Furaha huletwa na nini?

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
Wadau mi nimekosa majibu naomba mnipe mawazo.Kumbuka ukiwa na mipesa mingi presha na mawazo yanakuwa juu,hapa furaha hakuna.Utakuwa na mke/mume mzuri lakini kilasiku ni matusi au ngumi na mateke yaani kwa kifupi ni kuwa huna amani wala furaha ya maisha.Ukiwa maskini ndio kabisa kwa kuwa kila nukta unawaza namna utapata fedha za matibabu,chakula, mavazi na malazi bora.Je, inawezekana kuwa na mawazo kisha ukawa na furaha? Je,ni nini kinacholeta furaha?
 
Pesa ufunguo wa furaha pia huleta mapenzi
Walioikosa huhaha na wakujiona wapuuzi
Wakiwanazo huja furaha na kuwaridhisha vipenzi
Hata uwe na utanashati pila pesa hupendeki


Ajabu na kweli ya furaha haijapa mgunduzi
Hata mie nastahamili na moyo kupata ganzi
Ukiwanazo utadhani wapendwa kwa udhati na mapenzi
Kupenda hakutoshi kitu, pipoz wanakataka mkwanja.

Penzi hapewi wa mkono wa birika nimefanya ugunduzi
Wanawake ni waroho kwa pesa wanaume hufanya ushenzi
Kama huna pesa furaha ya kweli kuipata huwezi

 
mkuu furaha ni maisha ya upendo na amani kwa kila mtu ukiwa na uhuru wako na afya njema,ukiridhika na ukipatacho na ukakipangilia kwa maisha ya kesho na kujiweka tayari kwa lolote huku ukimcha mungu nina hakika utafurahi wewe na wanaokuzunguka!
 
'Maisha ni mchanganyiko wa tabu nyingi sana, zinazoambatana na chembe ndogo sana za raha'
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom