Furahia Uhuru ulionao sasa, ni zawadi kubwa sana maishani mwako

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,989
Nilikuwa sina mpango hata wa kuandika Hii thread lakini naiandika kwa ufupi sana baada ya kupita instagram na kukutana na clip hatari za wahuni wakiwa wanahamishwa gereza huko El salvador

Kuhamishwa kwao,mikao yao yani imenikumbusha Moment hatari sana nilizowahi pitia miaka ya zamani hiyo

Gusa Link hapa chini uone watu wanavyokimbizwa mchaka mchaka



Magereza ni sehemu ambayo hakuna haki kinachofanywa kwa hao raia ndio kinachofanywa na magereza mengi nchi karibia zote sema ni siri zao hawa tu ndio wameamua kutuonyesha.

na hii imeonyeshwa ili walioko uraiani El salvador wale makundi ya wahuni wabadilike au wahame nchi maana wameonyeshwa namna kinavyonukishwa kwa wenzao.

Ukitazama hizo video utaona Baadhi ya mambo yafuatayo

KUKIMBIA
Huu ni utaratbu uliowekwa na magereza makusudi kabisa ili mfungwa asiweze au asipate muda wa kuangalia pembeni kujua gereza limejengwaje limekaaje,yani ni mchaka mchaka

27666080-8258201-Gang_member_prisoners_are_rushed_out_of_their_rooms_during_the_m-a-53_1587907...jpg


KUANGALIA CHINI
A
skari nao walizingatia usalama wao,hivyo unapoambiwa head down yani kichwa chini maana yake ni marufuku kumuangalia askari usoni maana huchelewi kumkariri halafu wahuni wenzako wakija ukawasimulia askari yukoje wao wakamjua wakaenda kufanya kazi ya roho mbaya huko nnje,hivyo walizingatia hilo

chi.jpg


JINSI YA KUJIPANGA na KUKAA CHINI
Hii ni njia ambayo inatumika ili kurahisisha hesabu wakati mnahesabiwa kwahiyo kukaa chini magereza ni kauli mbiu sio ombi,na sio tu wakati wa kuhesabiwa ila ukiwa jela Kukaa chini ni 1 ya sheria, Ukiinuka ni either unaenda chooni au kuchukua chakula AU umeitwa Admission,ila huwezi kuwa ndani ya eneo la magereza halafu eti unasimama simama, huna cha kufanya tafuta sehemu kaa chini pigeni story na wenzio,ukikutwa umesimama "unalo".

panga.jpg

KUNYOA KIPARA
Magereza kunyoa Kipara ni amri,ukienda na rasta zitadondoshwa ukienda na kipilipili watakusaidia kukishusha chini, na usifikiri kuna saloon magereza,ni Amri tu inatolewa ikifika MUDA wa kuingia kulala uwe HUNA nywele hata 1, sasa utanyolea wembe, utanyofoa nywele, utajua mwenyewe haiwahusu.

Uzuri ni kwamba jela wema hawakosekani atakuepo mmoja atakupa wembe wake utanyolea. Ndio mana nasema kila siku kama unampenda mtu wako cheza michezo yote ila usimpeleke Jela maana anaweza kwenda kuchukua ugonjwa ambao kama si wewe kumpeleka jela asingeupata.

kipara.jpg


KIFUA WAZI,KUWA WAZI JUU
Hii ni njia mojawapo ya usalama kwa wafungwa wenyewe na askari,hii imewekwa makusudi ili usiweze kuficha kitu ndani ya shati,kwahiyo ukishuka tu kwenye gari kutoka mahakamani kabla hujaingia magereza Shati unatoa, mkiingia ndani kabla hamjaingia kulala shati mnatoa yani nadahani walitamani wafungwa washinde bila mashati sema ndo hivyo tena kuna haki za binadamu.

shat.jpg


KUKAA KARIBU KARIBU
Sio kwamba hamna nafasi ila JELA wanachofanya ni kukunyima uhuru,na hii wanaifanya makusudi ili hata ukitaka kufanya jambo utamgusa mwenzako na mtashtukiwa,maana mtatikisika kama ulitaka fanya chochote kitashtukiwa.

kwahiyo hata kama itokee gereza zima wamalize kifungo mbaki wafungwa 10 na vyumba vya kulala vipo 20,mtahukuliwa 10 mliobaki mtatafutiwa chumba kidogo chakuingia watu 8 mtawekwa nyie 10 ilitu mbanane,sheria yao iwe imekamilika,na hiii sio kwenye kukaa tu hiyo hadi kwenye kulala yani mbanano ndio kauli mbiu ya GEREZA LOLOTE.

kukaa karibu.jpg


Kwa ufupi hayo ni baadhi ya mambo na taratbu za Magereza,narudia kusema Furahia na thamini sana uhuru ulio nao maana ni zawadi kubwa sana Uliyo nayo ambayo yawezekana hujaijua.

usije ukakubali awae yeyote akakupokonya zawadi ya uhuru wako ni heri ulale njaa,utembee peku,ukose pakulala lakini uwe huru kwenda na kufanya lolote. Magereza ni DUNIA nyingine kabisa tofauti na hii tuliyopo sasa.

Nimewakumbusha wote ambao labda mmejisahau, epuka vitendo visasi vitakavyokusababishia ukapokonywa zawadi kubwa kuliko PESA na MAJUMBA na UFAHARI wowote ule kama UHURU.

