Fumbo la uumbaji, roho na mwili uozao

Fumbo la uumbaji, roho na mwili uozao

HII
Lakini kwenye vitabu vitakatifu (nimewahi soma kwenye biblia) kwamba wakati wa uumbaji Mwenyezi Mungu alikuwa akiumba viumbe wengine (including wanyama kama sokwe) kwa kunena tu na wakawepo. Lakini wakati wa kumwuumba mwanadamu alitumia mikono yake na udongo kisha akampulizia pumzi ya uhai ambayo in essence ndiyo roho. Sasa inakuwaje na wanyama ambao hawakupuliziwa pumzi ya uhai (roho) nao wawe na roho? Na je kama nao wana roho wanapokufa na miili yao kuoza, roho (energy) zao nazo ubaki na kutafuta jumba jingine?
THREAD HII NITAICHANGIA TENA KESHO
 
Wana roho na wana utambuzi tena mkubwa kuliko binadamu
Na kama wana utambuzi mkubwa kuliko binadamu nadhani ni katika specific areas siyo general. Kwa sababu generally binadamu ndiye anajulikana kwamba ana utambuzi mkubwa kuliko viumbe wote duniani. Ila kwenye specific areas ndiyo tunaweza kuona kuwa baadhi ya viumbe wanatuzidi mfano kwenye uwezo wa kunusa, binadamu tunazidiwa na tembo, mbwa, farasi, panya n.k.
 
Maada fikirishi sana, tungekuwa na aina fulani ya uthubutu kama huu wa kujiuliza maswali magumu na kuja na majibu chanya, tusingekuwa na tanzania ya hovyo kiasi hiki.... Watawala wanafikiri kawaida sana na ndio waliopewa jukumu la kuamua baadaye yetu katika ulimwengu huu wa kuonekana..
Nguvu ya ubuni ndiyo roho hiyo... Big up mshana
 
swali langu limetoka hapa .... KILA MMOJA KUITUNZA ROHO YAKE VYEMA ... huyo kila mmoja ni nani?? Mwili au nini
Kila mmoja = mtu = mwili + pumzi ya uhai yaani roho. Sasa mwili na roho vinaambiwa kwa pamoja kutunza vyema roho. Lakini wakati huo inaonekana roho ndiye mwenye nguvu kuliko mwenzie (mwili) na ndiye mwenye kuamua nini mwili ufanye kimawazo au kivitendo. Kisha roho kwa uwezo alionao wa kuweza kujitegemea anaamua kumkimbia mwenzake (mwili). Mwenzake (mwili) anabaki pekee yake asijue la kufanya hatimaye anaoza. Roho kwa vile ana uwezo wa kujitegemea anabaki sehemu fulani (na kutafuta mwili au jumba jingine? I don't know!). Sasa najiuliza hapo ni nani alitakiwa kumtunza mwenzie roho au mwili? Au mtu ajitunze nikimaanisha wote wawili (mwili na roho) watunzane? Na kama wanatunzana why baadae roho amkimbie mwenzie na kumwacha akioza na kukimbilia mwili au jumba jingine? Mambo yanachanganya sana. Ndiyo maana nashawishika kuamini kwamba Mungu yupo na ndiye mwamuzi wa fate ya kila mmoja.
 
Kwa kiasi Wanga wanasiri ! Elimu ya wachawi inafaa iwekwe wazi iliipate kudadavuliwa na kuwekwa kiwenye jaribio!
cc mshana jr
Tatizo hapa kuna vitu viwili vinaleta shida ...
Roho = software,
Mwili = Hardware
Mwili + Roho = Computer

Shida inakuja pale roho inapouona mwili (housing) umechoka na tayari wenyewe (moyo) umeishakuwakwa upgraded, hapo ndo moyo unapoenda kwa mwili mwingine
 
Mkuu kumbuka moyo ni kitu tofauti na roho. Moyo nao ni moja ya vitu vinavyooza kama sehemu ya mwili (jumba). Moyo uoza kama ilivyo kwa utumbo na figo wakati roho anapomkacha best yake mwili na kuondoka kwa mwendo mdogo mdogo.
 
Kama ukifuatilia na kusoma kwa umakini hapa nina maanisha kama ni mzito wa kuelewa lazima urudie mara mbili au mara tatu,alichokieleza mkuu mshana ni kwamba MWILI,NAFSI NA ROHO they all depend each other katika uhai wao although roho itabaki baada ya mwili kupotea hii nadharia ni kama ile ya utatu mtakatifu kwa wale wa kristu.ili uweze kuelewa kwa undani inahitaji ushibaji wa elimu ya roho.sasa ni vizuri swali likabaki kwa mkuu mshana je ni jinsi gani ya kuweza kuishi kwa kuzitunza roho?
 
Mkuu Mshana umejibu vizuri. Lakini bado napata swali kwamba kama baada ya roho kuachana na mwili na mwili huo kuoza, hiyo roho (energy) kama ina uwezo wa kutafuta jumba lingine si ndiyo kujitegemea huko wakati mwili (jumba) wenyewe hauwezi kujitegemea kwa kutafuta roho (energy) nyingine?
Maswali kuhusu roho yapo very critical kujibiwa na mtu mwingine,

hata mshana Jr ni kama unamuonea tu kumuuliza maswali sababu anaweza kupa jibu ambalo kwako si rafiki.

inabidi tu muhusika mwenyewe utumie hekima yako binafsi kujiuliza,kuyatafakari na hatimaye kuja na majibu.

Lakini ukisema umuulize mtu mwingine,utakuta kila jibu la swali unalomuuliza, linazaa swali lingine.
 
Umenipa changamoto nitafanya hivyo

Mshana,story za uumbaji,nk,nk za kibiblia ni uongo tu,waandishi wa biblia ni questionable human beings just like us,story wamewaza vichwani mwao,hamna ushahidi na evidence whatsoever...

Vitu vyote vya biblia na kiimani ambapo havileti sense emperically hua ni vya kutupa right away...

Mwandishi wa hiyo hadithi ukimuuliza source yake ni wapi hatakua na cha kujibu,atakuambia ameoteshwa ndoto,mungu kamtokea,which is not true.

The biggest lie on earth ni stori za vitabu vya dini...hakuna biggest lie bigger than that
 
Quran 15:26 Na tulimuumba mwanadamu kwa udongo mkavu unaotoa sauti(unapogongwa),unaotokana na matope meusi yaliovunda...
"NA TULIMUUMBA mwanadamu kwa udongo mkavu" Huyo ni Mungu mmoja nafsi tatu Baba Mwana na Roho Mtakatifu.
 
Maswali kuhusu roho yapo very critical kujibiwa na mtu mwingine,

hata mshana Jr ni kama unamuonea tu kumuuliza maswali sababu anaweza kupa jibu ambalo kwako si rafiki.

inabidi tu muhusika mwenyewe utumie hekima yako binafsi kujiuliza,kuyatafakari na hatimaye kuja na majibu.

Lakini ukisema umuulize mtu mwingine,utakuta kila jibu la swali unalomuuliza, linazaa swali lingine.
Mkuu ni sahihi ukisemacho. Lakini kumbuka hapa ni mjadala ambao unachangiwa na mdau yoyote mwenye uelewa kama watu mnapokuwa sehemu moja na mkawa mnajadili kitu fulani. Si lazima swali likawa linaelekezwa kwa mtu mmoja aliyejibu swali la awali na kwa maana hiyo Mshana Jr alipojibu swali la awali lililonisababisha mimi kupata swali jingine sikumaanisha kwamba ni lazima yeye Mshana Jr ndiye anijibu. Ni mjadala ulio wazi kwa mdau yeyote na ndiyo maana hata wewe umeweza kuni quote na kuchangia hapo juu.
 
Mkuu ni sahihi ukisemacho. Lakini kumbuka hapa ni mjadala ambao unachangiwa na mdau yoyote mwenye uelewa kama watu mnapokuwa sehemu moja na mkawa mnajadili kitu fulani. Si lazima swali likawa linaelekezwa kwa mtu mmoja aliyejibu swali la awali na kwa maana hiyo Mshana alipojibu swali la awali lililonisababisha mimi kupata swali jingine sikumaanisha kwamba ni lazima yeye Mshana Jr ndiye anijibu. Ni mjadala ulio wazi kwa yeyote na ndiyo maana hata wewe umeni quote na kuchangia hapo juu.
Basi sawa.
 
jamani mbona kutishana. kama roho ilishakuwepo ikaiingia kwangu na itarejea ilikotoka. so mbona mm sikumbuki nlikuwa nani kabla ya kuzaliwa?
 
jamani mbona kutishana. kama roho ilishakuwepo ikaiingia kwangu na itarejea ilikotoka. so mbona mm sikumbuki nlikuwa nani kabla ya kuzaliwa?
Hii ya roho kuhama kutoka kwa mtu huyu na kuhamia kwa mwingine kisha kwa mwingine tena inaleta utata. Kwa sababu itamaanisha kwamba roho zitakuwa chache huku watu wakiwa wengi siku zote kwa vile kazi ya roho itakuwa ni kuhamia tu kwa watu wapya wanaozaliwa kama kuziba nafasi vile. Mfano kama ukijumlisha watu walio hai leo dunia nzima (around 7.5bl) na waliokwisha kufa (mfano wawe 2.5bl so far) jumla wakiwa 10 billion roho zinaweza kuwa 10m ( kila roho ikiwa imefanya replacement kwa watu 1,000). Huo ni mfano tu.

Na kwa wale tulio na imani kwamba kuna siku Mungu atatoa hukumu kwa watu wake kulingana na matendo yao hao watu pamoja na roho zao sijui zitahukumiwaje katika mazingira ambayo roho zilikuwa ndani ya watu tofauti 1,000 na kila mtu akiwa na matendo yake tofauti kabisa na mwingine. Au miili itahukumiwa with the exclusion of their souls?

Najiuliza tu.
 
Roho ni energy hivyo haiweZi kujitegemea bali hutafuta jumba lingine refer dhana ya reincarnation, au roho zinazotangatanga,mizimu nk

Kwa muktadha huu nakubaliana nawe roho kwakuwa ndio uhai ina uwezo wa kujitegemea kwa kutafuta kiwanja kingine lakini mwili ni jumbabovu lisilo na uwezo wowote

Moyo ni sehemu ya mwili inapokaa roho..moyo ni kabati ndani ya nyumba sawa na control box kwenye gari

Hiki umeandika nini?,mbona unakataa kisha unakubali ?Ama huelewi unachoandika?.
Mwanzo umesema roho haiwezi kujitegemea kisha jamaa kakutingisha kidogo tu umehama na kukubaliana nae sasa nini ni nini.
Kuna siku niliwahi kukuambia mshana Jr kwamba upande huu haukufai nadhani hukunielewa.
 
Sio kosa lako kwa hiki ulichoandika ila kwa manufaa yako na ya wengine pia ni kwamba kwenye muunganiko wa kutengeneza nafsi roho haiweZi kujitegemea hilo ndio lilikuwa jibu langu la kwanza kisha jamaa akaja na reply ambayo ndio ilizaa jibu langu la pili kuwa kwenye ishu ya utengano roho huwa huwa ni kitu chenye mwendelezo ikiwa huru...haya mambo hayana jibu moja linalojitegemea kwakuwa kila aina ya swali huzaa jibu tofauti kwa muktadha wa maudhui yake.... hii elimu ya roho iko deep na vast kiasi kwamba usipokuwa makini na ukawa na rigid mind kama yako ni rahisi kutoa conclusion kama hii uliyotoa wewe....jisikie kuniuliza chochote nitakujibu kwa upole
791cb4f045cb80bc7ed7c4cf59a918cc.jpg
 
Kila mmoja = mtu = mwili + pumzi ya uhai yaani roho. Sasa mwili na roho vinaambiwa kwa pamoja kutunza vyema roho. Lakini wakati huo inaonekana roho ndiye mwenye nguvu kuliko mwenzie (mwili) na ndiye mwenye kuamua nini mwili ufanye kimawazo au kivitendo. Kisha roho kwa uwezo alionao wa kuweza kujitegemea anaamua kumkimbia mwenzake (mwili). Mwenzake (mwili) anabaki pekee yake asijue la kufanya hatimaye anaoza. Roho kwa vile ana uwezo wa kujitegemea anabaki sehemu fulani (na kutafuta mwili au jumba jingine? I don't know!). Sasa najiuliza hapo ni nani alitakiwa kumtunza mwenzie roho au mwili? Au mtu ajitunze nikimaanisha wote wawili (mwili na roho) watunzane? Na kama wanatunzana why baadae roho amkimbie mwenzie na kumwacha akioza na kukimbilia mwili au jumba jingine? Mambo yanachanganya sana. Ndiyo maana nashawishika kuamini kwamba Mungu yupo na ndiye mwamuzi wa fate ya kila mmoja.
Katika hivyo vitu viwili umesahau kiunganishi kimoja muhimu sana NAFSI ...huyu nafsi ndie zao la mwili na roho
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom