka wasichama wa Israel maeneo ya mashambani, kisha kuwakata shingo. Na sasa yanajivunia kutekeleza unyama huu.

Dunia isipoungana kuyaangamiza haya magaidi ya Hamas, Hizbollah na mengine yaliyojazana hapo Mashariki ya Kati, kuna siku Dunia itajuta.

Tuombee kampeni ya Israel ya kuyaangamiza haya magaidi, ifanikiwe. La sivyo, Dunia nzima siyo salama. Angalia yalivyotusumbua kule Kibiti na Mkurunga. Fikiria huko jimbo la Cabo Delgado Msumbiji, Somalia, Nigeria, Mali, na maeneo mengine mengi.

Haya magaidi yakipata ushindi ja yakizidi kujijenga, itafika mahali yatakuwa yanashambulia nchi yoyote au kiongozi yeyote kama hayaungi mkono.
Hiyo picha kwenye profile yako ni nani ?
 
Hiv upo serius kweli????Ni lini mayahudi yalikuwa na njema zaidi ya kuendelea.kuchukua ardhi kila kukicha
Nimeeleza wazi, hapo mwanzo Waarabu wa Palestine walipewa eneo la 40% la ukubwa wote. Walipewa kwenye mgawanyo uliosimamiwa na Umoja wa mataifa. Wakagoma. Israel kwa vyovyote wangependa wapate hata zaidi ya hiyo 60%, lakini UN kama taasisi ilisyosimama katikati iliamua Wayahudi wapewe 60% tu. Sasa ujinga wa Wapalestina, wakagomea hiyo 40% waliyopewa. Kila walipoanzisha vita, Israel ilizidi kuongeza eneo na kudai ni buffer zone, yaani ili iwe mbali na hawa wauaji. Lakini mazingira hayo waliyatengeneza Waarabu wenyewe.

Kama kungekuwa na wenye busara, huenda baadhi ya maeneo yangerudishwa, lakini kwanza kuwepo na trust. Vile vitendo vya magaidi kwenda kujilipua ndani ya Israel, na mashambulizi ya kushitukiza kwenye vizuizi vimejenga mazingira ya Waisrael kutowaamini waarabu hawa wa Gaza.

Misri ilipigana na Israel. Katika vita, Misri ilipoteza eneo la Sinai. Lakini baadaye kwa njia ya maelewano, Israel ililirudisha eneo la Sinai kwa Misri. Na toka wakati huo Misri imeendelea kuwa na uhusiano wa karibu sana na Israel, kuzidi hata ule wa Misri na baadhi ya mataifa ya kiarabu.
 
Hii ndio double standard, wakiua Hamas ni makusudi ila wakiua IDF ni umakini? Embu niambie kushoot hospitali yenye watoto wadogo waliopo ICU ni bahati mbaya? Kama wanajua hamas wapo kwenye handaki chini ya hospitali kwanini wasivamie hospitali mpaka walipue magorofa ilihali hamas wako chini huko hawawezi athirika na mabomu?
Sio kweli, West Bank haipo ndani ya mipaka ya TAIFA la Israel ila cha ajabu waisraeli laki 5 wamehamia huko na kupora ardhi ya wapalestina huku wakiwatoa kwa nguvu kwa risasi. Ni ajabu sana watu wanadhani mateso yameanza baada ya October 7!! Naomba ukafuatilie issue ya WALOWEZI ndio utaelewa kwanini hamas walivamia vijiji vile ambavyo ni ardhi ya palestina ila vimekaliwa kimabavu. Kama tu Urusi ilivyokalia kimabavu donbass au Kherson je wanakosea kutaka kuyakomboa?. Wakifanya Ukraine ukombozi akifanya Hamas ni ugaidi??
Njia ipi? Diplomasia imeshafeli, hata Mandela alitumia mbinu za ugaidi kwa kulipua majengo na kuteka wazungu ila waafrika wote na dunia nzima leo hii tunamuita Shujaa. Hata hao Israel walitumia ugaidi kuua na ku revenge kwa askari wa Hitler, viongozi wa arab nations kama Syria, Iran na Lebanon waliokua wanawapinga cha ajabu haiitwi ugaidi ila ujasusi na ukomandoo!! Hakuna lugha Israel anaelewa zaidi ya risasi na October 7 zitajirudia tu kila mwaka.
Ambacho hujui Israel ndio ilianzisha Hamas ili kudhoofisha PLO na palestina igawanyike. Hata hayo mahandaki ya huko Gaza mengi yalijengwa na Israel huko zamani sielewi kwanini hizi facts hamzijui. Kingine Israel ndio haitaki mazungumzo hasa hardliners maana Yitzakh Rabin waziri mkuu alitaka kuweka amani na palestina na kuondoa walowezi wote waliokalia palestina kimabavu. Ila akauwawa na askari wa Israel maana waliona ana surrender kwa adui. So its Israel isiyotaka mazungumzo sio Hamas.

Kuna kitu umekisema ni sahihi kabisa, ila conclusion yako umekosea. Sijui kama ni kwa bahati mbaya, au ilikupita.

Ni kweli kuwa kuna wayahudi ni hardliners ambao hawataki kabisa mazungumzo na makubaliano yoyote na wapalestina. Lakini hao ni raia tu wa kawaida, na baadhi wanaweza kuwa ni sehemu ya uongozi. Lakini watu hao hawana kundi lolote kama lilivyo Hamas, upande wa Palestina, hivyo wana nguvu ndogo ya kuzuia maamuzi yaliyo kinyume na wao.

