Fukuza Marekani nchini

Fukuza Marekani nchini

Kabla ya kufanya hivyo ujipange. Una sasa mwenyekiti wako analia kila siku Zimbabwe iondolewe vikwazo mpaka sasa Hawana hela yao wanatibiwa SA na nchi jirani. Sasa kwa wewe hapa Tz Anza na wagknjwa wanaopata ARV wapatao 2m plus wanaopata dawa bila kukata for 5 years kata uone msipo tanga a janga la kitaifa mpaka viongozi wenu.
Wanatibiwa SA tu, mpaka toilet paper itoke huko. Ukiona gari ya Mzim inatoka SA kuelekea kwao utaweza kufikiri kiama kimefika kwa ilivojazwa korokoro! Mungu atuepushe na laana na hasira za hawa watu.
 
Kutokana na historia yako kama ulivoeleza utakuwa ni dogo tu, hulikumbuki DONA MANJANO la miaka ya 82-84 mpaka likamfanya NYERERE aachie ngazi!
 
Ukiwa na kiburi...Uwe na Jeuri.

Kama huna jeuri ficha uwoga wako
Nilivyoona "...Huko kwa Badhad Al Asady Syria tokea 2011 nipo kidato cha nne amewachafua vibaya watu wa huko." Sikuendelea kusoma naomba summary ya hili bandiko maana kuna mchanganyiko... ama dalili za kumbukizi za Saddam Hussein wa Libya...
 
China pamoja na kuwa imetuzidi kwa uchumi na technolojia lakini company mmoja ya Marekani Google ilitetemesha nchi nzima. Palikuwa hapatoshi China. Kiufupi China ilitia huruma.
Sasa wewe kajamba nani unakimbizana na ukosefu wa madawati unaanza kuivimbia Marekani. Kila kitu unachotumia ni cha mabeberu. Hapo ulipo unapata hivyo vihela na wewe unaona umefika. Hawa mabeberu waache kama walivyo. Hii JF unayotumia bila mabeberu hata usingeiona. Mimi napata pesa kutoka kwenye makampuni ya mabeberu kama Propeller ads na ad.fly. Search engine unatumia ya mabeberu, movie unaangalia za mabeberu, elimu umeipata ya mabeberu. Bila mabeberu sasa hivi ungekuwa unachunga ng'ombe. Huwa unaangalia video YOUTUBE? Unaishi kwenye dunia ya 3 kwahiyo kuwa mpole.
Watu kujifanya mnajua!!!!
Ebu katafuteni elimu ndio muongee.
Hiyo Google iitetemeshe China uwezo inatoa wapi???
Huyo beberu unayemsifia ana watu waliomfanya atambe.
Hususan hiyo USA ni nchi iliyojengwa na watu wa tech wa asili ya India,Germany,Israel.
 
inawezekana likawa wazo zuri.. ila kabla hatujawafukuza nilitaka kujua tutaathirikaje na hayo maamuzi?
 
Hivi tangu wasitishe kutufadhiri umeme wa REA kutokana na chaguzi zetu za 2015 KUWA rigid je status ya kuweka umeme inaendelea vipi vijiji vyote
 
Chukua mfagio uifagie nyumba yako ndio uinyoshee kidole marekani. Uvundo unawafikia majirani mpaka wa mtaa wa pili.
 
Hivi tangu wasitishe kutufadhiri umeme wa REA kutokana na chaguzi zetu za 2015 KUWA rigid je status ya kuweka umeme inaendelea vipi vijiji vyote
Inaendelea vizuri tu na tena iko vema kuliko kipindi wanatufadhili umeme.
 
Watu kujifanya mnajua!!!!
Ebu katafuteni elimu ndio muongee.
Hiyo Google iitetemeshe China uwezo inatoa wapi???
Huyo beberu unayemsifia ana watu waliomfanya atambe.
Hususan hiyo USA ni nchi iliyojengwa na watu wa tech wa asili ya India,Germany,Israel.
Google kampuni ya Marekani ilitetemesha. Mchina akawa anatapata kuunda OS ya simu yake Huawei mpaka leo hola. Kaenda kwa Putin waungane ili wasitumie dola. Unaijua hata OS ya Android anamiliki nani? Google akiipiga marufuku China isitumie Os ya Android kwenye simu zake zote. China ndiyo kwaheri hivyo. Hata hii JF ni kazi ya mabeberu. China iliiba teknolojia ya beberu marekani na imetajirika sana kupitia product za marekani. Unaenda kununua simu ya Nokia, unakuta na copy ya kichina. Vitu vingi feki vinatoka china, watu waliokumbatia ujamaa lakini wanaiba teknolojia kwa mabeberu. Ujamaa ushaisha kitambo
Elimu ninayo ya kutosha ila naona wewe umepata elimu lakini hata haikusaidii kung'amua mambo madogo madogo. Nyerere alikuwa na mawazo kama yako ya socialism lakini alifeli. Sasa wewe hata milioni 20 hauna benki unaanza kukimbizana na Beberu. Unamjua Beberu au unamsikia? Hawa jamaa tukiri tu ndiyo wanaendesha dunia. Sasa wewe kajamba nani, na nchi yako inakimbizana na upungufu wa madawati na matundu ya choo uanze kupigana na Beberu.
Kama Muisrael au Mhindi anafanya kazi Marekani. Hiyo Kampuni itakuwa ya kihindi au Marekani? Timu ya France ilichukua kombe la dunia na ukiangalia Wafrika wengi kama Mbape, Pogba na wengine wana asili ya Africa. Sasa hilo kombe wamechukua wafrika au wafaransa? Utabaki na hayo hayo ohh wafrika wanafanya kazi ulaya na maendeleo ya Marekani yameletwa na watu wanaotoka nchi mbalimbali ndiyo sikatai ila maendeleo yatakuwa ya Marekani. Hao watu hawalipi fedha kama ujira? Huyo ndiyo Beberu akili nyingi ,nguvu kidogo. Hata wewe ukipata chance unaweza kuomba uraia wa Marekani na ukaajiriwa kuwa afisa wa CIA au Kama unakipaji unacheza kwenye Timu ya taifa. Wewe ulipo hata kubadili syllabus ya elimu yako umeshindwa leo ukimbizane na Beberu utamuweza? Fishing industry in Norway. Ha ha ha ha
WEWE UNAYEHANGAIKA NA MATUNDU YA CHOO, MAJI NA UHABA WA MADAWATI. WENZIO WANANGAIKA KWENDA KWENYE SAYARI KAMA MARS.
 
inawezekana likawa wazo zuri.. ila kabla hatujawafukuza nilitaka kujua tutaathirikaje na hayo maamuzi?
Hayo ndiyo mambo ya Mugabe. Unampinga Beberu halafu ukiuugua unaenda kwake kutibiwa lazima akudunge sindano ya sumu. Viongozi wa afrka hawajitambui kabisa. Wewe unatumia kila kitu cha mabeberu halafu unasema wanakuonea wivu kwa lipi? Ghadafi alikuwa anajisifia sana kuwa mabeberu hawamuwezi lakini alitolewa kirahisi sana kupitia watu wake. Usicheze na Marekani. Kiduku mwenyewe alikuwa mwepesi kama karatasi. Tanzania inaweza kuiwekea vikwazo Marekani?
 
Na, Robert Heriel.

Nani asiyejua kuwa Marekani ndiye Baba wa Ukoloni mamboleo. Nani asiyejua kuwa Marekani ndiye aliyejivika kibweka miaka ya 1945 kufanya Decolanization ili naye apate ulaji kupitia mlango wa nyuma wa Neo-colonialism. Nani asiyejua nauliza.

Huyu marekani anafahamika kwa siasa zake za ujanja ujanja wenye kuumiza. Yeye akiwa Baba wa Mabeberu akishirikiana na vibeberu vidogo vidogo kutoka magharibi. Amejimilikisha hii dunia na kuifanya kama kigoda cha kuwekea Kalio lake.

Nani asiyejua Marekani ni moja ya watu waliohusika kumtoa kimabavu Muammar Ghadafi, Sadamu Hussein kwa kile wakiitacho kupigania demokrasia. Huko kwa Badhad Al Asady Syria tokea 2011 nipo kidato cha nne amewachafua vibaya watu wa huko.

Kupitia mashirika yake ambayo ameyaita yakimataifa amekuwa bingwa wa kuunda propaganda zenye malengo mbalimbali. Lakini kwa kawaida Marekani anafahamika kama bingwa wa kutia watu hofu. Bingwa wa fitina wa siasa za dunia.

Miezi iliyopita alitoa taarifa kuwa Tanzania inaweza kupata shambulio la kigaidi wakati wowote hivyo inawatahadharisha watu wakazi wake. Ikavunja taratibu za kutoa taarifa kama hivyo bila kuwashirikisha mamlaka husika za ndani. Tukio lile waliomba radhi. Nikawapongeza kwa kuwa Waungwana japo macho bado lazima tuwatolee.

Haya Jana wamewapa tahadhari watu(hasa watu wa marekani) wanaotaka kuja Tanzania kuwa kuna matishio yanayohatarisha maisha ya watu nchini Humu.
Matishio hayo;
1. Tishio la ugaidi.
2. Tishio la ugonjwa wa Ebola
3. Tishio la Ujambazi na uporaji.
4. Mashoga kunyanyaswa na kupigwa vita n.k.

Hoja hizo na zingine ndizo zimewafanya Wamarekani watoe tahadhari kwa rai wao.

Marekani lazima ajue haya na bila shaka anayajua.
Ebola ni ugonjwa usiojificha kama Ukimwi. Ebola ikianza hakuna siri. Ebola ni kama pembe la ng'ombe wakati UKIMWI ni kama Nyeti za Kuku.

Marekani inaposema Serikali inaficha Ebola sijui inazungumzia nini kama sio kutengeneza hofu kwa watu kama ilivyokawaida yao. Kama hawana mpango wa nyuma ni jambo gani wanataka kulifikisha.

Tanzania haina chakujificha katika EBOLA. Yapo magonjwa mengi isijifiche Why iwe kwa Ebola. Yalikuja mafua ya ndege yakapiga maeneo ya Arusha huko ndani ndani serikali ikatangaza. Ilikuja Dengue serikali ikatangaza.

Sasa huyo Ebola na Marekani wana uhusiano gani mpaka sisi tushindwe kumuanika kuwa katinga nchini. Marekani acheni zenu. Tutawafukuza. Ili mfanye hizo propaganda zenu vizuri.

Lini hapa nchini Raia wa kigeni wameishi kwa bughuza. Lini hapa nchini Wamarekani wamenyoshewa hata kidole na Raia wetu bora kuliko wote dunia wenye upendo.

Licha ya ninyi wageni hususani Wamarekani kutesa na kujivinjari kuliko Wageni katika ardhi yetu lakini Watanzania wanawapenda na kuishi na ninyi vizuri. Alafu leo muongee mambo ya kipuuzi puuzi mkidhani sisi ni wajinga.

Ningekuwa mimi ndiye Kiongozi wa Taifa hili. Ningewatimua. Ningewafukuza ili muende mkafanye Propaganda zenu za kipuuzi huko nje kwa uhuru.

Nisingesubiri muwatahadharishe watu wenu kuwa wasije huku. Ningewagukuza na kuwapiga marufuku kukanyaga nchi hii mpaka nitakapoondoka.

Ati mashoga tunawanyanyasa. Mulitaka wafanye mambo yao yakipuuzi mitaani. Kama ninyi mnawajali sana hao Mashoga na wapenzi wa jinsia moja. Wachukueni muende nao huko kwenu mnapowapa uhuru wa kufanya upuuzi wao.

Hata hivyo bado serikali inamambo mengi. Bado ingehitajika ishuhulike haswa na watu hawa ili muongee vizuri.

Tunajua wapo mawakala wenu mliowasomesha enzi za nyuma wanaowasaidieni katika kueneza upumbavu. Sasa mnataka mrudishe pesa zenu mlizotumia kuwasomeshea. Tunajua wapo wanaonufaika na yale mnayoyapigania. Tunajua yapo mashirika binafsi mnayoyadhamini kwa ajili ya kuwapigieni chapuo. Tunajua wapo vibaraka katika baadhi ya makanisa uchwara na wanasiasa uchwara.

Tunajua wapo Wachungaji mnaowatumia wamtumie Yesu kutetea mashoga. Sasa taarifa ni hii. Waambieni hao vibaraka wenu kuwa kama Yesu naye alitetea Hao mashoga mwambieni naye hatumtaki. Ingawaje tunajua hawezi kufikia kiwango hicho cha upuuzi bali ninyi ndio mnamlisha maneno.

Fukuza hao Wamarekani ili wajue wao sio lolote katika taifa hili. Tunajua tutapata tabu kwa miaka hii kumi kutokana na mazoea mabaya ya utegemezi na athari za Ukoloni mamboleo lakini Ukweli ni kuwa tutakuwa Stable baada ya miaka 20.

Marekani lazima ijue kuwa Taifa hili ni taifa kubwa. Linavijana wenye fani zote hata zisizokuwepo Marekani. Linavijana wajuvi wa fani mbalimbali. Lina wanawake mashujaa na wachapakazi.

Kinachowakwamisha ni baadhi ya viongozi vibaraka na Wafanyabiashara Wakubwa wanaotegemea zaidi Bidhaa za kibeberu zinazoua viwanda vyetu.

Serikali fukuza Marekani irudi kwao ikafanye propaganda zake vizuri za kuchafua nchi yetu.

Ni muda wa Kumthibitishia Marekani na Vibaraka wake kuwa wao sio lolote zaidu ya chochote keenye taifa hili.

Wapo watu watakaosema kuwa oooh! Naongea porojo. Mara taifa letu ni masikini. Sijui Blah Blah hapa.

Taifa hili sio masikini bali linahitaji msuko wa kifikra kwa vijana kuhusu mtazamo kuhusu ubora wetu.

Sisi ni watu bora. Kila mwenye akili analijua hili. Kila kijana mwenye mapenzi na nchi hii analijua hili. Nna ataungana na jambo hili.

Najua wapo maadui hata hivyo ni lazima muwepo ili tuweze kuona nguvu zetu tunapopambana na nyie. Tunajisikia fahari na mchezo mzuri kupambana na adui zetu ambao baadhi yao ni ndugu zetu tuliozaliwa katika taifa hili.

Mnajua tutawashinda ninyi wenyewe. Ninyi wenyewe mnajua sisi tumewazidi mambo mengi muhimu na yalazima.

Fukuza Marekani ikafanye siasa za kipropaganda zake vizuri. Isijeona tunaiogopa na ipate funzo kuwa sisi sio watu wa mchezo.

Andiko hili ni moja ya maandiko yangu yanayolenga kuzipa nguvu mitazamo ya vijana na kuibadili iwe bora bila woga.

Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi.
0693322300
Hiyo nchi ina wivu sana hawataki kuona watu wakipata amani, na maendeleo.wao wamekuwa viranja wa dunia
 
Unaropoka sana then inaonesha ww ni mjawa kasumba huna ulijualo hata mifano ulotoa butu.
SIJASEMA KUWA WAFANYAKAZI WA KIHINDI SIJUI BLAA BLAA NYINGI KM USEMAVYO MAANA UMEROPOKA SANA NA WALA HAUJUI UWEZO WANGU WA KIAKILI.
HIYO CHINA UNAYOISEMEA WW INA INVENTIONS ZAKE ZINATUMIKA WORLDWIDE.
HIYO CHINA UNAYOSEMEA WW VIFAA VYA UTENDEAJI KAZI VYA VIWANDANI USA ANANUNUA KWAKE.
HIYO CHINA UNAYOISEMEA WW INA RESERVES YA DOLLARS KUMSHINDA HUYO BEBERU.
HIYO CHINA UNAYOISEMEA WW NDIO PROCESSOR WAKUBWA WA HT IPHONE UNAYOTAMBA NAYO.
HALAFU NIKUWEKE SAWA KTK ISHU YA GOOGLE.
ILE ILIKUA NI MIONGONI MWA TRADE WAR KAT YA USA NA CHINA.
KMA ULIKUA HAUJUI USA ILIONEKANA KUUMIA NDIO MAANA GOOGLE WENYEWE WALIOMBA USA ITOE SANCTIONS KWA CHINA.
NA KM HAUJUI WACHINA WANATEST HARMONY S IKIKUBALI BEBERU WAKO AJIANDAE KULIA.
KWASABABU CHINA ANA CONTRIBUTE 60% OF MANUFACTURED GOODS DUNIANI.
ANATENGENEZA FAKE NA ORIGINAL PIA.
SIKATAI KUNA BAADHI YA TECH ANAIBA NA SIO KWA BEBERU TU HADI KWA MJAPAN HALAFU HAISHII HAPO ANAI MODIFY INAKUA BORA KULIKO ALIYOIIBA.
MATHALAN KTK BULLET TRAINS CHINA NDIYE MTENGENEZAJI BORA WA MAGLEV TRAINS KULIKO GERMANY MUHASISI.
KWAHIYO USIMCHUKULIE CHINA POA FUNGA BAKULI.

KUHUSU TECH ZA USA NINAMAANISHA KUWA TECH ZAKE NYINGI ANACHUKUA AMA ZINATOKA KWA WAHINDI,WAISRAEL,WAGERMANY.
HIVI HAUJIULIZI KWANN USA HUILINDA SANA ISRAEL?
NENDA KAKAE CHINI UTAFUTE CHANZO.
NA SASA HV BEBERU WAKO ANAPOROMOKA KISHENZI FUATILIA UCHUMI WA DUNIA UENDAVYO USIKAE KUJAZWA KASUMBA ZA MWAKA 47 HUKOOO.

TANZANIA NI NCHI AMBAYO IKIAMUA INAWEZA KUINUKA VZURI TU PASI NA KUMUOGOPA HUYO BEBERU KWASABABU KWAN HUYU BEBERU ANATUTAFUNA KMA ZIMWI KIUJANJA.
HALAFU FUATILIA UCHUMI WA NCHI YAKO PIA WAPI UMETOKA NA WAPI UNAKWENDA NA INAONEKANA HT MASUALA YA SYLLABUS HUYAJUI KUNGUNI WW.
HIVI SYLLABUS YA TZ NA USA ZINAFANANA?
KILICHOTUSHINDA SISI NI KUANDIKA MITAALA YA ELIMU KWA KISWAHILI TU LAKINI MITAALA MBONA IMEBADILISHIKA MARA KIBAO TU AU HAUNA MTOTO WW ANAYEENDA SHULE??

