Fumbo la uumbaji, roho na mwili uozao

Fumbo la uumbaji, roho na mwili uozao

Lakini kwenye vitabu vitakatifu (nimewahi soma kwenye biblia) kwamba wakati wa uumbaji Mwenyezi Mungu alikuwa akiumba viumbe wengine (including wanyama kama sokwe) kwa kunena tu na wakawepo. Lakini wakati wa kumwuumba mwanadamu alitumia mikono yake na udongo kisha akampulizia pumzi ya uhai ambayo in essence ndiyo roho. Sasa inakuwaje na wanyama ambao hawakupuliziwa pumzi ya uhai (roho) nao wawe na roho? Na je kama nao wana roho wanapokufa na miili yao kuoza, roho (energy) zao nazo ubaki na kutafuta jumba jingine?
Mikono ya Mwenyezi MUNGU yaweza kuwa ni maneno yake. Kumbuka maneno yake yanasema Mwenyezi MUNGU anapotaka jambo hukiambia kuwa na mara huwa! Hivyo maneno yake ni kama mikono kibinaadamu. Hata alivyosema na tumuumbe mtu kwa mfano wetu, haimaanishi ana sura na umbo kama la mtu bali hiyo inamaana kubwa tofauti na hiyo ya kiuandishi. Naomba kuwasilisha.
 
Ukiitunza roho itauongoza Mwili na usipoitunza roho, mwili utajiongoza wenyewe. Kumbuka roho inajua yale ambayo mwili hauyajui, hivyo, kutoongozwa na roho mwili upo kwenye risk kila wakati. Chakula cha roho ni neno, chakula cha mwili sote twakijua. Nimejaribu kadadavua fikra zangu kidogo, nipo tayari kukosolewa ila tukumbuke Quran inasema "Wanauliza habari za roho? Waambie, Ninyi hamkufunuliwa elimu hiyo isipokuwa kidogo"
Kwa hiyo sote hapa tunatapatapa tu maana hata Mwenyezi MUNGU aliyetuumba anasema wazi kuwa hakuifunua elimu juu ya roho isipokuwa kidoogo. Ngoja tuendelee kutapatapa
Na hiyo roho tunaitunza kwa kutumia nini au ndiyo hilo neno? Na hilo neno ndiyo nini? Hii mada naipenda.
 
Tatizo hapa kuna vitu viwili vinaleta shida ...
Roho = software,
Mwili = Hardware
Mwili + Roho = Computer

Shida inakuja pale roho inapouona mwili (housing) umechoka na tayari wenyewe (moyo) umeishakuwakwa upgraded, hapo ndo moyo unapoenda kwa mwili mwingine
Ndio maana tunaambiwa tutunze roho zetu maana zisijejikuta zinaingia kwenye mwili wa kuku! Just joking, haya mambo yananizidi upeo. Mfano wa software na hardware umekaa poa sana kwa wale wagumu kuelewa.
 
Mkuu kumbuka moyo ni kitu tofauti na roho. Moyo nao ni moja ya vitu vinavyooza kama sehemu ya mwili (jumba). Moyo uoza kama ilivyo kwa utumbo na figo wakati roho anapomkacha best yake mwili na kuondoka kwa mwendo mdogo mdogo.
Neno roho na moyo hutumika interchangebly na lengo huwa ni kumaanisha Roho. Kuna wajuvi wanasema roho ipo ndani ya moyo.
 
Sio kosa lako kwa hiki ulichoandika ila kwa manufaa yako na ya wengine pia ni kwamba kwenye muunganiko wa kutengeneza nafsi roho haiweZi kujitegemea hilo ndio lilikuwa jibu langu la kwanza kisha jamaa akaja na reply ambayo ndio ilizaa jibu langu la pili kuwa kwenye ishu ya utengano roho huwa huwa ni kitu chenye mwendelezo ikiwa huru...haya mambo hayana jibu moja linalojitegemea kwakuwa kila aina ya swali huzaa jibu tofauti kwa muktadha wa maudhui yake.... hii elimu ya roho iko deep na vast kiasi kwamba usipokuwa makini na ukawa na rigid mind kama yako ni rahisi kutoa conclusion kama hii uliyotoa wewe....jisikie kuniuliza chochote nitakujibu kwa upole
791cb4f045cb80bc7ed7c4cf59a918cc.jpg
Nimeipenda zaidi picha hiyo na ujumbe wake. Ukikutana na mtu aliyosoma kitabu kimoja tu tena cha dini yake tu! Hawa watu huo ni shiida na ni hatari sana kwa ustawi wa sayari dunia, hawana maarifa kabisa ni wepesi wa hasira na kupinga vitu bila kufikiri nje ya box
 
Kama umechoka kwa kukosolewa kidogo kama hivyo basi inadhihirisha jinsi ulivo mkavu sana kichwani.
Siwezi kuleta hoja kwa kitu kisichohitaji hoja.Tafuta thread zangu uone naandika nini humu kisha jipime.
Karibu sana katika ulimwengu huru.
....Free ideas.....
Tupe link mkuu. Critisize in positive way, sote tunajifunza hapa sio unaleta majigambo as if wewe wajua kila kitu
 
Mikono ya Mwenyezi MUNGU yaweza kuwa ni maneno yake. Kumbuka maneno yake yanasema Mwenyezi MUNGU anapotaka jambo hukiambia kuwa na mara huwa! Hivyo maneno yake ni kama mikono kibinaadamu. Hata alivyosema na tumuumbe mtu kwa mfano wetu, haimaanishi ana sura na umbo kama la mtu bali hiyo inamaana kubwa tofauti na hiyo ya kiuandishi. Naomba kuwasilisha.
Niliwahi kujiuliza sana kuhusu Mungu kutuumba kwa mfano wake. Mfano wake kivipi kisura, kiumbo, kifikira au kimatendo? Kwenye kufanana kisura Mungu ni handsome, disfigured au? Kufanana kiumbo nako kunagoma kwani kama miguu ya nini kwa Mungu wakati yeye yuko kila sehemu kwa wakati mmoja, pua ya nini kwake au meno ya kuuma au kulia chakula gani? Kama ni kufanana kifikira au kimatendo napo vinagoma kwa sababu Adam na Hawa walikuwa na fikira na matendo yenye kasoro hadi kufikia kutenda dhambi.
 
Nimeipenda zaidi picha hiyo na ujumbe wake. Ukikutana na mtu aliyosoma kitabu kimoja tu tena cha dini yake tu! Hawa watu huo ni shiida na ni hatari sana kwa ustawi wa sayari dunia, hawana maarifa kabisa ni wepesi wa hasira na kupinga vitu bila kufikiri nje ya box
Na ogopa sana mtu ambaye hawezi kubalance mambo ukimuonyesha leo bilauri iliyojaa kimiminika ukamwambia haya ni maji na kesho bilauri hiyo hiyo ikawekwa konyagi na mtu mwingine akaja kumwambia yale sio maji mnaweza kugombana naye
 
Niliwahi kujiuliza sana kuhusu Mungu kutuumba kwa mfano wake. Mfano wake kivipi kisura, kiumbo, kifikira au kimatendo? Kwenye kufanana kisura Mungu ni handsome, disfigured au? Kufanana kiumbo nako kunagoma kwani kama miguu ya nini kwa Mungu wakati yeye yuko kila sehemu kwa wakati mmoja, pua ya nini kwake au meno ya kuuma au kulia chakula gani? Kama ni kufanana kifikira au kimatendo napo vinagoma kwa sababu Adam na Hawa walikuwa na fikira na matendo yenye kasoro hadi kufikia kutenda dhambi.
Kuna kitu kinachotufananisha; nafikiri ni ule uwezo wa kutambua jema na baya labda.
Quran imesema wazi kuwa Mwenyezi MUNGU ni wa pekee, hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hana anachofanana nacho hata kimoja. Hili ni andiko ambalo niliamua kulichagua ña kuliamini
 
