Funga mwaka 2012: Nape amwita Jeetu Patel "Baba"

Funga mwaka 2012: Nape amwita Jeetu Patel "Baba"

Amiliki

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Posts
2,085
Reaction score
1,005
Kweli Waliosema Njaa Mwanaharamu, hawakukosea. Si huyu huyu Nape aliyejigeuza vuvuzela na kupita kila kona na kuwatuhumu wale wote waliohusika na wizi wa EPA na kuwaita Majina! Si huyu huyu Nape aliyetaka Mafisadi wote waondoke ndani ya CCM na kuwaita ni Magamba na wanakichafua Chama!

Si huyu huyu Nape aliyekuja na Siku 90 za kukisafisha Chama kwa kuwaondoa Mafisadi ambao wengine walibatizwa jina la "Mapacha Watatu"
Si huyu huyu Nape aliyepinga kwa nguvu zote Ufisadi uliopelekea Jengo la Umoja wa Vijana wa Magamba kukodishiwa Mtu kwa Bei ya Kutupa hata ikampelekea kukorofishana na Lowasa na hatimaye, Pamoja na Wenzake kuanzisha kwa Siri Chama cha Siasa cha CCJ!

Inamaana Leo hii Nape amesahau kwamba Jeetu Patel ni Miongoni mwa Mafisadi wakubwa ambao ndio waliopelekea hata yeye kutaka wale walioshirikishwa naye kwenye Wizi wa pesa za EPA wafukuzwe chamani!

Kinasaba, tunajua kabisa kwamba Nape hana Undugu wowote, au wa damu au wa kurithishwa na Jeetu Patel. Leo hii iweje Nape aibuke na kumwita Mtu aliyetupa mateso Watanzania "Baba"!

Ama kweli Penye udhia, Penyeza Rupia. Baada ya kulishwa vipande thelasini leo hii Nape Unakuwa Mtetezi mpaka wa Mafisadi na kutusaliti nduguzo kweli!

Nape amenikatisha tamaa zaidi ya alivyonikatisha toka mapema. Sintoshangaa siku nikimsikia Nape akimwita Rostam, Mjomba'ke, na Lowasa na Chenge Baba walezi.

Wonders shall never end.


 
Wewe umechelewa kumfahamu NAPE.

Ni mtu wa akili za wastani, au chini ya wastani. JK alihitaji mtu ambaye akitumwa anasema YES kila wakati.

Huyu bwana mdogo hajielewi na hajui siasa ni nini, anajiegemeza upande wa JK ambao una umebakiza miaka miwili tu madarakani.

Kweli haoni mbali. Njaa itamfanya atampigia magoti EL nyie ngojeni tu
 
Kamuita wapi jamani? Hebu dadavua, walikuwa dinner ama? Mnanichelewesha kucheka. Mwanume mzima unamuita mume wa mwanamke mwingine baba! That is insulting!
 
Amiliki umetueleza ila hujasema siku ya kuitana baba na mwana ilikuwa lini na wapi! Mbona umekuwa na haraka kiongozi? BTW Nape kisiasa bado kabisa! Iko siku atamuita Dr. Slaa anko...akishakuwa rais! Mark my word!
 
Last edited by a moderator:
unaona kumuita mwaka jana ni sahihi? Hahaha, kama ni mume wangu huyu nape, ningemuacha bila kesi!
Haya elezea mazingira basi, alimuita wapi na ilikuwa kuwaje?

Kumbe wewe ni she?
 
unaona kumuita mwaka jana ni sahihi? Hahaha, kama ni mume wangu huyu nape, ningemuacha bila kesi!
Haya elezea mazingira basi, alimuita wapi na ilikuwa kuwaje?
Kwa Nape na uelewa wake ni sahihi.Lakini,kwa GTs si sahihi.Si sahihi kwa sababu kubwa moja: Jeetu si mtu safi kwa watanzania karibu wote.Mkuu King'asti,Nape alikuwa akielezea anaouita unafiki wa Wakili Msomi Mabere Nyaucho Marando ya kwamba yeye(Marando) huwaponda mafisadi kwenye majukwaa ya siasa lakini huwawakilisha na kuwatetea Mahakamani. Bandiko hili kwakuwa lilijaa pumba lilimfanya Nape apigwe Ban kama @Nnauye Jr kabla hajaibuka tena kwa ID ya Nape Nnauye
 
Last edited by a moderator:
Mwalimu wako wa mwandiko alikufa ukiwa hujajua kuandika vizuri nini
 
mkuu tunashukuru kwa post yako hebu weka ushabiki pembeni kua kama thinker kwa kuweka bayana tukio hilo lilitokea lini na wapi na ktk mazingira yepi ili watu wajue zaidi otherwise post yako itakosa ladha tarajiwa!!
 
Amiliki

Wewe unamatatizo kwa sababu kama unadhani mtu mzima mwanaume ambaye kashafikia umri wa uzee akiwa fisadi sasa ataitwa dada au kaka kwa kuwa ni fisadi hiyo ni akili iliyoshindwa kupambanua mambo.

Kama mtu ni baba ataendelea kuitwa baba na kama ni mama ataendelea kuitwa mama hata kama atakuwa fisadi. Balafu baada ya hapo kama ni kushughulikiwa atashughulikiwa kama wahalifu wengine.hata kama mtu ni babu kwa mfano! Kumpenda kwako saaana hakuwezi kumfanya akaitwa mzee kijana.
 
Last edited by a moderator:
Wewe umechelewa kumfahamu NAPE.
Ni mtu wa akili za wastani, au chini ya wastani. JK alihitaji mtu ambaye akitumwa anasema YES kila wakati.
Huyu bwana mdogo hajielewi na hajui siasa ni nini, anajiegemeza upande wa JK ambao una umebakiza miaka miwili tu madarakani.
Kweli haoni mbali. Njaa itamfanya atampigia magoti EL nyie ngojeni tu
hii hoja yako imeniacha hoi!
kuna mtu mmoja anasema kuwa jk aliposikia naibu waziri wake wa elimu Mh. Amin Agustino akisema kuwa Tanganyika iliungana na Zimbabwe alicheka sana, ndio nikagundua kuwa yeye anatafuta dizaini za watu ambao umma ukimponda atawajibu "si mumewaona wasaidizi wangu" ili ionekane ndio wahaharibu
 
Niliiona iyo post, I was shocked! Niliisoma juujuu baada ya kuona imeandikwa na mpuuzi in the model of Nape lakini nakumbuka alikuwa anawatetea "mafisadi" na kumsema Marando kuwa ni wakili wa Jeetu but akiwa public anapinga ufisadi. Hivyo Jeetu alimpiga mkwara Marando kuwa kama anataka kuendelea kuwa wakili wake basi aache kumsema kwenye media. Akasema Mabere ali-apologize. Pia Nape akadai kuwa ana izo communication exchanges, kama vipi atazitoa. Na hapo ndipo kijana Nape alipotamka kwa unyekekevu mkubwa (pengine huku akiwa ameweka mikono nyuma kwenye masaburi yake) ---- Jeetu Patel, baba yangu....!! Pumbavu kabisa huyu kijana. Mr. President, ondoa impurities hizo, zitawa-cost! Ukisoma post zake zimejaa umbeya na mipasho ya uswazi. Unproffessional! Hovyo!
--HOPE SIJA-BREAK HOUSE RULES. No Ban please.
 
Napata taabu kidogo kuelewa hili andiko...kamwita wapi?...kulikuwa na nini??...bado halijatushibisha kulielewa...hata hivyo kwa desturi zetu kuna mazingira ambayo unaweza kumwita mtu aliyekuzidi umri..au labda umri unalingana na baba yako au mama yako kumwita majina hayo baba, mama, babu nk ...hivyo si jambo la ajabu sana ni heshima tu kwa mtu aliyekuzidi umri.....
 
hebu mtoa mada iweke vizuri, wapi alimwta jeet p baba wa nape? Ni vizuri 2tajua chanzo chake.
 
Back
Top Bottom