Kuna jamaa yangu alikuwa kwenye ujenzi wa nyumba wake,jamaa kauzu sana mtu wa kufuatilia kila sent yake imetumikaje. Sasa akamwambia fundi amwandikie na kumpigia hesabu idadi za materials kama mbao na bati fundi alipomaliza jamaa akashika karatasi akamwambia fundi twende kununua vifaa. Fundi akamshawishi ili kuokoa gharama issue ya mabati waende Kiwandani kabisa. Jamaa akapokea wazo wakaenda Kiwanda kimoja kipo Nyerere Road,jamaa akatoa oda pale na kulipa kila kitu then wakapewa mzigo wakaondoka nao.
Sasa baadae fundi akafanya kazi yake akamaliza,sasa ikaja kuonekana kuwa kuna mabati yamepungua na jamaa akawa wakati ule hana hela,akaanza kujiuliza imekuwaje bati zipungue na hesabu ilikuwa sawa. Wakati huo fundi yupo mkoani kwenye kazi nyingine,jamaa ikabidi aende pale kiwandani kuulizia kulikoni,jamaa ndio wakamsanua kuwa fundi kakupiga,jamaa kupiga hesabu vizuri fundi alimpiga kama 2ml. Jamaa akachoka na hasira juu,kumbe pale kiwandani yule fundi anafahamika sana na anawapelekea wateja wengi sana,kwa hiyo ana signals zake anazowapa wale wafanyakazi.
Sent using
Jamii Forums mobile app