MWISHO NIKWAMBIE USIDHARAU MTU HUJUI UCHUMI WANGU UNAPOONGEA STICK TO THE TOPIC MWANAMAMA.
NA KM HUYO BEBERU WAKO USA AKILI NYINGI NGUVU KIDOGO KWANN TECH AZITOE NCHI ZINGINE KWANN WAZAWA WAKE WASIJENGE NCHI KWANN BOEING SHIRIKA ANALOTAMBA NALO LA NDEGE MWANZILISHI WAKE NI ASILI YA UJERUMANI WILHELM BOEING??
KWANN TECH NYINGI ANAZOTAMBA NAZO HAZINA ASILI YA WAZAWA WA MAREKANI?
NA KWANN TRADE WAR KATI YAKE NA MCHINA ANAFELI KM YEYE ANA AKILI NYINGI NA MCHINA ANAMNYOOSHA MBAYA MBOVU BEBERU WAKO NA BADO.
USIPENDE KUONGEA KWA KASUMBA NA DHARAU KUMBE UMEJAZWA VITU VYA MIAKA 47 HUKO.
Google kampuni ya Marekani ilitetemesha. Mchina akawa anatapata kuunda OS ya simu yake Huawei mpaka leo hola. Kaenda kwa Putin waungane ili wasitumie dola. Unaijua hata OS ya Android anamiliki nani? Google akiipiga marufuku China isitumie Os ya Android kwenye simu zake zote. China ndiyo kwaheri hivyo. Hata hii JF ni kazi ya mabeberu. China iliiba teknolojia ya beberu marekani na imetajirika sana kupitia product za marekani. Unaenda kununua simu ya Nokia, unakuta na copy ya kichina. Vitu vingi feki vinatoka china, watu waliokumbatia ujamaa lakini wanaiba teknolojia kwa mabeberu. Ujamaa ushaisha kitambo
Elimu ninayo ya kutosha ila naona wewe umepata elimu lakini hata haikusaidii kung'amua mambo madogo madogo. Nyerere alikuwa na mawazo kama yako ya socialism lakini alifeli. Sasa wewe hata milioni 20 hauna benki unaanza kukimbizana na Beberu. Unamjua Beberu au unamsikia? Hawa jamaa tukiri tu ndiyo wanaendesha dunia. Sasa wewe kajamba nani, na nchi yako inakimbizana na upungufu wa madawati na matundu ya choo uanze kupigana na Beberu.
Kama Muisrael au Mhindi anafanya kazi Marekani. Hiyo Kampuni itakuwa ya kihindi au Marekani? Timu ya France ilichukua kombe la dunia na ukiangalia Wafrika wengi kama Mbape, Pogba na wengine wana asili ya Africa. Sasa hilo kombe wamechukua wafrika au wafaransa? Utabaki na hayo hayo ohh wafrika wanafanya kazi ulaya na maendeleo ya Marekani yameletwa na watu wanaotoka nchi mbalimbali ndiyo sikatai ila maendeleo yatakuwa ya Marekani. Hao watu hawalipi fedha kama ujira? Huyo ndiyo Beberu akili nyingi ,nguvu kidogo. Hata wewe ukipata chance unaweza kuomba uraia wa Marekani na ukaajiriwa kuwa afisa wa CIA au Kama unakipaji unacheza kwenye Timu ya taifa. Wewe ulipo hata kubadili syllabus ya elimu yako umeshindwa leo ukimbizane na Beberu utamuweza? Fishing industry in Norway. Ha ha ha ha
WEWE UNAYEHANGAIKA NA MATUNDU YA CHOO, MAJI NA UHABA WA MADAWATI. WENZIO WANANGAIKA KWENDA KWENYE SAYARI KAMA MARS.
A
 
Vipi huko North Korea,Iran na China mbona anakwama??
Mbona hadi leo kashindwa kumuondoa Bashar Al Assad huko Syria??
Hayo ndiyo mambo ya Mugabe. Unampinga Beberu halafu ukiuugua unaenda kwake kutibiwa lazima akudunge sindano ya sumu. Viongozi wa afrka hawajitambui kabisa. Wewe unatumia kila kitu cha mabeberu halafu unasema wanakuonea wivu kwa lipi? Ghadafi alikuwa anajisifia sana kuwa mabeberu hawamuwezi lakini alitolewa kirahisi sana kupitia watu wake. Usicheze na Marekani. Kiduku mwenyewe alikuwa mwepesi kama karatasi. Tanzania inaweza kuiwekea vikwazo Marekani?
 
