FT: Jwaneng Galaxy 0 - 0 Simba | CAFCL | Francistown Stadium | 02.12.2023

uran

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
7,580
10,817
1701464611181.png

Match Day
🏆CAF Champion League

⚽ Jwaneng Galaxy vs Simba
🏟️ Francistown Stadium
🗓️ 02.12.2023
⏰ 1600hours (EAT)

Kikosi cha Jwaneng' Galaxy kinachoanza.
20231202_151816.jpg


Kikosi cha Simba Kinachoanza
20231202_151507.jpg

All the Best Mnyama.

Updates...
Sasa ni Saa Tisa na Dakika 25 Alasiri.
Hali ya hewa ya Dar es Salaam ni ya joto kidogo, maeneo mengi yana mawingu ya hapa na Pale...

Zimebaki dakika 34' tu kipute hiki kianze.
Huko FrancisTown Stadium.

Saa 9:55 Alasiri, team ndio zinaingia Uwanjani sasa,
Uwanja unaonekana kuwa na mashabiki wachache sana.

Simba atacheza ugenini bila pressure ya Mashabiki...

10:00 jioni.
Mpira umeanza na Walionzisha ni Jwaneng'

Dakika 0' sekunde ya 55 Simba wanakosa goli la wazi hapa

Dakika 2'
Onana anapiga mpira unatoka nje inakuwa goli kick

Dakika 3'
Kibu anacheza faulu hapa.

Dakika 8'
Simba waapata faulu nje kidogo ya 18.
Inapigwa vizuri ,
Kipa wa Jwaneng' anaokoa

Dakika 9'
Jwaneng' wanakosa goli hapa

Dakika 10'
Jwaneng' wanapata kona ya kwanza.
Inapigwa lakini haileti madhara yoyote

Dakika 12'.
Tumeotea. (offside)

Dakika 13'
Ngoma anapiga shuti kali , linapaa juu inakuwa goal kick.

Dakika 16'
Jwaneng' wanapata faulu.
Inapigwa anadaka vizuri kipa wetu Ayubu

Kuna mzozo unatokea hapa.
Baleke amechezewa vibaya lakini refa anauchuna

Dakika 19'
Kipa wa Jwaneng' anafanyiwa matibabu .
Mpira umesimama kidogo

Dakika 21'
Simba tunachezea nafasi ya wazi hapa.
Mpira hautulii kabisa mguuni.

Wakati huo huo Kibu D yuko chini. kafanyiwa faulu

Dakika 24'
Tunakosa tena goli la wazi kabisa hapa

Dakika 26'
Jwaneng' wanapiga faulu ila inatoka nje inakuwa goal kick

Dakika 27'
Baleke anakosa tena hapa.
Huku Possession ikiwa ni Sisi 71%
Wao 29%

Dakika 29'
Saido anachezewa faulu inapigwa haileti mafanikio

Dakika 31'
Mpira umesimama kwa Dakika 1
Wanakunywa maji.
Joto ni kali.

Dakika 33'
Game On...
Simba tunahitaji utulivu kidogo tu hawa watu wanapigika

Dakika 34'
Baleke anakosa tena

Dakika 35'
Jwaneng' wanafanya shambulizi lakini halizai matunda.
Hawa jamaa ni wepesi sana

Dakika 37'
Inapigwa faulu kuelekea Simba.
Mohamed Hussein anaondosha
Jwaneng' wanapata kona ya Pili hapa
Inapigwa haizai

Dakika 39'
Game On..
Simba wanatawala mpira ugenini

Dakika 40'
Simba tunapata kona ya kwanza

Dakika 41'
Tunapata faulu eneo zuri sana.
Saidoo nyuma ya mpira.
Inpigwa kipa anadaka mpira

Dakika 43'
Mpira unarushwa kuelekea simba.
Anarusha moja kwa moja Ayubu anadaka

Dakika 44'
Jwaneng' anapata kadi ya njano kwa kujaribu kumdanganya refa.
Amejirusha makusudi kabisa ndani ya box

Dakika 45' +1
Tunapata faulu eneo zuri sana.
Anapiga Saidoo ila inaokolewa na Kipa wa Jwaneng'

Dakika 45' + 3
Kanoute anapigwa Yellow.

Mpira ni HT.

Dakika za kipindi cha kwanza zimetamatika hapa.

Bila bila...

Tukutane tena kipindi cha pili.

Updates...2nd Half.
Dakika 46'
Limetokea shambulizi kali upande wa Simba.
Inonga anapigwa Yellow.
Faulu inapigwa nje kidogo ya 18
Game on...

Dakika 48'
Inapigwa faulu inatoka nje.

Dakika 50'
Onana anapiga inatoka nje

Dakika 51'
Simba tunapata kona,
Inapigwa haizai matunda.

Dakika 55'
Game On...
Simba hatujawa na Muunganiko mzuri bado

Dakika 57'
Game On.
Simba wanamiliki mpira vizuri.
Onana anaonyesha udhaifu kidogo hapa

Dakika 59'
Zimbwe anapiga ila unatoka nje

Dakika 62'
Sub. Simba wanafanya hapa
Onana Out
Chama Inn
Kanoute Out
Mzamiru Inn...

Dakika 66'
Jwaneng' wanapiga kona yao hapa.
Haileti madhara yoyote kwa Simba.
Goal Kick

Dakika 68'
Jwaneng' wanapata kona nyingine hapa.
Inapigwa haileti madhara

Dakika 70'
Tunapata kona haileti faida yoyote

Dakika 71'
Kona nyingine inapigwa na Simba haileti madhara.
Saido anaunawa mpira.

Dakika 73'
Game On...
Simba wanautawala Mpira.
Ila mawasiliano sio mazuri.
Baleke amechoka.
Abadilishwe

Chama anashindwa kufanya maamuzi ya haraka, tunapoteza tena nafasi

Dakika 75'
Mpira umesimama kwa Dakika Moja kupoza joto kidogo.

Dakika 77'
Game On....
Bado hakuna m'babe hapa

Dakika 78'
Simba wanafanya Sub hapa.
Saido Out
Miquisonne Inn
Kibu D Out
Phiri Inn

Dakika 79'
Ngoma anacheza faulu na inapigwa inaishia kwenye mikono ya Ayubu.

Dakika 81'
Game On ila bado Simba wanamiliki mpira japo Muunganiko sio mzuri.
Linatokea shambulizi kwa Simba Ayubu anadaka mpira

Dakika 83'
Jwaneng' kama vile wanapoteza muda hivi.
Wameingia uoga. wanatafuta Suluhu

Baleke anabaki na Kipa ila anashindwa kabisa kufanya maamuzi.
Mguu wake unapata kigugumizi kikali

Dakika 86'
Baleke Offside

Dakika 88'
Mchezaji wa Jwaneng' yuko Chini hapa akipatiwa matibabu.
Ametolewa nje kwa matibabu zaidi, ila amenyanyuka ni ishara yakupoteza muda.

Dakika za Nyongeza ni 4'
Baada ya muda wa kawaida kumalizia.
Wakati huo huo
Inapigwa shuti ya moto kwa Jwaneng'.
Haizai matunda

Dakika 90'+2
Simba wanafanya mabadiliko
Israel Inn
Zimbwe Out...

Full Time.
Jwaneng' 0- 0 Simba.
Hakuna M'babe...

#Nguvumoja#...
 
Back
Top Bottom