SoC03 Fursa katika kutunza mazingira na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa

Stories of Change - 2023 Competition

Antony semsi

New Member
May 14, 2023
1
1
Mazingira ni jumla vitu vyote vinavyotuzunguka vikiwemo viumbe hai na visivyo hai.mfano wa viumbe hai ni pamoja na binadamu ,mimea na wanyama visivyo hai ni pamoja na mawe magari nyumba n.k
Mazingira hayo pia yamegawanyika tena katika sehemu mbili;
(1)mazingira ya vijijini
(2)mazingira ya mijini

images (1).jpeg
images.jpeg

Katika mazingira yetu mimea na wanyama tuna tegemeana ili kuweza kuendelea kuishi mimea inazalisha hewa ya okisijeni tunayotumia wanyama katika upumuaji na sisi binadamu tunazalisha hewa ya kabonidayoksaid inayotumika na wanyama katika usanisi nuru hivyo mazingira ni muhimu kwa mimea na wanyama.

Binadamu hutumia vyanzo mbalimbali vya nishati katika maisha ya kila siku vipo vyanzo amabavyo havileti madhara katika mazingira lakini vipo vyanzo vya nishati vinavyoleta madhara kwa mazingira na viumbe vyake

Nishati isyoleta madhara kwa mazingira na viumbe wake huitwa NISHATI JADIDIFU mfano;
1. Gesivunde
2. Umeme
3. Fueli

Nishati zenye madhara kwa viumbe hai na mazingira ni pamoja na
1. Kuni
2. Mkaa

Nishati jadidifu huweza kurejelezwa na kutumika tena tofauti na nishati isiyojadidifu. Asilimia kubwa ya matumizi ya nishati ni nishati isiyo jadidifu ambayo ina madhara makubwa kwa mazingira na viumbe hai

Madhara yatokanayo na matumizi ya nishati isiyojadidifu;
1. Kusababisha ukame kwa kukata miti
2. Kusababisha ongezeko la joto
3. Kuchochea mmomonyoko wa ardhi
4. Kuharibu muonekano wa mazingira
5. Kusababisha magonjwa katika mfumo wa upumuaji kutokana na moshi
6. Husababisha kifo mfano kulala na jiko la mkaa kweny chumba kisicho na mzunguko mzuri wa hewa

FAIDA ZA KUTUMIA NISHATI JADIDIFU
1. Haiharibu mazingira
2. Inapatikana muda wote
3. Ni rafiki wa mazingira
4. Ufanisi wake ni mkubwa

FURSA ILIYOPO KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA KUPUNGUZA MATUMIZI YA KUNI NA MKAA
Serikali imekua mstari wa mbele katika kuhimiza matumizi ya nishati jadidifu hasa kwa wakazi wengi wa vijijini japo umeme haujafka sana maeneo mengi ya vijijini hivyo wanahimiza sna matumizi ya gesii.je kwenye gesi kuna fursa gani ambatana na mimi.

GESI ni mojawapo ya nishati ambayo ni jadidifu na huwa imewekwa kwenye mitungi mbalimbali kulingana na ujazo wake.
images (4).jpeg

Gesi katika mitungii ina gharama zake wakati wa kununua na pia wakati wa kujaza inapokua imekwisha kwa utafiti nilioufanya kama ukijikita kwenye biashara ya kuuza na kusambaza gesii faida ni kubwa ukifanya kwa ubunifu amabao ni pamoja na;
1. Kuwa na bussiness card kuhusu biashara yako na mahali ulipo
2. Fanya free delivery kwa wateja wako wa karibu
3. Kuwa na mzani wa kupimia gesi kabla hujampelekea mteja
4. Tembelea hoteli migahawa makampuni omba ubia/tenda ya kuwasamabazia gesii
5. Uza pia vifaa vya majiko ya gesii
6. Uwe na fundi wako wa masuala ya majiko ya gesii na vifaa vyake
7. Kuwa na kauli nzurii kwa wateja
8. Waskilize wateja
9. Uwe na mawasiliano ya uhakika ambayo mteja anaweza kupiga simu na kupelekewa mtungii wake

Hakika kupitia fursa hiyo utaweza kutengeneza ajira kwa watu wengii na pia utakua umesaidia kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na kupafanya DUNIANI kua mahali salama pa kuishi.

Mpaka unaskia COP 22 yote hiyo ni katika kuhakikisha DUNIA inabaki kua salama kwa viumbe hai
Mabadiliko ya tabia ya nchi yanaanza kidogo kidogo hapo ulipo utaanza na mti mmoja unakata halaf mwingine hatimaye msitu hivyo ni jukumu letu sote kushiriki kupunguza kama si kuacha matumizi ya kuni na mkaa PAMOJA TUTAKUA TUMEIUNGA MKONO SERIKALI YETU.

images (3).jpeg
 
Back
Top Bottom