Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,395
- 3,499
Wakuu sauti iliyopzwa imemfikia Waziri Dkt. Gwajima D Wanafunzi hao kurudi shule baada ya kupita kwenye programu ya marekebisho tabia.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema wanafunzi wa kike mkoani Tabora waliofukuzwa shule kwa makosa ya kujirekodi picha za utupu, watapelekwa kwenye programu ya marekebisho tabia kisha watarejeshwa katika shule nyingine. Waziri Gwajima amesema Serikali inapochukua hatua ni kwa lengo la kufanya marekebisho ya tabia na kuwalinda watoto.
"Kwa ufupi ni kuwa, hawa ni watoto chini ya miaka 18 ambapo, chini ya sheria ya mtoto watapelekwa kwenye mpango wa program ya marekebisho tabia kama wanavyopelekwa wengine wote na baada ya hapo watarejeshwa tena shuleni eneo lingine. Wito wangu ni jamii kukumbuka kuwa, sisi ni viongozi wenye dhamana na watoto wote hivyo, tunapochukua hatua ni kwa lengo la kufanya marekebisho ya tabia na kuwalinda wengine."
Waziri Gwajima ameongeza kuwa; "Naomba sasa hii taarifa nayo muisambaze vilevile. Aidha, wazazi tuendelee kukaa karibu na watoto Ili kuhakikisha wanakuwa na makuzi na malezi mema kipindi chote cha utoto wao. Ahsanteni sana kwa mjadala moto moto na Mungu awabariki."
Pia, Soma:
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema wanafunzi wa kike mkoani Tabora waliofukuzwa shule kwa makosa ya kujirekodi picha za utupu, watapelekwa kwenye programu ya marekebisho tabia kisha watarejeshwa katika shule nyingine. Waziri Gwajima amesema Serikali inapochukua hatua ni kwa lengo la kufanya marekebisho ya tabia na kuwalinda watoto.
Waziri Gwajima ameongeza kuwa; "Naomba sasa hii taarifa nayo muisambaze vilevile. Aidha, wazazi tuendelee kukaa karibu na watoto Ili kuhakikisha wanakuwa na makuzi na malezi mema kipindi chote cha utoto wao. Ahsanteni sana kwa mjadala moto moto na Mungu awabariki."
- Tabora: Wanafunzi wafukuzwa kwa kujirekodi picha za utupu na kuzisambaza
- Waziri Gwajima, wanafunzi kufukuzwa shule sababu ya picha za utupu siyo suluhisho na haiwasaidii, wanatakiwa kupewa mwongozo na kuelewa athari zake
- Tabora: Wanafunzi Tabora wakamatwa na simu zaidi 120 zilizoungwa makundi wanayotumia kutumiana picha/video za ngono