Mike Tyson ndani ya Francis Ngannou dhidi ya Tyson Fury

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
145
335
JUZI (Oktoba 28), Kingdom Arena, Riyadh, Saudi Arabia, ilipigwa boxing match yenye tafsiri nne;

Mosi; Bingwa wa Mixed Martial Arts, Francis Ngannou, kucheza mechi ya kwanza ya Boxing dhidi ya mpinzani mgumu mno, halafu bingwa wa dunia uzito wa juu, Tyson Fury.

Pili; The high risk fight; Fury ana pambano la hundreds of million dollars dhidi ya bingwa mwenzake wa uzito wa juu, Oleksandr Usyk, Desemba 23, 2023. Fury angechapwa na Ngannou, dili lingeingia kirusi.

Tatu; Ni baba dhidi ya baba. Fury akiwa mtoto, afya gogoro kwa sababu alizaliwa njiti, alipewa jina “Tyson” na baba yake, John Fury, kwa imani kuwa mwanaye angekuwa mpambaniaji kama Mike Tyson.

Hivyo, Mike Tyson ni kama Baba wa Fury. Na amekuwa akijivunia mafanikio ya Fury kwa sababu anabeba jina lake.

Kuelekea mechi ya Fury vs Ngannou “The Battle of the Baddest”, Ngannou aliomba coaching ya Mike, ambaye alikubali. Mike alisema alitaka awe sehemu ya fight bora duniani, hivyo akamnoa Ngannou.

Nne; Kipimo cha Mike kufundisha boxing. Performance ya Ngannou dhidi ya Fury, ndio ingetoa tafsiri ya skills za Mike kama kocha wa Boxing.

Twende kwenye fight; nani alisema ni exhibition match? Ilikuwa total war! Fury alianza vema round ya kwanza, ya pili Ngannou aliufanya ulingo kuwa mdogo kwa Fury. Ya tatu, Ngannou akaiduwaza dunia alipomlambisha sakafu Fury kwa left hook.

Kuna kitu utakipenda kuhusu Fury. Mwanamichezo halisi. Hapanic mchezoni. He was knocked down, alinyanyuka. Kengele ikamwokoa.

Round ya nne, Fury aliurejesha mchezo upande wake. Kisha ya tano, sita na saba. Ile ya nane, Ngannou alimnyanyasa vibaya Fury. Hakuna aliyetarajia, Ngannou angeenda distance na Fury kwa 10 rounds.

Fury alishinda kwa split decision. Majaji wawili walimpa Fury 95 – 94 na 96 – 93. Jaji mmoja alimpa Ngannou 95 – 94.

Unapaswa kumheshimu Ngannou. Kutoka maisha hohahe Cameroon, alifanya kazi ngumu akiwa na umri wa miaka 10. Alikamatwa mara sita akijaribu kuvuka mpaka, kuingia Ufaransa. Akalala mitaani Paris. Mwaka 2015 akawa Bingwa wa Dunia UFC Heavyweight.

Jana, akaonesha kuwa sasa Boxing imepata mtu na Mike ni bonge la kocha.
 
Ukicopy andiko la mtu toa acknowledge kwa mhandishi
 
Back
Top Bottom