Fungu la mchicha limefikia ShT. 1000/=

tuache kulalamika, wenzetu huko japan wanaishi magorofani lakini kwa mboga za kutumia wanajitosheleza wenyewe. Wao wanapenda vitu fresh, so wamepanda mboga kwenye makopo, au kule juu kabisa wametengeneza concrete slabs ambazo zimewekwa udongo, sasa wa dar es salaama msiotaka kushika uchafu, hayo ndio matokeo yake.
 
Acha 2 mi nilinunua wiki iliyopita huku kwe2 moshi 800 sa kumbe wenze2 mmefika elfu,tunakoelekea .....
 
dagaa si misumari tena bali almasi.kwani haununuliki.hata ule wa mwanza nao umekuwa almasi kilo elfu nne.
 
tuache kulalamika, wenzetu huko japan wanaishi magorofani lakini kwa mboga za kutumia wanajitosheleza wenyewe. Wao wanapenda vitu fresh, so wamepanda mboga kwenye makopo, au kule juu kabisa wametengeneza concrete slabs ambazo zimewekwa udongo, sasa wa dar es salaama msiotaka kushika uchafu, hayo ndio matokeo yake.

Mchele, dagaa, nyama, sukari, maharage ,unga navyo kila mtu afanye namna ya kujipatia bila kununua?
 
Siku hizi WATAWALA wana lugha zao za kejeli na maudhi; utasikia mara 'TUKO KWENYE MCHAKATO...', 'SERIKALI IMEJIPANGA....', 'WANANCHI WA KAWAIDA....' n.k. .

Hebu fikiria lita moja ya mafuta ya taa ni zaidi ya sh. 2,000 gunia la mkaa sh. 35,000, maharage kilo moja sh. 2,500, mtungi wa gesi ya kupikia kilo 15 sh. 55,000; kwa gharama hizi kweli tutafika?

Nafikiri umefika wakati wa kuiga yanayofanywa na wenzetu kama Nigeria, Syria na kwingineko pamoja vinginevyo Watanzania tumekwisha....
 
Mchele, dagaa, nyama, sukari, maharage ,unga navyo kila mtu afanye namna ya kujipatia bila kununua?

ofcourse siyo kila kitu utaweza kujitosheleza, lakini kwa vile ambavyo una uwezo wa kuzalisha mwenyewe kwanini usifanye mwenyewe ukapunguza japo kidogo bajeti yako?
 
ofcourse siyo kila kitu utaweza kujitosheleza, lakini kwa vile ambavyo una uwezo wa kuzalisha mwenyewe kwanini usifanye mwenyewe ukapunguza japo kidogo bajeti yako?
Binafsi napenda sana wazo la kujiwezesha na ndivyo tulivyokua tunafanya kule kwetu Moshi, mtu ananunua mafuta tu na chumvi tu wakati mwingine. Ila Dar, sehemu ambayo wengi wanaishi kwenye nyumba za kupanga ambazo hazina hata sehemu ya kuotesha maua kujiwezesha huko hakuwezekani.
 
tuache kulalamika, wenzetu huko japan wanaishi magorofani lakini kwa mboga za kutumia wanajitosheleza wenyewe. Wao wanapenda vitu fresh, so wamepanda mboga kwenye makopo, au kule juu kabisa wametengeneza concrete slabs ambazo zimewekwa udongo, sasa wa dar es salaama msiotaka kushika uchafu, hayo ndio matokeo yake.

Wako wengi wanaotaka kufanya hivyo na wana maeneo ya kutosha kabisa lakini maji ya kumwagilia watapata wapi ilhal hata yale ya kutumia tu kwa shughuli za lazima majumbani yanapatikana kwa mbinde.
 
Labda ni ahueni ya mkulima iwapo kamsimamia kooni mchuuzi! Washika jembe nao wanakazi jamani!
 
uzalishaji wa mjini sio mkubwa sana lakini unasaidi matumiz ya hapa na pale. Pili lazima tukubali maeneo ya kilimo kidogo kidogo yapo mengi tu ila watu hawajatia akilini kwamba yawezekana kufanya hivyo.

Msukumo wa kuzalisha mwenyewe lendo sio kujitosheleza tu, ni kuweza kupata chakula fresh unachojua kimekuajekuaje, pili hewa safi, tatu ni kijishughuli tu cha kukufanya uwe buzi. Yawezekana kabisa kajisehemu hako huwezi kuzalisha vyote unavyohitaji, lakini unaweza kuzalisha japo asilimia tano!

Maji ya kumwagilia sio mengi sana. Ila maeneo mengine ya mjini kwenye baadhi ya majengo ni marufuku kulima ama kufuga!
 
Tanzania has surely,irreversibly gone to the dogs. There is something terribly wrong with our production and distribution system if a fungu of mchicha costs tsh 1000.
 
Ndugu,

Nakumbuka katika kipingi cha awamu ya tatu (Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe) fungu la mchicha hapa kwetu Ubungo (Riverside) lilikuwa linauzwa sh. 150/= na sukali kipindi hicho ilikuwa 600/= leo hii vitu hivyo havishikiki! Mchicha ni sh. 500/= na sukali kilo moja ni sh. 2400/=

Ongezeko hili haliendani kabisa na ongezeko la vipato kwa watanzania, mishahara iko pale pale lakini hata kama ikipaga haiwezi kuongeza tija kwasababu kuna ongezeko kumbwa la bidhaa. Serikali inabidi isimamie haraka mfumuko wa bei vinginevyo fungu la mchicha litauzwa sh. 10,000/= wakati huo huo serikali italaimika kutengeneza noti ya 100,000/=
 
Back
Top Bottom