Ndio maana tunaambiwa tutunze roho zetu maana zisijejikuta zinaingia kwenye mwili wa kuku! Just joking, haya mambo yananizidi upeo. Mfano wa software na hardware umekaa poa sana kwa wale wagumu kuelewa.
Nimekusoma ila utata bado upo sana kwenye mambo mengi ...
 
Iko hivi mwili ni jumba roho ni pumzi ya uhai hivi viwili vikiungana ndio vinatengeneza nafsi
Kama mwili (jumba) na roho (pumzi ya uhai) vikiwa pamoja vinatengeneza nafsi basi naweza kusema hiyo nafsi ndiyo mtu fulani yaani ndipo tunapompata mtu mmoja mmoja tofauti kabisa na mwingine duniani. Na kama tafsiri hiyo ni sahihi basi mtu (nafsi) anabaki kuwa mwili plus roho. Yaani bila kuihesabu nafsi kwa sababu mwili na roho ndivyo vinavyotengeneza nafsi na haiwezekani mwili, roho na nafsi vitengeneze tena nafsi.
 
Niliwahi kujiuliza sana kuhusu Mungu kutuumba kwa mfano wake. Mfano wake kivipi kisura, kiumbo, kifikira au kimatendo? Kwenye kufanana kisura Mungu ni handsome, disfigured au? Kufanana kiumbo nako kunagoma kwani kama miguu ya nini kwa Mungu wakati yeye yuko kila sehemu kwa wakati mmoja, pua ya nini kwake au meno ya kuuma au kulia chakula gani? Kama ni kufanana kifikira au kimatendo napo vinagoma kwa sababu Adam na Hawa walikuwa na fikira na matendo yenye kasoro hadi kufikia kutenda dhambi.
Mmmh.... Mungu akasema na tuumbe mtu kwa mfano wetu...! Mungu ni roho sio mwili yeye ni universal soul , roho huingia kwenye jumba lolote, concept ya Mungu kuumba mtu kwa mfano wake ni kiroho zaidi ya kimwili ila kutokana na jinsi tulivyoumbwa tunapata picha halisi ya Mungu
 
Kama mwili (jumba) na roho (pumzi ya uhai) vikiwa pamoja vinatengeneza nafsi basi naweza kusema hiyo nafsi ndiyo mtu fulani yaani ndipo tunapompata mtu mmoja mmoja tofauti kabisa na mwingine duniani. Na kama tafsiri hiyo ni sahihi basi mtu (nafsi) anabaki kuwa mwili plus roho. Yaani bila kuihesabu nafsi kwa sababu mwili na roho ndivyo vinavyotengeneza nafsi na haiwezekani mwili, roho na nafsi vitengeneze tena nafsi.
Sahihi kabisa
 
Mmmh.... Mungu akasema na tuumbe mtu kwa mfano wetu...! Mungu ni roho sio mwili yeye ni universal soul , roho huingia kwenye jumba lolote, concept ya Mungu kuumba mtu kwa mfano wake ni kiroho zaidi ya kimwili ila kutokana na jinsi tulivyoumbwa tunapata picha halisi ya Mungu

Thibitisha kwamba kuna MUNGU!.
 
Kuna mahali tulijadili kwa undani kuhusu roho zinazotangatanga, hizi kwa kiasi kikubwa ndio huleta shida katika jamii, japo kuna wakati yaweza kuwa dhana za kufikirika tuu
Tukirudi kwenye swali roho ni moja tu ndani ya mwili
DUUUH! naikumbuka hyo mada mkuu...Sema ndo ivyo bado ni kiza au fumbo kubwa sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom