Fundi hata umbane vipi akitaka kukuibia atakuibia tuu

Hawa tena ndio wanakufumua kishenzi maana wako kibiashara zaidi
Me mwenyewe nimemshangaa .et anaona kutumia kampuni ndo njia salama ...wakat wale kwenye quotation wataongeza margin kwenye kila material...na km sio mfuatiliaji unakuta ushapigwa
 
Utaibiwa tu hata ufanyeje.

Nina WORKSHOP ya fabrication ya vyuma na Welding in general

Sasa wale madogo wako pale mbinu zao zote za upigaji nimeshazijua, mfano mteja anataka atengenezewe kitu, atatengenezewa QUOTATION ya vyuma vizito kwa thickness za milimita, lakini linapokuja suala la kufabricate unatengenezewa chuma chepesi, kama ilitakiwa itumike Round pipe ya mm2 inchi moja na nusu inayouzwa elf 55, utatengenezewa ya mm1 inayouzwa elfu 35, hiyo 20 ya kila pipe kama ziko kumi 200,000 ishaibwa.

Kama mteja ni king'ang'anizi wa kuongozana Hardware anapigwa kwa MEASURING TAPE, yaani hapa material yanazidishwa kwenye QUOTATION, idadi iliyozidi inarudishwa hardware kwa bei pungufu, ukileta mtu wa kusimamia Chuma zinakatwakatwa zitauzwa kama offcuts. ukitaka ufanyiwe kazi site kwako bei inaongezeka.

Sasa kuna soo walilifanya mpaka jamaa (Mteja) akakoma, jamaa alikuwa anakuja anawachukua WORKSHOP wakapime kazi, alafu kazi anapewa fundi mwingine sababu ya bei ya hao madogo, jamaa alirudi kwa staili ile kama mara tatu, kila wakipima kazi,kazi anapewa fundi mwingine. Siku akaja akawachukua hadi site alikuwa anajenga guest, madogo wakapima grills(madirisha) wakaandika vipimo vyao in vice-versa kwa makusudi kabisa, urefu ukawa ndo upana na upana ukawa ndo urefu,wakampa vipimo, akasema atakuja kuwachukua workshop wakafanye ile kazi kumbe anaenda kumpa fundi wake vile vipimo achome zile grills. fundi wake akachoma zile dirisha kwa vipimo alivyopewa. kwenda kuzifitisha ikawa kizazaa, dirisha hazifiti, jamaa alikoma kwa ujuaji wake.

NB:Kumtoa fundi ofisini kuna bei yake



Sent using Jamii Forums mobile app
Duh huyo boss aliwezwa kwel ... yan kadri unavo m'bana fundi ndo anazidi kuongeza mbinu za kukuibia
 
Unaweza kumbana na asiibe,Mimi nilikuwa na Jenga,mafundi hasahasa huiba cement,Mimi nilinunua idadi ya cement aliyosema Kisha Ile mifuko ya cement niliiwekea alama ndogo Sana ya sili,ni ndogo Sana na nikimuomba fundi anihifadhie mifuko yote atakayo itumia,Nina kazi nayo muhimu,nikiporudi nilikuta Kati ya mifuko mitupu aliyoniwekea mitatu haikuwa yangu,means alichukua mifuko mitupu mingine akaniwekea akasepa na na cement mifuko 3 nilimuomba tu fundi naomba cement yangu,na kweli alirudisha

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Mkuu huwez kum'bana kwa 100% ...Fundi ni fundi tuu
Asipokuibia hela ,atakuibia material,asikuibia material atakuibia muda wako....na hapo uliibiwa muda wako
 
Hata hawa wa makampuni ni wezi tu kiufupi hamnaga fundi asiekua mwizi muache unoko matajiri
Makampuni nayo yanapiga mnoo ....unaweza kuta sehemu ya kutumia mbao 30 wakasema 50 ...ukiwabana wanasingizia kwamba kuna emergency
 
Bado Niko puzzled! Kwamba ni sifa na fahari kuiba?!?

Wakandarasi wazawa wakinyimwa contracts tunakasirika!!
Ndo maana makampuni ya nje yanazidi kupiga hatua na kuchukua tender kila siku .... yan ma contractor wengi wa kibongo wanaiba na bado kazi inakua chini ya kiwango
 
Lakini huu ni uhuni, mafundi waache hizi za upigaji wa kijinga, yeye anapotaka kupiga pesa ya bosi wake hajui kamba mwenzake ame-hustle kiasi gani kuipata hiyo pesa.

Halafu hiyo kazi unayofanya unalipwa wizi wa nini tena. Ndo maana mafundi njaa njaa hawa hawana maisha ya maana japo wanafanya kazi za pesa nyingi.
Mkuu Fundi ..atabaki kuwa fundi .jenga naye urafiki upunguze chance za kupigwa
 
Ndo maana makampuni ya nje yanazidi kupiga hatua na kuchukua tender kila siku .... yan ma contractor wengi wa kibongo wanaiba na bado kazi inakua chini ya kiwango
Siyo kwamba makampuni ya nje hazidishi wala kupiga hela,, hakuna kampuni ambayo haitaki faida kubwa tena ndiyo wanapiga pesa balaa, mnaweza gawana nusu kwa nusu pesa ya ujenzi wa nyumba yako,, mbona kwenye makampuni mpaka vitu vinabaki vingi sana kuliko mtu binafsi
 
Habarini wakuu,

Fundi yeyote ana taaluma ambayo wewe huna jifunze namna ya kuishi na fundi kupunguza chances za kukuibia

Fundi yeyote yule unapo mpa kazi mpe uhuru wa kuifanya ile kazi cha muhimu ni kuzingatia ubora wa kazi yako
Fundi asipokuibia hela ,atakuibia materials, asipo kuibia materials atakuibia Muda wako

Huwa naona watu wengi sana wanapoteza muda kufuatana na mafundi especially hawa wa buildings works km carpenter, painter,plumber, electrical & air condition technicians ...n.k
Lakini pamoja na kuwafuatilia hatua kwa hatua bado wanaendelea kuibiwa pasipo kujua ..kwakua lazima tukubali kuwa fundi yeyote amekuzid knowledge ya hiyo taaluma yake ..hvyo bhac ,iwe Kampuni ,Taasisi au Mtu binafsi ..unapokua na kazi yako ..focus zaidi kwenye ubora wa kazi na sio fundi um'bane vipi ili asikuibie

Nimeona mifano mingi sana ya watu wanaolalamika kila siku kuibiwa na mafundi lakini ukifuatilia kwa makini ni watu wanao wabana sana mafundi wakat wa kazi zao lakini ukweli ni kwamba kadri unavozidi kumbana fundi ndo unamuongezea nafasi ya kukuibia

Kwa upande wa hela fundi kukuibia anaweza akataja bei tofaut na bei elekezi..au kazi ambayo angeweza kuifanya kwa lisaa limoja anaweza akaifanya kwa masaa matano ili uone ni kazi complicated umpe hela nyingi

Kwa upande wa materials hapa ndo wanatupigaga sana hususani hv vitu vya spare iwe vyombo vya usafiri, vifaa vya umeme,bomba ,Ac nk hapa hata uwe unajua bei ya kila kitu anaweza akakudanganya kitu flani kimeharibika ni cha kubadilisha kwakua hujui chochote ukimpa hela tayari anakua ameshakupiga hata ukitaka recept za EFD zinanunuliwa..so sio big deals..

Kwa upande wa muda hapa mara nyingi n kwa mafundi walio ajiriwa kwenye makampuni au taasisi ambazo nature ya kazi zao ni za ku move kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine hapo watakua wanatumia muda wa ofisi kufanya kazi zao binafsi

Hebu kila mmoja aelezee mbinu anazozijua ambazo mafundi wanatumia kutuibia kila siku ili angalau tujifunze
Africa ina laana. Watu ni kuibiana tu. Lazima umbane kisomi. Ama sivyo utafanyiwa kazi mbaya. Suluhisho ni kusimamia ujenzi mwenyewe mchana na usiku. Au tafuta mtu mwaminifu asimamie hasa kuhakiki kazi ni imara, ratio za siment ni sawa. Unene wa nondo ni sawa. Pima maji, kobiro, na skwea zipo. Nk.
 
Hizi changamoto za kusumbuana na mafundi mnazitaka wenyewe client, Siku hizi kuna makampuni mengi tu class VII wanajenga hadi nyumba za viwili, kaa nao chini mpatane muingie mkataba, mkiendelea kujenga ki local hvo mtapigwa sana na nasema mtaendelea kupigwa tu!
Hakuna asiyetaka haya elewa siyo kila mtu ana uwezo wa kuanza project mpaka ikakamilika bila kukwama.

Wabongo wengi jenzi zetu ni za mafungu mafungu unakuta leo msingi kupanga tofali kesho lintel kesho kutwa alimradi nyumba ikamilike.
 
Hakuna asiyetaka haya elewa siyo kila mtu ana uwezo wa kuanza project mpaka ikakamilika bila kukwama.

Wabongo wengi jenzi zetu ni za mafungu mafungu unakuta leo msingi kupanga tofali kesho lintel kesho kutwa alimradi nyumba ikamilike.
Hata kampuni zinafanya hvo pia, wanajenga kwa phase kulingana n uwezo wako,
 
Hi ndo mbinu ya kupunguza chance za kuibiwa japo sio kwa 100%
Sawa, usimchukulie kama fundi mchukulie kama mtu wako wa karibu mwenye thamani kubwa kwako akigundua umemthamini ataamini hata akiwa na shida mbali na ufundi wake utaweza kumsaidia kwahiyo atajistukia atakuwa muaminifu kwavile unapiga naye story, unakula naye, na unakunywa naye.
 
Sisi wa umeme ni wastaarabu sana, hasa ukipata mwenyewe yule wa taaluma atakufanyia kazi kwa ueledi kwa kuzingatia viwango vyote na ubora. Wizi unatokea pale mnapoongea kazi mdomoni, kama unahitaji kufanyiwa kitu tumiwa quotation, kaa nayo na kuijadili kwa umakini mkubwa.
Kama kutakuwepo na gharama ambazo huelewi uliza ili upewe maelezo toshelezi. Kazi nyingi ninazofanya natumia muundo huo au namwambia mteja wangu anunue materials Mimi atanipa hela ya ufundi, na materials yanayotoka na yanayobaki ni ya kwake labda amue mwenyewe kunipa. Tumieni mafundi waaminifu na siyo vishoka
 
Back
Top Bottom