Funga mwaka 2012: Nape amwita Jeetu Patel "Baba"

Funga mwaka 2012: Nape amwita Jeetu Patel "Baba"

mkuu tunashukuru kwa post yako hebu weka ushabiki pembeni kua kama thinker kwa kuweka bayana tukio hilo lilitokea lini na wapi na ktk mazingira yepi ili watu wajue zaidi otherwise post yako itakosa ladha tarajiwa!!
Kwa Nape na uelewa wake ni sahihi.Lakini,kwa GTs si sahihi.Si sahihi kwa sababu kubwa moja: Jeetu si mtu safi kwa watanzania karibu wote.Mkuu,Nape alikuwa akielezea anaouita unafiki wa Wakili Msomi Mabere Nyaucho Marando ya kwamba yeye(Marando) huwaponda mafisadi kwenye majukwaa ya siasa lakini huwawakilisha na kuwatetea Mahakamani. Bandiko hili kwakuwa lilijaa pumba lilimfanya Nape apigwe Ban kama @Nnauye Jr kabla hajaibuka tena kwa ID ya Nape Nnauye
 
hebu mtoa mada iweke vizuri, wapi alimwta jeet p baba wa nape? Ni vizuri 2tajua chanzo chake.
Kwa Nape na uelewa wake ni sahihi.Lakini,kwa GTs si sahihi.Si sahihi kwa sababu kubwa moja: Jeetu si mtu safi kwa watanzania karibu wote.Mkuu,Nape alikuwa akielezea anaouita unafiki wa Wakili Msomi Mabere Nyaucho Marando ya kwamba yeye(Marando) huwaponda mafisadi kwenye majukwaa ya siasa lakini huwawakilisha na kuwatetea Mahakamani. Bandiko hili kwakuwa lilijaa pumba lilimfanya Nape apigwe Ban kama @Nnauye Jr kabla hajaibuka tena kwa ID ya Nape Nnauye
 
Napata taabu kidogo kuelewa hili andiko...kamwita wapi?...kulikuwa na nini??...bado halijatushibisha kulielewa...hata hivyo kwa desturi zetu kuna mazingira ambayo unaweza kumwita mtu aliyekuzidi umri..au labda umri unalingana na baba yako au mama yako kumwita majina hayo baba, mama, babu nk ...hivyo si jambo la ajabu sana ni heshima tu kwa mtu aliyekuzidi umri.....
Kwa Nape na uelewa wake ni sahihi.Lakini,kwa GTs si sahihi.Si sahihi kwa sababu kubwa moja: Jeetu si mtu safi kwa watanzania karibu wote.Mkuu,Nape alikuwa akielezea anaouita unafiki wa Wakili Msomi Mabere Nyaucho Marando ya kwamba yeye(Marando) huwaponda mafisadi kwenye majukwaa ya siasa lakini huwawakilisha na kuwatetea Mahakamani. Bandiko hili kwakuwa lilijaa pumba lilimfanya Nape apigwe Ban kama @Nnauye Jr kabla hajaibuka tena kwa ID ya Nape Nnauye
 
Kweli Waliosema Njaa Mwanaharamu, hawakukosea. Si huyu huyu Nape aliyejigeuza vuvuzela na kupita kila kona na kuwatuhumu wale wote waliohusika na wizi wa EPA na kuwaita Majina! Si huyu huyu Nape aliyetaka Mafisadi wote waondoke ndani ya CCM na kuwaita ni Magamba na wanakichafua Chama!

Si huyu huyu Nape aliyekuja na Siku 90 za kukisafisha Chama kwa kuwaondoa Mafisadi ambao wengine walibatizwa jina la "Mapacha Watatu"
Si huyu huyu Nape aliyepinga kwa nguvu zote Ufisadi uliopelekea Jengo la Umoja wa Vijana wa Magamba kukodishiwa Mtu kwa Bei ya Ku[SI

CHEZEA PEJA VEVE!
 
Ni kupoteza muda kumjadili "Half-minded Person"....
 
Kwa faida ya wale wasioliona lile bandiko la Nape alipokuwa anamponda Wakili Mabere Marando na kudai kwamba anawapinga mafisadi jukwaani huku akiwatetea mahakamani, ndipo Nape alipokwenda mbele zaidi na kuandika "Baba Jeetu Patel, alitaka kuiondoa kesi kwa Marando" huku akidai kuwa na mawasiliano ya Marando na "Baba" Jeetu Patel.Kitu ambacho I am sure 2 years back asingethubutu kukitamka! Shame on his njaa! Shame on his Unafiki!!
 
New political terminologies for strengthening the unity and remove all loopholes among ccm members.
 
Usicheze na fweza mjomba nape kalegea mbele ya Epa fraud......!!!!! Ccm bwana kwisha kbs
 
Yaani wewe sijui ni teja, ndio umeandika nini sasa hapo. Mbona unalalamika na hueleweki? Za kujificha hizo ndio madhara yake uache
 
Kuhusu "Mapacha watatu", nakumbuka Waziri mstaafu Mhe. Sumaye alihoji siku moja kuwa kuna watu wametumia pesa za chama (yaani akina Naape na MMkama) wakizunguka kila mkoa huku wakitaja majina ya mapacha hao bila aibu kwamba chama kimewapa siku 90 wajiondoe wenyewe kabla ya kulazimishwa na vikao vya juu kwa lazima. Mhe. Sumaye alisema ikigundulika hizo tuhuma ni za uongo watu hao watachukulkiwa hatua gani? Hata hivyo hii ni CCM, mwisho wa siku lao ni moja.
 
Kweli Waliosema Njaa Mwanaharamu, hawakukosea. Si huyu huyu Nape aliyejigeuza vuvuzela na kupita kila kona na kuwatuhumu wale wote waliohusika na wizi wa EPA na kuwaita Majina! Si huyu huyu Nape aliyetaka Mafisadi wote waondoke ndani ya CCM na kuwaita ni Magamba na wanakichafua Chama!

Si huyu huyu Nape aliyekuja na Siku 90 za kukisafisha Chama kwa kuwaondoa Mafisadi ambao wengine walibatizwa jina la "Mapacha Watatu"
Si huyu huyu Nape aliyepinga kwa nguvu zote Ufisadi uliopelekea Jengo la Umoja wa Vijana wa Magamba kukodishiwa Mtu kwa Bei ya Kutupa hata ikampelekea kukorofishana na Lowasa na hatimaye, Pamoja na Wenzake kuanzisha kwa Siri Chama cha Siasa cha CCJ!

Inamaana Leo hii Nape amesahau kwamba Jeetu Patel ni Miongoni mwa Mafisadi wakubwa ambao ndio waliopelekea hata yeye kutaka wale walioshirikishwa naye kwenye Wizi wa pesa za EPA wafukuzwe chamani!

Kinasaba, tunajua kabisa kwamba Nape hana Undugu wowote, au wa damu au wa kurithishwa na Jeetu Patel. Leo hii iweje Nape aibuke na kumwita Mtu aliyetupa mateso Watanzania "Baba"!

Ama kweli Penye udhia, Penyeza Rupia. Baada ya kulishwa vipande thelasini leo hii Nape Unakuwa Mtetezi mpaka wa Mafisadi na kutusaliti nduguzo kweli!

Nape amenikatisha tamaa zaidi ya alivyonikatisha toka mapema. Sintoshangaa siku nikimsikia Nape akimwita Rostam, Mjomba'ke, na Lowasa na Chenge Baba walezi.

Wonders shall never end.

Nape anawatesa sana nyie wajumbe wa mikutano ya hadhara ya chadema,sasa anakukera nape kumwita jitu baba kuliko mwanasheria wa chadema anaemramba miguu na kumtetea jitu mahakani ili asifungwe kwa wizi wa hela za EPA?!!Toa kwanza mwiba ulio takoni ili uweze kukaa chini na kuutoa mwiba ulio mguuni kirahisi,busara ya kawaida kabisa inasema hivyo,other na wewe utaonekana ni wa akili za wastani ama chini ya hapo,nyambaff!
 
Wana bahati wanawatawala na kuwaongoza watu wenye hofu ya Mungu!! Kujikomba ni sera ya CCM kuelekea 2015. Mengi tutayashuhudia tusubiri wakati uamue. Nape atakuwa wa kwanza kupanda jukwaani na kumpigia debe EL au mteule wa EL kwenye urais 2015.
 
Kwa Nape na uelewa wake ni sahihi.Lakini,kwa GTs si sahihi.Si sahihi kwa sababu kubwa moja: Jeetu si mtu safi kwa watanzania karibu wote.Mkuu,Nape alikuwa akielezea anaouita unafiki wa Wakili Msomi Mabere Nyaucho Marando ya kwamba yeye(Marando) huwaponda mafisadi kwenye majukwaa ya siasa lakini huwawakilisha na kuwatetea Mahakamani. Bandiko hili kwakuwa lilijaa pumba lilimfanya Nape apigwe Ban kama @Nnauye Jr kabla hajaibuka tena kwa ID ya Nape Nnauye
Sawa mheshimiwa.....lakini bado tunajadili kitu ambacho hatujajua bado kilitokea wapi??......lini?? na kulikuwa na nini??
 
Back
Top Bottom