Fursa ya kupeleka mchele nchini Rwanda

@UNSPECIFIED,sijui kwa awamu hii,lakini miaka ya nyuma hata tani kumi unakodi fuso unaingia zako kigali unauza
 
Hahaha nenda jukwaa la biashara na uchumi kuna mawazo mengi utashindwa wewe, biashara sio kwa kila mtu.
Najivunia kuwa mlinzi, usiku kucha, niko macho mchana kutwa nalala. Napishana na dunia, inaenda mimi narudi.
We achana na mawazo yao, tembea kifua mbere Magu yupo anapigania wanyonge kama mimi.
Sawa bana,afu usinitoe kwenye reli nia yangu ni kula madini ya Biz ya Wali huko Chigali, kwanini iwe inalipa kushinda DRC wewe tukana na utembee kifua nyuma ka unataka.
 
hii biashara inafaa upeleke mchele wa Kyela ambao ukipikwa mpaka mtaa wa pili wananusa harufu....
 
Huwezi kufanya biashara hiyo kama huna pesa ,namaanisha pesa sio una tani 60, unataka kupeleka mchele ng'ambo
Usipotoshe mkuu!! Watu hadi tani 30 wanapeleka sembuse tani 60!!!unapozungumzia tani sitini sio mchezo kama ni mchele hapo unazungumzia sio mtaji wa kitoto ni kama milioni 80!!!
 
hii biashara inafaa upeleke mchele wa Kyela ambao ukipikwa mpaka mtaa wa pili wananusa harufu....
Biashara za huko huwezi peleka mchele wa kyela, uuzaji wake ni mgumu sana, kwani bei itakuwa kikwazo!! Kule unapeleka wa kawaida, labda uwe na order maalum!! Huo wa kyela mfano uununue tsh. 1800!!hujaweka ushuru, usafiri, utauuza bei gani?
 
Biashara za huko huwezi peleka mchele wa kyela, uuzaji wake ni mgumu sana, kwani bei itakuwa kikwazo!! Kule unapeleka wa kawaida, labda uwe na order maalum!! Huo wa kyela mfano uununue tsh. 1800!!hujaweka ushuru, usafiri, utauuza bei gani?
Mkuu mchele wa kyela unafaa upelekwe kipindi kama hiki cha mavuno unakuwa very cheap coz debe la mchele linashuka mpk 25000/-.
 
Mimi nimeshawahi kupeleka mchele kule. Nilikua nachukulia Nzega kwa sababu ya bei nk.. Na kigali nilikua nauzia sehemu moja inaitwa Gikondo. Watu wengi hupenda kuchukulia kahama wana sababu zao. Ukitaka ufanye biashara kwa raha kodisha store yako kule.
Bei mimi nklikua nauza 50kg kwa Rwf 55,000 ni kama Tsh 138,000 hivi. Kwenye gari ilikua inaingia mifuko 660 ya 50kg. Gari moja unaweza kuiuza kwa muda usiozidi wiki kwa vile kule sio walaji sana wa mchele kama sisi.
NB: usiuze rejareja. Na biashara ya dagaa ni nzuri kule lakini kwa wanawake
 
Ukishindwa kule jaribu Bujumbura ila mchele uchukulie Mpanda.
Jaribuni na viazi, vitunguu na ndizi kule Lusaka ni bonge la dili.
Kidogokidogo jaribuni kuvuka mipaka na Mwenyezimungu atajaalia Inshallah.
 
Money money...we dada hustler sana i can bet my money on you ️TOP

Yaani nasema Mungu nipe pumzi..huku wananiangaliaga tu yaan..afu waniita mchaga😂😂wanasema wanawake wa kisukuma hawana mwamko kbs wa kuhustle..ila its true😉.. mie nikifika kila siku niwe naweka 200k ntakamilisha kbs my long term plans..huku ukiweza tu kujitoa kbs uhakika wa kupata even 200k@ day upo...toa ishu za madini.ntakuja pm tmr..
 
Ila wanyarwanda wamejaaje Kahana wananunua mchele
Habari ndugu wanajamii forum!

Wakati Tunaposubiri Ccm watoke madarakani 2020 jaribu pia kuendelea kutafta fursa hapa na pale kabla hakijanuka

Nimekutana na vijana wadogo kbs wameona fursa ya kupeleka mchele Rwanda...

nimejaribu kuongea nao wanadai lazima uwe na leseni ya Afrika mashariki..wajuvi wa mambo mngesaidia sana kuelezea hii leseni inapatikana vipi..

Jamani kuna watu wanapiga helaaaa..nimechoka mimi..nimechoka sana...!
Umewahi sikia kuna vijana wanacheza michezo ya 5,000,000/= per month?
Shimeee! wenye mitaji "yenyu"

Kocha Mkuu
@BILGER
 
Back
Top Bottom