Bila shaka hapo ni bangi ndio zinazoongea ,eti tumeizidi marekani kila kitu,kweli bangi na mbaya.

Mkuu kwa Heshima kabisa nnaomba usiifananishe Bangi na mambo ya ajabu kama ya huyu mleta Uzi , Pls .
 
Unaropoka sana then inaonesha ww ni mjawa kasumba huna ulijualo hata mifano ulotoa butu.
SIJASEMA KUWA WAFANYAKAZI WA KIHINDI SIJUI BLAA BLAA NYINGI KM USEMAVYO MAANA UMEROPOKA SANA NA WALA HAUJUI UWEZO WANGU WA KIAKILI.
HIYO CHINA UNAYOISEMEA WW INA INVENTIONS ZAKE ZINATUMIKA WORLDWIDE.
HIYO CHINA UNAYOSEMEA WW VIFAA VYA UTENDEAJI KAZI VYA VIWANDANI USA ANANUNUA KWAKE.
HIYO CHINA UNAYOISEMEA WW INA RESERVES YA DOLLARS KUMSHINDA HUYO BEBERU.
HIYO CHINA UNAYOISEMEA WW NDIO PROCESSOR WAKUBWA WA HT IPHONE UNAYOTAMBA NAYO.
HALAFU NIKUWEKE SAWA KTK ISHU YA GOOGLE.
ILE ILIKUA NI MIONGONI MWA TRADE WAR KAT YA USA NA CHINA.
KMA ULIKUA HAUJUI USA ILIONEKANA KUUMIA NDIO MAANA GOOGLE WENYEWE WALIOMBA USA ITOE SANCTIONS KWA CHINA.
NA KM HAUJUI WACHINA WANATEST HARMONY S IKIKUBALI BEBERU WAKO AJIANDAE KULIA.
KWASABABU CHINA ANA CONTRIBUTE 60% OF MANUFACTURED GOODS DUNIANI.
ANATENGENEZA FAKE NA ORIGINAL PIA.
SIKATAI KUNA BAADHI YA TECH ANAIBA NA SIO KWA BEBERU TU HADI KWA MJAPAN HALAFU HAISHII HAPO ANAI MODIFY INAKUA BORA KULIKO ALIYOIIBA.
MATHALAN KTK BULLET TRAINS CHINA NDIYE MTENGENEZAJI BORA WA MAGLEV TRAINS KULIKO GERMANY MUHASISI.
KWAHIYO USIMCHUKULIE CHINA POA FUNGA BAKULI.
KUHUSU TECH ZA USA NINAMAANISHA KUWA TECH ZAKE NYINGI ANACHUKUA AMA ZINATOKA KWA WAHINDI,WAISRAEL,WAGERMANY.
HIVI HAUJIULIZI KWANN USA HUILINDA SANA ISRAEL?
NENDA KAKAE CHINI UTAFUTE CHANZO.
NA SASA HV BEBERU WAKO ANAPOROMOKA KISHENZI FUATILIA UCHUMI WA DUNIA UENDAVYO USIKAE KUJAZWA KASUMBA ZA MWAKA 47 HUKOOO.
TANZANIA NI NCHI AMBAYO IKIAMUA INAWEZA KUINUKA VZURI TU PASI NA KUMUOGOPA HUYO BEBERU KWASABABU KWAN HUYU BEBERU ANATUTAFUNA KMA ZIMWI KIUJANJA.
HALAFU FUATILIA UCHUMI WA NCHI YAKO PIA WAPI UMETOKA NA WAPI UNAKWENDA NA INAONEKANA HT MASUALA YA SYLLABUS HUYAJUI KUNGUNI WW.
HIVI SYLLABUS YA TZ NA USA ZINAFANANA?
KILICHOTUSHINDA SISI NI KUANDIKA MITAALA YA ELIMU KWA KISWAHILI TU LAKINI MITAALA MBONA IMEBADILISHIKA MARA KIBAO TU AU HAUNA MTOTO WW ANAYEENDA SHULE??
MWISHO NIKWAMBIE USIDHARAU MTU HUJUI UCHUMI WANGU UNAPOONGEA STICK TO THE TOPIC MWANAMAMA.
NA KM HUYO BEBERU WAKO USA AKILI NYINGI NGUVU KIDOGO KWANN TECH AZITOE NCHI ZINGINE KWANN WAZAWA WAKE WASIJENGE NCHI KWANN BOEING SHIRIKA ANALOTAMBA NALO LA NDEGE MWANZILISHI WAKE NI ASILI YA UJERUMANI WILHELM BOEING??
KWANN TECH NYINGI ANAZOTAMBA NAZO HAZINA ASILI YA WAZAWA WA MAREKANI?
NA KWANN TRADE WAR KATI YAKE NA MCHINA ANAFELI KM YEYE ANA AKILI NYINGI NA MCHINA ANAMNYOOSHA MBAYA MBOVU BEBERU WAKO NA BADO.
USIPENDE KUONGEA KWA KASUMBA NA DHARAU KUMBE UMEJAZWA VITU VYA MIAKA 47 HUKO.A
Tangu nchi yako ilipopata uhuru mwaka 1961 inakimbizana na matundu ya choo, uhaba wa madawati na maji mpaka sasa bado haijatatua. Sasa utaongea nini mbele ya beberu wakati vitu vidogo tu umeshindwa kuvimaliza kwenye nchi yako? Tangu mwaka 1961 unapokea misaada halafu na wewe unajiona mwamba kwa lipi?. Tatizo unaandika ujinga bila kufikiri. HAPO ULIPO UPO KWENYE KISIMU CHAKO CHA KICHINA UNAANDIKA HUU UJINGA. KAJAMBA NANI NAYE ANABISHANA NA MAREKANI. NA WEWE UNAJIONA MJANJA KUANDIKA HUU UJINGA KWA ID FEKI. KESHO NENDA KWENYE VYOMBO VYA HABARI UKAUSEME HUO UJINGA WA KUWAFUKUZA WAMEREKANI. HUYO KIONGOZI ALIYEKUMEZESHA HUO UJINGA ATAKUWEKA NDANI
 
Vipi huko North Korea,Iran na China mbona anakwama??
Mbona hadi leo kashindwa kumuondoa Bashar Al Assad huko Syria??
Ushavurugwa tayari mpaka unaanza kuniquote mara mbilimbili. North Korea na China kwasasa hawana lolote kwa Marekani. Kiduku mpaka anaenda kwenye mkutano na Trump hlalafu useme bado yupo imara kwa lipi?. Iran ni suala la muda. Sasa wewe kajamba nani unakimbizana na madawati unataka kuanzisha ligi na Marekani utamuweza?
Ukitaka kuanzisha ligi na Marekani unatakiwa uwe vizuri kwenye
1. UCHUMI
2. SILAHA
Ukiwa vizuri kwenye hizo sekta ndiyo uanze ligi na Marekani. Tofauti na hapo nenda kajifunze Fishing industry in Norway
 
Njia pekee ya wewe kama wewe kuonyesha juhudi zako zote kwa hali na mali na kwa nguvu zako zote ni wewe kujiunga ktk vikundi vyenu vya kiimani na kuelekea Syria kuendeleza mapambano uso kwa uso kumng'oa kwanza huko kwenye uwanja wa vita ndipo uje ktk vita baridi hapa home na tutakuunga mkono.
 
Ubavu huo mnao?

ebu kausheni,msituletee balaa wengine tukapigwa block

Tukaishia waona watoto wetu instagram
 
Back
Top Bottom