Furahia Facebook BURE ukitumia mtandao wenye kasi Tanzania

Vodacom Tanzania

Official Account
Aug 12, 2013
320
107
Habari Wakuu,

Mnafahamu kwamba hakuna kinachofurahisha kama kuwa hewani muda wote ukitumia Vodacom. Sasa unaweza ku-share picha, ku-like, ku-comment, kucha mewanzo mwisho bure kabisa bila malipo yoyote ya data. Kuwa hewani muda wote ukiwasiliana na washkaji na familia kwenye Facebook bure kabisa na mtandao wenye kasi zaidi Tanzania.

Unafahamu ofa ya kutumia Facebook bure?
Vodacom inatoa ofa ya kutumia Facebook bure kwa wateja wake wote. Watumiaji wote wa Vodacom wanaweza kufurahia Facebook kwenye simu zao au kupitia App ya Facebook bila malipo yoyote.

Nani anaweza kutumia Facebook bure?
Mteja yoyote wa Vodacom anayetumia huduma ya Prepaid, hybrid au postpaid anaweza kufurahia ofa hii ya aina yake. Unachotakiwa kufanya ni kutembelea www.facebook.com au unaweza kutumia App ya Facebook ufurahie ofa hii bure.

Unatumia vipi Facebook bure?
Ili uweze kutumia Facebook bure na Vodacom ni lazima uingie kwenye akaunti yako kupitia www.facebook.com kwenye browser [kisakuzi/kivinjari chochote] yoyote au kupitia App ya Facebook kwenye smartphone yoyote.

Unaweza kfungua akaunti ya Facebook kupitia www.facebook.com jaza jina lako, namba yako ya simu au barua pepe na utengeneze neno siri. Ndani ya dakika 5 tu utaweza kuanza kutumia Facebook ukiunganishwa na uwapendao mkifurahia pamoja bure kabisa.

MASWALI NA MAJIBU
Facebook ya bure ni nini?
Facebook bure ni huduma kutoka Vodacom kwa wateja wake wote. Wateja wa Vodacom wataweza kutumia Facebook bure kabisa bila kulipia kifurushi chochote. Wateja wataweza kupakia au kuangalia picha, kuchati, ku-post, ku-comment, ku-like na ku-share bure.

Ni wakati gani ninaweza kutumia Face book bure?
Watumiaji wote wa Vodacom wanaotumia huduma ya prepaid, postpaid na hybrid wenye simu zenye uwezo wa intaneti watakuwa wamekidhi mahitaji ya kutumia Facebook moja kwa moja bure kabisa. Mteja hatohitaji kununua bando au kuongeza salio ili kutumia Facebook kwa huduma za bure. Hata kwa wateja ambao hawana salio kabisa wataweza kufurahia Facebook bure.

Mteja anwezaje kupata Facebook bure?
Wateja wanaweza kupata Facebook kupitia http://facebook.com App ya Facebook ya Android, App ya Facebook Lite ya Android, App ya Facebook ya iphone na pia Facebook kwenye simu za kawaida. Kwenye App ya Facebook ya iphone wateja hawataona picha ya tangazo “Facebook bure kutoka Vodacom”, lakini wataweza kutumia bila kilipia.

Nitajuaje nina tumia Facebook bure?
Utakuwa unatumia Facebook bure ikiwa juu ya akaunti yako ya Facebook utaona “Facebook bure kutoka Vodacom”. Kwa wateja wanaotumia App ya Facebook kwenye iphone hawataona picha ya tangazo lililoandikwa “Facebook bure kutoka Vodacom”, lakini wataweza kutumia Facebook bure.

Je, Facebook Messanger ni bure?
Ni sehemu tu ya Facebook messanger ambayo ni bure. Utaweza kutuma au kupokea ujumbe na kupakia au kuangalia picha bure. Kupakia na kuangalia video kwenye Messanger sio bure, uatalazimika kulipia. Mbali na hapo, ujumbe wa sauti kupitia Facebook Messanger pia sio za bure.

Ni bure kama nikiangalia video?
Hapana. Ukiangalia video kwenye Facebook utalazimika kulipia kulingana na kiwango cha matumizi yako. Ikiwa umeanza kuangalia video kwenye Facebook ukitumia simu yako au App ya Android, utaona ujumbe unaokuarifu kuwa utatozwa kiasi cha malipo kulingana na matumizi yako. Kwenye App ya Facebook kwenye iphone hutapata ujumbe huo lakini malipo yatakatwa.

Je, ni bure kama nikibofya linki kwenye Facebook?
Hapana. Taarifa zozote zilizo za Facebook ndio zitakuwa bure mbali na hapo video nyingine zisizo za Facebook zitahitajika kulipiwa. Kwenye App ya Facebook kwenye Android au tovuti http://facebook.com utapokea ujumbe kukuarifu kuwa utatozwa kiasi cha malipo kulingana na matumizi yako. Kwenye App ya Facebook kwenye iphone hutapata ujumbe huo lakini malipo yatakatwa endapo utaangalia video zisizo za Facebook.

Unaweza kutumia Free Basics bure unatumia huduma ya roaming?
Hapana. Free basics inatumika Tanzania tu na sio ukiwa unatumia huduma ya roaming.

Je, ni bure kutumia Facebook kwenye WAP au BlackBerry?
Huwezi kutumia Facebook bure kwenye WAP na BlackBerry

upload_2016-10-20_10-32-54.png
 
Je ninawezaje kujitoa ktk huduma hii ya facebook ya bure. Siihitaji huduma hii katika simu yangu... I wonder kwa nn mmeniunga automatically.
 
Mmechelewa sana kuleta hii huduma, washindani wenu wameileta kitambo nyie ndio mnazinduka
Ila hii haitoshi, huduma zenu za vifurushi ni ghali sana, watu wanawakimbia kwa kasi msiporekebisha bei zenu,
Mwenyewe voda naitumia kwa huduma za M pesa tu sasa, intaneti na kupiga natumia mitandao mingine kwa kuwa ipo na gharama nafuu na kwa kasi nzuri pia
 
Mie sipendagi sms zenu mara umeshinda hiki mara umepata hiki nakereka sana, wakati mwingine labda nasubiri majibu ya sms ya muhimu halafu ikiingia meseji nakuta na hayo mameseji yenu:(:(:(
 
Safi sana VodaCom

Ni hatua nzuri sana japo wenzenu walianza mapema sana.

Tatizo jingine liko kwenye bei ya vifurushi vya internet, mmevikwanyua mno aiseeee.
 
Back
Top Bottom