Upande wa Palestina, yapo makundi kama hili la Hamas, hayataki kabisa mazungumzo yoyote kati ya Israel.na Wapalestina. Haya makundi yanatamka wazi kuwa Wayahudi hawatakiwi kuwepo hapa Duniani. Na makundi hayo yalianzishwa na yanagharamiwa na kuungwa mkono na Iran.

Mwaka 1993, Yasar Arafat na Yitzak Rabin, chini ya usaidizi wa Marekani, walikubaliana kuundwa kwa Taifa la Palestina, lakini uundwaji wa Taifa hilo uende hatua kwa hatua kwa sababu kila upande kulikuwa na upinzani wa ndani.

Wakati Yasar Arafat anampa mkono Yitzak Rabin, Rabin hakuupokea mkono wa Arafat, halafu baadaye akampa, na kumwuliza, "sijui kama unajua kuwa hiki tunachokifanya leo ni hukumu yetu ya kifo. Watakaoniua mimi siyo wapalestina bali ni Wayahudi. Na watakaokuua wewe siyo Wayahudi bali ni Wapalestina". Na hicho ndicho kilichotokea. Wayahudi wenye misimamo mkali walimwua Rabin. Na Hamas walim-sassinate Arafat.

Lakini, kama hatua ya mwanzo kuekekea kuundwa kwa taifa la Wapalestina, mamlaka ya ndani ya Palestina iliundwa. Kabla ya kwenda mvele zaidi, Hamas ilizuia kabisa kuoiga hatua yoyote nyingine mbele. Ikaanzisha vita dhidi ya Serikali ya mamlaka ya ndani ya Palestina. Kwa msaada wa Iran, Hamas wakashinda. Wakaua ndoto zote za kuanzishwa taifa la Palestina kwa sababu wao wakasema hawataki Taifa la Palestina lenye mipaka pungufu ya ile ya kabla ya mwaka 1967. Baada ya hapo wakaendeleza mashambulizi mbalimbali dhidi ya Israel, yamiwemo ya kujitoa mhanga.
 
- USA hakuwaachia nchi magaidi, alitoa mafunzo ya kijeshi kwa jeshi la Afghanistan kwa karibia miaka kumi, ajabu wale jamaa bado wakashindwa kujilinda, ndipo USA akaona ujinga huu, akaondoka.

- Sio kweli unavyosema njia anayotumia Hamas ndio hiyo hiyo anayotumia Israel, ni wapi jeshi la Israel limewateka na kuwaua raia wa nchi zisizohusika na ile vita?

- Hamas kuwa mnyonge hakuhalalishi kwao kuua raia wasio na hatia kwa kuwachinja, na wengine kuwapiga risasi individually huku wakiwarekodi kwa video, wale ni wahuni na wendawazimu walioamua kuhamishia stress za vita yaoa na Israel kwa wasiohusika.

- Hiyo intention ya Hamas uliyoandika hapo ndio umethibitisha mwenyewe hao Hamas walivyo wapuuzi, kama wamefanikiwa kuingia Israel, kwanini wasi target maeneo waliyopo/kumilikiwa na waisrael, badala yake wanageuza vita kama mchezo wa kamari?

- Tunawalaani Hamas kwasababu ni wahuni wasiotoa ultimatum ili kuanza mashambulizi yao, badala yake wamejigeuza mashetani watoa roho zisizo na hatia kwa kuzichambua individually na kuwapiga risasi huku wakishangilia, pure lunatics.

Jitahidi utafakari sana kabla ya kuandika.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Madhara ya Dini yanafanana Kwa karibu sana na madhara ya Bangi au pombe Kali yenye kuharibu akili. Dini inaharibu akili na inaondoa umakini wa kutafakari na kuchanganua mambo. Linapoongelewa suala la Dini watu wote ambao huonekana au kujifanya ni wafia Dini huweka utu pembeni ni kuweka ujinga wao wa kidini mbele.

Hebu angalia hata baadhi ya Dini zetu zile zinazojipepetua kwamba zinafuata zaidi matakwa ya Mwenyeji Mungu zilivyo na mambo ya ajabu. Fikiria mtu anadiliki kujiita yeye ni Bora zaidi kuliko wengine ati tu Kwa sababu ana imani Fulani ambayo hakuna uhakika hata kama analofanya ni takwa halisi la Mungu.

Hata hii issue ya Palestine vs Israel, mtu analaani au kutetea mara nyingi siyo Kwa kuangalia actual fact Bali ni Kwa mihemuko au Bangi za kidini. Suala kama hili lilijionesha wazi hata wakati ule wa DP World, ilikuwa ni ujinga huo huo.

Mtu anabeza au kutotilia maanani kuuwawa Kwa vijana wetu ati Kwa kulinganisha na wenyeji wanaokufa huko. Issue ni kwamba hao vijana ni WA kwetu sisi kutoka nyumba yetu wenyewe na hatupashwi kuwalinganisha na yeyote asiye WA kwetu.
 
Wanao watetea ni marafiki zao.
Waliotaka kuandamana kutoka Jangwani mapaka mnazi mmoja ni marafiki zao.
Unataka kuficha kichwa kwenye mchanga wakati ta** lipo juu kama mbuni, ni aibu ya supporters wa Magaidi ya kiislamu!

Dini ya kiislam ina kazi kubwa ya kujitenga na ugaidi. Kwa sababu kila gaidi anapenda kujitambulisha na uislam. Mtu anamchinja mwenzake huku anasema Allahu akbar, kuashiria hicho anachokifanya kina uhusiano na uislam.
 
Back
Top Bottom