Furaha!

Ikunda

JF-Expert Member
Jul 12, 2010
718
151
Amani iwe kwenu wana JF,

Napenda kuwashikrikisha ili wapendwa ( tulichambue, tuelezana, tufundishana)

Katika jamii yetu kila binadamu anahitaji furaha katika maisha yake yote, lakini furaha iyo yapatikana wapi? nani anaepaswa kukupa furaha??

Kuna kamsemo tumezoea kusema, mke mwema, baba bora hawa watu wanapatikana vipi?? utawajua vipi??

Kuna mtu yeye anasema mke mwema awe na mdomo mdogo, maana yake asiwe mwanamke wa kuongea akiaanza kuongea hasubuhi hadi hasubuhi anaongea tu,
(macho makubwa), awe anataza mbali, mbunifu n.k
(masikio madogo), awe ni mtu wa kusikiliza na kupambanua mambo, sio kaambiwa kitu na shogayake yeye huyo ananunaaaa (miguu iwe mizito kama ya tembo), mwanamke unatakiwa kutulia nyumbani kwako sio kila siku kiguu na njia shughuli isikupite, sare wewe n.k

mume bora awe anaejua majukumu yake.

Mwisho tunatakiwa furaha ianzie na wewe.

Wewe mdau wa JF, unaweza kuongezea,unahitaji mkeo awe vipi, mumeo awe vipi ili furaha itawale nyumbani kwako?

nawakilisha.
 
amin...amin...amin_nakuambia,...furaha ya kweli na ya kudumu iko ndani yako.

nashukuru kwa kulifahamu hilo, ila wako wanaosubiri kutafutiwa, na hapohapo wanawakwaza wengine
 
nashukuru kwa kulifahamu hilo, ila wako wanaosubiri kutafutiwa, na hapohapo wanawakwaza wengine

Sio wewe unaeongelea furaha inayoletwa na mke/mume? Masikio sijui yawe madogo , macho sijui makubwa. Ukubwa wa pua unaguarantee wingi wa kamasi.

Na usipokua na furaha wewe mwenyewe hata ukipewa dunia nzima uifanyie chochote upendacho hutofurahi kweli.
 
hahaaaa Lizzy bwana habari yako?

Lizzy umesoma vizuri na kuelewa?

Labda nikuulize swali, Furaha ktk ndoa nani anaepaswa kuileta?? wewe, mume au watoto?
 
Furaha yangu ninayo mwenyewe,
Hakuna wakunipa furaha isipokuwa mm mwenyewe,
Nikiweza kufurahi mwenyewe ndipo nitaweza kupokea furaha kutoka kwa mwingine.
 
Furaha yangu ninayo mwenyewe,
Hakuna wakunipa furaha isipokuwa mm mwenyewe,
Nikiweza kufurahi mwenyewe ndipo nitaweza kupokea furaha kutoka kwa mwingine.

Amen.

Huwa unakasirika?? partner wako hasipotimiza wajibu wake kama mume utakuwa na furaha?
 
Back
Top Bottom