PreGE2025 G55 Moshi na Temeke waondoka CHADEMA

PreGE2025 G55 Moshi na Temeke waondoka CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Wakuu,

Mpango wa kupiga kelele kwenye media ili wasisahaulike unaendelea :KEKLaugh: hivi hawaoni walivyokuwa majinga? Ukiamua kumla chura hakikisha unachagua aliyenona, sasa unakula chura afu unachagua chenye kimedhoofu na utapia mlo, unamla, anakuua, inakuwa ni fezea:KEKLaugh::BearLaugh::BearLaugh:

Wacha tuendelee kukinga maji yanayovuja tukaflashie chooni!

Pia soma Pre GE2025 - Ogopa Teknolojia na Mungu! Sasa ni rasmi G55 wametumwa kuifumuafumua CHADEMA mpaka isambaratike

dar.jpg
moro.jpg
moshi.jpg

Moshi wameanza kuunguruma


Meza kuu inajumuisha
  • Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Moshi DC - Exaudi Wilson Mamuya
  • Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya Moshi DC - Michael Kilawila
  • Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Kilimanjaro - Grace Kiwelu
  • Katibu wa BAVICHA Kanda ya Kaskazini - Rachel Sadiki
  • Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro - Gervas Mgonja
  • Katibu wa Mkoa wa Kilimanjaro

Gervas Mgonja Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro
Mwenendo wa chama chetu hauridhishi, tuliokuwa tunamsapoti Mbowe tumekuwa hatuishi kwa amani ndani ya kipindi hiki. Najivua rasmi vyeo vyangu na uanachama wa CHADEMA kuanzia leo Mei 11, 2025.

Rachel Sadiki Mwanachadema & na Founder wa CHADEMA jimbo la Mkinga-Tanga
Nilipeleka harakati kwa mara ya kwanza CHADEMA, nilifanya kazi mpaka nikafukuzwa serikalini, nikafirisika. Tulishauri lakini tulichukuliwa kama wahalifu. Hatujapewa haki ya kujieleza wala kusikilizwa, suala la kuondolewa/kushughulikiwa kwetu lina baraka za chama, sioni mwanga huko tunapoenda. Ninajitoa uanachama wa CHADEMA na kujivua nyadhifa zilizonazo na kufanya shughuli nyingine kama alivyosema Mbowe

Grace Kiwelu Mwenyekiti BAWACHA Kilimanjaro, Mwenyekiti Kamati ya Fedha Kanda ya Kaskazini, Mjumbe Kamati Tendaji BAWACHA Taifa

Tulizunguka nchi nzima na Mbowe kuitangaza CHADEMA toka 1992, badala ya kuvuna heshima tunavuna matusi. Tunawezaje kuzuia uchaguzi bila kushiriki? Kusema wananchi waandamane, nikiwaangalia wananchi kule vunjo wataanzia wapi kuandamana? Viongozi wanaona matusi hawakemei, kosa ni kumuunga mkono Mbowe. Nilimuunga kweli Mbowe kwasababu niliona kazi aliyoifanya ya mageuzi ndani ya chama na nchini, bila Mbowe tusingekuwa na CHADEMA ambayo tunayo leo. Kuanzia leo Mei 11, ninajiondoa CHADEMA, ninakwenda nyumbani kupumzika, nakwenda kulea mjukuu wangu, nimechoka matusi ya mtandaoni.

Michael Kilawila Mwenyekiti Mstaafu wa Moshi DC, na Mwenyekiti wa Mkoa Awamu ya 3 Kilimanjaro

CHADEMA yenye upendo na mshikamano imeanza kupotea, chuki ilianza baada ya kutompendelea mtu mmoja ili achaguliwe kugombea ubunge jimbo la Korogwe mwaka 2020. Kuna mtu alikimbia na familia yake na kutuacha hapa akataka tumpokee kishujaa wakati yeye sio shujaa, mimi na Basil tukaanza kushughulikiwa. Nimeamua kuondoka na maamuzi yangu binafsi, nimeona CHADEMA sio mahali salama tena pa kuendelea kufanya siasa. Leo Mei 11, 2025 ninaachana na CHADEMA, ninaenda kupumzika, kadi yangu nitaitunza ili wajuu wangu waje waione wajifunze kwenye historia kwamba nilitukanwa sana. CCM wasinipigie simu, sitaenda CCM, hamtasikia kwamba nimeenda CCM lakini lazima nitafute chama ambacho naona kitafikia malengo yale ambayo wananchi wanataka.

Exaudi Wilson Mamuya Makamu Mwenyekiti wa Moshi DC
Nimekuwa mwananchama wa CHADEMA toka nikiwa na umri mdogo, nimekitumikia chama kwa wivu mkubwa na mapenzi mpaka sasa tumefika mahali naumia moyoni. Kwenye uchaguzi Mkuu sisi tulichagua kumuunga mkono Mbowe, tulipambana pamoja naye kipindi cha magufuli na tulisimama naye kwenye uchaguzi wa chama kwakuwa tulimuamini, lakini baada ya uchaguzi tumekuwa tukiishi kwa hali ngumu sana, tunaonekana waasi, tutakaa pembeni wao waendelee. Leo Mei 11, ninatangaza kuachana na chama, nitapumzika kwa kipindi hiki kifupi lakini sitaacha siasa. Najua timu ya G55 tuna ushawishi, tutakuwana na wananchi tutawashawishi na tutafanya siasa kupitia chombo kingine cha siasa.

Answari Kimaro Mjumbe wa Kamati ya TEHAMA Kanda ya Kaskazini
Mimi nilimuunga Odero, lakini sasa hivi kuna ugomvi kati ya pande mbili, hatuwezi kufika popote. Nina ushahidi, watu walipewa nafasi kwasababu wanamuunga Lissu mkono si sababu wanna sifa. Natangaza kuondoka CHADEMA na nnajivua vyeo vyangu vyote! Pia nawapa changamoto waende kwenye kata yangu pale, wakipata hata mtu mmoja wa CHADEMA Mungu afanye atakachopenda.


Wengine waliojivua uanachama ni pamoja na;

- Mwenyekiti wa Moshi Vijijini - Rose Masuruali
- Kumsapoti Mbowe siyo kosa - Nimejitoa CHADEMA, nitaenda kwenye chama kingine - si CCM

- Katibu wa Vunjo Joseph Mosha
- CHADEMA kulikuwa na jambo ninaloliamini, sasa hivi hakuna - Nimejitoa CHADEMA na najivua rasmi nafasi zote nilizokuwanazo, nitatafuta forum sahihi ya kwenda kuwasemea wananchi

- Katibu Same Mashariki - Magreth Mbwambo - Nimeihangaikia CHADEMA kwa hela, nguvu na jasho na hatukupata chochote. Zamani chama kilikuwa na upendo, sasa ni manyanyaso, nikipata sehemu ambako kuna mwanga nitaenda - Najiondoa CHADEMA

- Katibu Mwanga - Togolani Sinzira - Viongozi wa chama taifa wanakumbatia watu wanaotutukana, tutafakari pa kwenda lakini sio CCM - Najiondoa CHADEMA

- Katibu Same Magharibi - Haika Ngowi - Chama chetu kimekuwa cha wanaharakati na diaspora, hao ndio wanakishauri chama, hakuna tena upendo, chama kimekuwa cha matusi - Nimejitoa CHADEMA, na kujivua vyeo vyote, naenda kutafakari niangalie pa kuelekea lakini sio CCM

- Katibu wa Jimbo la Same Mashariki
- Nimehangaikia chama sana lakini matokeo yamekuwa haya, wakati natumikia chama nilishaletewa bahasha na chama tawala, nikaikataa, kwahiyo sitegemei kurudi huko, sina mpango na CCM, wale niliokuwa nawaongoza tutafute mwelekeo mpya. Ilinipa uchungu kutosaini uchaguzi halafu baadaye wanakwambia tutaangalia namna, hiyo namna ni ipi? - Nimejivua uanachama CHADEMA

Wawakilishi wa Manispaa ya Moshi (G55) kwa niaba ya wengine, Halmashauri ya Moshi na Vunjo (G55) Jasmine Minja, Pius Mrema, Haika Letuu, Lilian Kimei, Vicky Massawe Mwenyekiti BAWACHA Moshi DC sitaenda CCM, Fredy Shayo Katibu BAZECHA na Mweka Hazina nasubiri G55 iniambie inaenda wapi ili nami niingie, Jabir Weta - Tunaondoka CHADEMA sababu ya ubaguzi kisa tulimsapoti Mbowe, walitakiwa kumpa tuzo Mbowe na si tuzo ya matusi

G55 Temeke


Meza kuu inajumuisha;

Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Temeke - Herman Kiloloma najivua uanachama wangu CHADEMA pamoja na wenzangu kwasababu tumeona hatuko salama ndani ya chama chetu toka uongozi mpya upatikane, tunabaguliwa. Sababu nyingine ni ajenda ya chama kutoshiriki uchaguzi - mimi binafsi nilibaguliwa na Heche, watu 80 tuliokuwa nao hapa na wenyewe wanaondoka CHADEMA. Waliobaki tunawaheshimu na tunaowaacha waheshimu pia uamuzi wetu, tusishambuliwe na maneno. Tutawaita waandishi tutakapotaka kwenda kujiunga na chama kingine

Mwenyekiti Mstaafu Jimbo la Temeke Idi Mahuta

Mratibu wa BAWACHA Mkoa wa Temeke - Yvonne Haule
- Kokote utakapopita najulikana kama mama wa CHADEMA kwa uchungu sana, nawatakia wote wanaotaka kunifuata tunawakaribisha tutakapoenda- najivua uanachama CHADEMA

Mwenyekiti wa Kata ya Makangalawe - Josephine Mwenda - Najivua uananachama mimi na baadhi ya wananchi wangu amabo wananifuata.

Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke - Hamza Kinyema - Tumejitolea sana kwenye chama lakini sasa hivi kuna visa na visasi, kama sisi tunabaguliwa itakuaje kwa wananchi? Tunatukanwa sana kwenye magroup, nimezima simu siingii kabisa kwenye magroup sababu ya matusi. Tutashawishi na wananchi kwenye kwenye chama ambacho tutaelekea. Waandishi wa habari nahitaji kipindi maalum ili tuweze kuzungumzia mambo kwa undani - najivua uanachama wa CHADEMA,
 
Wakuu,

Mpango wa kupiga kelele kwenye media ili wasisahaulike unaendelea :KEKLaugh: hivi hawaoi walivyokuwa majinga? Ukiamua kumla chura hakikisha unachagua aliyenona, sasa unakula chura afu unachagua chenye kimedhoofu na utapia mlo, unamla na anakuua, inakuwa ni fezea:KEKLaugh::BearLaugh::BearLaugh:

Wacha tuendelee kukinga maji yanayovuja tukaflashie chooni!

Kwenye vyama vya siasa wanaoweza kukiangusha chama sio viongozi ni wanachama wenyewe.
 
Wakuu,

Mpango wa kupiga kelele kwenye media ili wasisahaulike unaendelea :KEKLaugh: hivi hawaoi walivyokuwa majinga? Ukiamua kumla chura hakikisha unachagua aliyenona, sasa unakula chura afu unachagua chenye kimedhoofu na utapia mlo, unamla na anakuua, inakuwa ni fezea:KEKLaugh::BearLaugh::BearLaugh:

Wacha tuendelee kukinga maji yanayovuja tukaflashie chooni!

Hao wasaka tonge wanao jiita G55 kwa kuwa walishatoka CHADEMA, kwa njia ya kuvuliwa uanachama na kujivua wao wenyewe hawana haki ya kutumia alama za chama (nembo, rangi, nk.).
 

Moshi, Dar na Morogoro​

Mpango wa kupiga kelele kwenye media ili wasisahaulike unaendelea :KEKLaugh: hivi hawaoi walivyokuwa majinga? Ukiamua kumla chura hakikisha unachagua aliyenona, sasa unakula chura afu unachagua chenye kimedhoofu na utapia mlo, unamla na anakuua, inakuwa ni fezea
Ina maana media za Dar hazisikiki Moshi na Morogoro au lengo lao kuzurura wamekosa cha kufanya Dar?
 
Leo watamsema nani? Jana ilikuwa zamu ya Lema. Sasa yule malaya Emma alikuwa mweka hazina wa kaskazini alikuja dar kufanya press na leo kule kwao viongozi wenzake wanafanya press. Au wanakutana kimafungu kutokana na mafungu ya mgao wa Abdul? Kila kundi na fungu lake?
 
Back
Top Bottom