Furaha yangu mimi kulia... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Furaha yangu mimi kulia...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtaftaji, Jun 7, 2012.

 1. M

  Mtaftaji JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 207
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Natumai wengi wenu mmelala kwa kua ni ucku mkubwa,bat kwa upande wangu naic ni mchana kwani ndio natoka kufua now nguo zangu,sitoweza kukufuru na mshkuru MUNGU sana na nautumikia mtihani wake alonipa,siwezi jua kipi ameniandalia kizuri kwenye dunia au akhera yangu(maisha baada ya kifo)kwani nabii Ayubu aliumwa kwa miaka mingi mpaka mke na familia yake ikamtenga na wala hakukufuru na zawadi yake kupitia mtihani wa maradhi mungu alim2nukia pepo wakati kuna walopata uzima duniani wakamsahau mungu wakaonja moto,nachotaka kusema mtihani wowote unakufanya uwe karibu na mungu wako,uwe mtihani wa maradhi,riziki,ndoa n.k,naitaji dua zenu wana jf kwani nimemaliza waganga na wagaguzi,hospital bila mafanikio,hapa nilipo mikono inauma kwakufua kila siku,mda huu na kiu lakini nashindwa kunywa maji kwasasa np macho ila nikifumbatu jicho haja ndogo inanitoka bila hisia,ila nikilala mchana wala hii hali hijitokezi ni ucku tu,nashkuru mungu ni mzuri wa sura kiasi changu nilicho jaaliwa wengi wananitaka kwa ndoa ila na sita kwasababu ya tatizo langu huenda kilio kikazidi katika ndoa,nilijaribu kueka post yangu ya kutafuta mwenza mwenye sifa kama zangu bila mafanikio,hua naumia sana ndugu na majirani kujua matatizo yangu na kunibeza mda mwengine hua nahic nawatia aibu wazazi wangu,hua nasubiri watu wote walale ndionifue naona haya kuanika kwenye kamba kwa kuepusha maswali kwanini kilasiku nafua?nguo na anika ndani kwa hiyo hukauka bila kupigwa najua kwa hali hiyo kila cku na nusurika kunga'twa na tandu au nnge hufuata ubaridi katika nguo,ebu vuta picha kipindi hiki cha kipupwe âlafu unaamka ukiwa umeroa unaskia baridi kiasi gani?na nakoga sa 11 kabla watu hawajaamka hua baridi mda huo sana naomba mungu niepushe na nimonia.Wana jf mshukuruni mungu kwa maneno na vitendo kwa neema ya uhai,uzima,rizki,mali,watoto,ndoa,n.k kuna watu hawana.ucku mwema!
   
 2. D

  Doreen22 JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 475
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hi, pole, embu uliza madoctor humu Fj, jitahidi kuwa happy, hata kwa kuangalia movie za kuchekesha, usijiumize mwili wako kwa huzuni, usiku mwema na kwako pia
   
 3. R

  RockyII Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanza pole sana
  umejaribu kwnda kwa madaktari au wajificha tu ndan fanya ivyo kwanza....
  doreen kasma cha maana jaribu kupunguza mawazo, usikae sana pekee yko...
  Ucku mwema.
   
 4. majorbuyoya

  majorbuyoya JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,815
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Dada pole sana na unatakiwa kuondoa hofu juu ya tatizo linalokusumbua. Waganga na madaktari wanaweze kushindwa kutatua hilo tatizo lakini kwa Mungu hakuna kinachoshindikana. Tulia na utafute hospital ya makini ktk matibabu, nina imani Mungu atakusaidia kurudi katika hali yako ya kawaida ili ufurahie maisha sawa sawa na kusudio la Mungu.
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Dada pole sana kwa tatizo lako.
  Na kweli ni mtihani, kutokana na jinsi ulivyo eleza inaonekana wewe ni miuslamu. Kama umeweza kwenda kwa waganga natumaini waweza kwenda kwa maombezi.

  Mimi huwa naangalia channel za dini na hasa Emmanuel TV, tatizo hilo watu wengi sana wanalo. Na wengi wakiombewa wanapona kwa ni evil spirit tu ambao hawataji uishi maisha ya kawaida.

  Kuna watu wanaombea, ila si wote wana karama za kuombea watu na kupona. Waso na karama mara nyingi humtupia lawama muonbewaji kuwa imani yake haba (ingekuwa haba angefunga safari). Hivyo sina ushahidi juu ya wa hapa bongo nani mwenye karama nani hana. Ungeweza ungeenda Lagos Nigeria (process ukitaka nitakuPM), la kuna walioenda husali kila ijumaa na kuombea watu.

  Kama uko interested niambie nikutafutie details kukicha wapi wanapatikana.

  Mwisho pia kama hautajali nitumie Majina yako nitume prayer request thru email au sms, au wewe mwenyewe waweza tuma hiyo prayer request. Ingia <www.scoan.org>

  Kumbuka matatizo mengi tuliyonayo root cause ni shetani, hivyo tunapaswa kumkataa kabisa pamoja na fahari zake!

  Niko nawe ktk hili!
  Pole mpenzi!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Pole sana tafuta wataalamu wakusaidie usikate tamaa mapema hivyo.
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ......dah, kweli kusoma si kuelewa. Sijajua unakilio gani hapa. Una weak bladder?...
   
 8. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  This is so sad. Pole saana. Mungu akupe Imani...
   
 9. YNNAH

  YNNAH JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,663
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Pole sana ndugu yangu..,last week niliona post kule jf doctors inazungumzia hilo swala na utatuzi wake. Hebu kasome huenda ukafanikiwa. Kila la kheri,ila usiwe mnyonge utapona inshaallah.
   
 10. Bufa

  Bufa JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 4,167
  Likes Received: 3,371
  Trophy Points: 280
  Pole sana ila usikate tamaa endelea kutafuta dawa utapata tu siku moja Mungu yupo.
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Dada,kwanza nakupa POLE,pili usijuchukie,hilo ni moja,pili amini tatizo lako litaisha MUNGU NINAEMUAMINI NI MWENYE UPENDO.Umezungumzia waganga sijaona mahali ulipotaja hospital,kama hujaenda nenda.Pia jaribu kuwatafuta wataalam wa saikolojia na utambuzi wakujengee kujipenda na kujiamini.Baada ya hayo mtafute DAKTARI WA MADAKTARI WOTE,YESU KRISTO,hakuna ugonjwa uliomshinda na utakaomshinda huyu.Msikilize mke wangu mtarajiwa Kaunga hapo juu!
   
 12. mapanga3

  mapanga3 JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 659
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 180
  pole sana dada binafsi nawiwa kukusaidia, kwakuwa umesha kwenda kwa waganga na waganguzi bila mafanikio ningekuomba ufanye jambo moja, nenda kanisani kwaajili ya maombez, Mungu hakukuumba uishi kwa kudhalilika bali hizo n hila za adui shetani, kama unahofia kwenda kanisani ni pm ntakupa namba za mchungaji ambaye anaweza kukuomkea hata kwa simu na tatizo likaisha na kama utakuwa tayari kwenda kwenye maombi niambie nikuelekeze mahali ambapo waweza kusaidiwa.
   
 13. M

  Mtaftaji JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 207
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Furaha yng itapatikana kati ya haya yafuatayo,kupata kazi ili kuweza kunua materialdepers)yatakayonipunguzia adhabu ya kufua,au nipate mume atakae kua na ttz km lng ili iwe hamna wa kum isolate mwenzk,lkn hili litazaa tatizo ktk ndoa kwani huenda 2cpendane bali matatizo yakawa yametueka pa1,nirahic kujitokeza kwa cheating na mwisho wk ni maradhi au kuzaa msongo mwngn wa mawazo,kuna kipindi akili yang ilintuma niolewe na m2 mzima alitmka mwnyw antk kunioa nikakubali akaja ni chumbia,b&#259;da ya hapo nik&#259;amua kumwambia ukweli wa tatizo jibu lake lilikua ucjali ntakua nawe kwenye shida na raha nikafarijika huzuni ckuijua tena,nikaic umri wake busara na hekima itakuepo ksb alinizidi miaka 20, visa vikaanza nimevumilia nimechoka nikakata mawasiliano ya cm mpaka sasa ni mwezi wa 6 juzi kati ndio anmtuma mtu atusuluhishe kwa kukwepa aibu familia yng itamchkuliaje kunipotezea kwake, now nimepata serengeti mwnzangu 2mepishana mika miaka 3,annipenda sn alf family frend nikimwambia akilichkulia negative c ntazidisha kidonda na pata picha KAZI ndoitakua faraj&#259; kwangu na kuondosha kero kwa mwezi wangu na pia huenda KAZI ndo ikawa mume wangu mungu ndo mjuzi wa may future life.
   
 14. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,377
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Pole sana dada nakumbuka nilivokua o level kule iringa kulikua na rafiki yetu anatatizo kama lako,tulikaa na washkaji ili tuone jinsi ya kumsaidia kweli tulifanikiwa kwan tulikubaliana tuwe tunamwamsha kukojoa usiku pale tu mtu unapokumbuka hivyo tulifanya hivyo hata kama alikua ammeamshwa dakika 5 au 2 na tulimsimamia hadi akojoe, yaani jamaa alikua mtata kuamka ila tuliweza kwani mwisho wa siku ile sumbua sumbua ilimwingia akilini akazoa kwa miezi 3 tu hadi leo jamaa yupo chuo anatushukuru sana kwani anasema nyumbani hadi alitengwa kutokana na tatizo lake na alipona tukiwa form 3.
  USHAURI WANGU KAMA HUNA MTU WA KUKWAMSHA USIKU KILA MARA ILI UKAJISAISIE HEBU TEGESHA ALARM KILA BAADA YA DK KADHAA ILI UWE UNASHTUKA KWENDA KUJISAIDIA THEN WAONE MADOKTA NA YOTE TISA KUMI NENDA KWENYE MAOMBI KAFANYIWE MAOMBI LABDA KUNA MKONO WA MTU ULIFANYA KOSA KUBWA KWENDA KWA WAGANGA WA KIENYEJI HATA KAMA DINI YAKO HIRUHUSU WE NENDA KWA MAOMBI DADA KWENYE KUTAFUTA TIBA HAKUNA KUOGOPA MIFANO TUNAYO!
  AMANI YA BWANA IWE NAWE...
   
 15. Master jay

  Master jay Senior Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 187
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  0786124678 mtume rojas wa arusha, mpigie atakusaidia. Weng wamepona kwake
   
 16. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,646
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Pole sana jtahidi na maombi na pia nenda CCBRT
   
 17. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,135
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  Kweli kabla hujafa hujaumbika,pola sana dada,usikate tamaa endelea kumwomba Mungu huku ukitafuta wataalamu wa hilo tatizo lako.
   
 18. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  jamani pole sana! MUNGU MWEMA AKUPONYE!
   
 19. mbalu

  mbalu JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pole sana Dada kwa tatizo hilo, jitahidi uwaone wataalamu wa saikolojia watakushauri nini cha kufanya.
   
 20. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mpendwa, binafsi matatizo yako yamenigusa mno na kusikia uchungu kuwa kumbe kuna watu wengine wanapata shida kiasi hiki nyakati za usiku na wakati wengine wakienjoy usiku wao bila vikwazo.

  Kama alivyosema Kaunga, tatizo lako linaokena kutibika. Jaribu kwenda kwenye hosp kama CCBRT, KCMC na Muhimbili kuna madaktari bingwa wa njia za mikojo na saikolojia. Pia jaribu kuhudhuria mikutano ya maombezi kwa yeyote yule ambaye una imani na amani naye na kuendelea kumuomba Mungu kwa ajili ya hilo tatizo.

  Mimi pia nitaendelea kukuombea Mungu akuponye kila nikipata nafasi ya kufanya hivyo. Usihuzunike sana wala kukata tamaa, tuko duniani na dunia yenyewe ndo kama hii imejawa na dhiki za kila namna.

  Mungu akutie nguvu, na upone haraka.
   
Loading...