Fungu la mchicha limefikia ShT. 1000/=

Fungu la mchicha limefikia ShT. 1000/=

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,345
Ndio.
Hiyo ndio hali halisi, hii ndio bei mpya ya mchicha kutoka viunga vya pale O'bay, adjacent na kota za polisi Oysterbay.

Fungu hilo lilikuwa likiuzwa ShT. 500/= katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, hivyo bei mpya ni sawa na ongezeko la 100%, pamoja na kwamba pale ndio sehemu ya kwanza ya uzalishaji, yaani hakuna gharama za kusafirisha wala faida ya mchuuzi wa rejareja.

Tafakari,
CHUKUA HATUA!
 
Aisee. . .
Kweli tumekwisha. Sasa watu watakula nini chenye unafuu wa bei? Nashindwa kuamini hiyo ilikua bei ya kilo ya nyama miaka michache tu iliyopita.
 
Ndio.
Hiyo ndio hali halisi, hii ndio bei mpya ya mchicha kutoka viunga vya pale O'bay, adjacent na kota za polisi Oysterbay. Fungu hilo lilikuwa likiuzwa ShT. 500/= katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, hivyo bei mpya ni sawa na ongezeko la 100/=, pamoja na kwamba pale ndio sehemu ya kwanza ya uzalishaji, yaani hakuna gharama za kusafirisha wala faida ya mchuuzi wa rejareja.
Tafakari,
CHUKUA HATUA!

Ongezeko hilo ni 100/= au 100% ?
 
mchele umefikia 2600/= tusonge mbele!

Kwahiyo hapo mtu mwenye familia ya baba,mama na watoto wawili jumlisha na dada wa kazi siku akiamua kupika wali na mchicha tu pesa itakayowatoka sio chini ya 4000 (vitunguu+mafuta+ moto+ chumvi na maji) kwa mlo mmoja. Kweli maisha magumu.
 
Ndio.
Hiyo ndio hali halisi, hii ndio bei mpya ya mchicha kutoka viunga vya pale O'bay, adjacent na kota za polisi Oysterbay. Fungu hilo lilikuwa likiuzwa ShT. 500/= katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, hivyo bei mpya ni sawa na ongezeko la 100/=, pamoja na kwamba pale ndio sehemu ya kwanza ya uzalishaji, yaani hakuna gharama za kusafirisha wala faida ya mchuuzi wa rejareja.
Tafakari,
CHUKUA HATUA!

Well done kwa serikali legelege ilobaki sasa wajiandae kutengeneza noti ya elfu20 na elfu50 na hata laki ikiendelea kuwa mbaya
 
sasa wote tukikimbilia kijijini, mjini atabanana nani mpenzi?
Halafu huko kijijini mi sijazoea jembe meen?

Tunakoelekea hali ikiendelea kugangamala hivi utazoea tu bila hata mwenyewe kujua umezoea je?
 
Tunakoelekea hali ikiendelea kugangamala hivi utazoea tu bila hata mwenyewe kujua umezoea je?

sure,maana ucpoenda kwa mangi kwa siku 2,basi ujue unapotoka utoke na hela ya ziada,coz bei itaongezeka!
 
Sasa jaribu kupika wali na nyama loooooooo! Twafa.

Bora tungekufa, kuliko hii bakora waliyoamua kutuchapia nayo ni hatari tupu ama ni sawa na kutuchoma na msumari wa moto kwenye kidonda
 
Kazi nzuri kwa Jk na timu yakd cjui kampeni ya 2015 ccm mtakuwa na kauli mbiu gani maana zote mlizokuwa nazo zimekuwa vicd verser
 
Akufukuzaye mjini hakwambii toka! Kwa bei hizi mjini kutatushindi narudi 'Malinyi' kupanda mpunga na kuasha kibatari.
 
Usirudi kijijini,we songambele.ndio kauli mbiu.dola haipai utafika tu.
 
Back
Top Bottom