UHURU hauna cha kulinganishwa nacho,Uhuru ni zawadi itunze ithamini na iheshimu.

#WASIKUZOEEElakini

Isikieni Magereza/JELA kwenye mitandao tu na kwenye media ila Usiombe wala usijaribu kunusa hayo maeneo.
 
Afande makalo wa kirumba central mshe*Zi sana yule bwana,ikifika wakati wa kulala usiku anamuamrisha nyampala achote maji chooni amwage kwenye sakafu ili watu walale kwenye maji.nilikaa mule siku 3 ila nilitoka nimekonda nimebaki kichwa tu!!
 
Hawa wanawatreat hivi kwasababu ni wafungwa hatari sana. We waone mitatoo kama mayakuza.
Mara kadhaa wanachapana wanauana kwa mamia gerezani.

Magenge ya cartel huwezi wapeleka soft ni ubabe ubabe tu maana hawa watu kuua kwao ni sawa na kuvuta fegi tu.

Raisi wao yule bitoz aliyeanzisha account za bitcoin kwa kila.mwananchi na akaishia kuchoma mabilioni ya pesa za serikali kwa sababu it didnt work alipitisha marshal law hivyi anaweza kumkamata na kumfunga mtu yeyote, amejenga magereza mengi na wengi wametupwa huko mpaka yamejaa balaa.

Naona west wanamlaumu sana ila anajaribu kusafisha nchi maana nchi imejaa magenge ya wahalifu yani ilikuwa ni moja ya sehemu hatari zaidi duniani kuliko hata nchi zenye vita.

Kwa sasa uhalifu umeshuka kwa 56%.

Nilikua sina mpango hata wa kuandika Hii thread lakini naiandika kwa ufupi sana baada ya kupita instagram na kukutana na clip hatari za wahuni wakiwa wanahamishwa gereza huko El salvador....
 
Afande makalo wa kirumba central mshe*Zi sana yule bwana,ikifika wakati wa kulala usiku anamuamrisha nyampala achote maji chooni amwage kwenye sakafu ili watu walale kwenye maji.nilikaa mule siku 3 ila nilitoka nimekonda nimebaki kichwa tu!!
😄
 
KUANGALIA CHINI

ile tumetoka kukaguliwa pasport zetu palee bet bridge na kugongewa mihuri ya kuingiza SA ilikuwa kama saa 7 usiku tukarudi kwenye basi tulilokuwa tukisafiri nalo ilikuwa mwendo kama wa lisaa limoja na nusu nafikiri ilikuwa saa 8:30 au saa tisa kamili usiku

Ndipo kati ya abiria mwenzetu alipoomba kwenda kujisaidia alibanwa na haja dereva ilibidi amsaidie ashuke akajisaidie ndipo aliporudishwa kwa kasi ya ajabu na vipande kama vitatu vikiwa na bunduki tulianza kupukutishwa/kuibiwa sim na pesa huku wazee wa kazi wakipita city moja moja kutusachi huku akikuwekea bunduki kichwani; MUNGU UTULINDE WATOTO WAKO WATULIVI

HAPO ILIKUWA; don’t look at me, yaani usiniangalie huku anakwambia angalia chini:

Nilicheka sana baada ya kuibiwa na wale majambazi kuondoka bila ya kumdhuru yeyote kwenye basi lile,

Kwenye siti ya watu watatu tulikaa wanaume wawili na kidada kimoja sasa hapo nishakula kipondo cha kutosha na kujibana bana na kutoa nilivyotoa na nilivyoficha ALHAMDULLILLAH ndio kaka jambazi akaamia kwa huyo dada tuliyokaa nae city moja alikuwa akiambiwa DON’T LOOK AT ME- dada alikuwa haelewi chochote alizidi kumkodolea macho yule jambazi/kibaka daah ikabidi nimwambie huyo anakwambia usimuangalie angalia chini dada atakuua huyoo ndipo dada akashituka na kuanza kuangalia chini maana alikuwa akipigwa kwa kutoelewa daah kitambo sana - MR.FINISHI alikuja kufanya kazi yake ya kufinish daah hatari

Sister nimekumisi sana kama unaona ujumbe huu najua utakumbuka kitu em ni dm tupige stori miaka minne sasa imepita
DAAH MAISHA HAYAA MMMH
 
Bro maisha yana Mambo mengi ila uhuru ni kitu muhimu.
👉Imagine niliwai kosa kuuliwa, kisa nilikimbia kipigo home, so nikaenda kulala sehemu wanayotunzia nafaka dah sitosahau. Kuna mzee alipiga the hell out of me, lakini walinijua ila hawakuwa na huruma. F uck them

Nilipelekwa polisi, sitosahau aisee maana niliwaza story za kuvunjwa na kupasuliwa lock up but nilitolewa asubui chap
 
Kuna tukio niliwahi kulifanya mwaka 2004, nikapelekwa butimba na mzee wangu akakomaa nisichomoke kwa dhamana for 28 days.

Jesus Christ, hapo nilikua mahabusu tu, niliyo yaona shetani akasome wallah
Umekaa Butimba, Pale Pagumu mzee
 
Afande makalo wa kirumba central mshe*Zi sana yule bwana,ikifika wakati wa kulala usiku anamuamrisha nyampala achote maji chooni amwage kwenye sakafu ili watu walale kwenye maji.nilikaa mule siku 3 ila nilitoka nimekonda nimebaki kichwa tu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom