FT: Yanga SC 1-0 KMC | NBC Premier league | Benjamin Mkapa Stadium

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Karibuni katika mtanange huu wa kukata na shoka baina ya Yanga na Kmc utakaochezwa saa 1 jioni Estadio De Benjamin Mkapa.
.
Huu ni mchezo wa namba 69 wa Ligi Kuu ya NBC 2022/2023.
.
Yanga akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya Kmc.
.
Karibuni Wakuu.

=======

01' Mtanange umeanza Benjamin Mkapa.

05' Aziz Ki anaanchia mkwaju wa adhabu ndogo baada ya Tuisila Kisinda kuchezewa ndivyo sivyo, mlinda mlango anapangua.

12' Makambo anajaribu kupiga shuti la chini lakini linatoka pembeni ya lango.

23' Yanga na KMC wanacheza kwa zamu huku sehemu kubwa mpira ukiwa katikati ya uwanja.

32' KMC wanapata kona tatu mfululizo bila mafanikio ya bao.

35' Yanga wanapangilia mchezo kuelekea lango la KMC, mpira unamkuta Aziz Ki na anapiga fyongo, off target.

39' Boli linatembea kwa KMC, almanusra KMC watangulie lakini umaliziaji unagharimu.

42' KMC wanaendelea kufika kwenye lango la Yanga.

43' 🟡 Ambundo anapewa kadi ya njano.

44' KMC wameamka, almanusura Mateo aitangulize lakini mpira uliomshinda Diarra naye unampita.

45' Makambo anapiga kichwa na kinatoka pembeni kidogo ya lango la KMC.

45+2' Mpira unaenda mapumziko na milango bado migumu kwa pande zote.

=====

45' 🔁 Moloko anaingia kuchukua nafasi ya Kisinda.

45' 🔁Feisal anachukua nafasi ya Ambundo.

45' 🔁Bakari Mwamnyeto naye anaenda bench nafasi yake ikichukuliwa na Zawadi Mauya.

48' Feisal anajaribu shuti la mbali, off target.

54' Mlinda mlango wa KMC anafanya kazi ya ziada kulinda goli lake.

55' 🟡 Kelvin Kijiri analamba kadi ya njano.

56' 🟡Robert David, mlinda mlango wa KMC anapewa kadi ya njano.

59' 🟡 Bigirimana anapewa kadi ya njano.

62' Feisal anamsetia Aziz Ki, Aziz anaachia shuti anapaisha juu.

65' 🔁 Masoud anaingia Awesu.

66' 🔁Saliboko naye anaingia kuchukua nafasi ya Emmanuel upande wa KMC.

68' Moloko anapiga krosi kati lakini anakosekana mmaliziaji.

69' Mateo anabaki yeye na goli lakini anashindwa kutumia nafasi vyema na kupiga off target.

73' Makambooooo, anapiga kichwa maridadi, chuma cha goli kinamuokoa mlinda mlango.

75' Mateoooo, Diara anasimama imara kudaka shuti la Mateo.

76' Wanaendelea kushambuliana kwa zamu.

77' Bigirimana anaachia mkwaju unapaa juu ya lango.

77' 🔁 Denis Nkane anachukua nafasi ya Bigirimana.

79' ⚽ Feisaaaaal, anaitanguliza yanga kwa shuti la ndani ya 18. Yanga 1-0 KMC.

90+3' Kipenga kinapulizwa na Yanga inakusanya alama 3, mechi ya 44 kwa yanga kwenye ligi kuu bila kupoteza.
 
Come On Yangaaa
JamiiForums715621336.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibuni katika mtanange huu wa kukata na shoka baina ya Yanga na Kmc utakaochezwa saa 1 jioni Estadio De Benjamin Mkapa.
.
Huu ni mchezo wa namba 69 wa Ligi Kuu ya NBC 2022/2023.
.
Yanga akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya Kmc.
.
Karibuni Wakuu
Kwakuwa ninaishi ndani ya wilaya ya Kino, sina budi kuwa mzalendo leo
 
Back
Top Bottom