From Zanzibar: Kura za Maoni Shwari!

From Zanzibar: Kura za Maoni Shwari!

CCM wanajificha maana hata mwangalizi hakuna ,lile kundi la akina Shamhuna ni kundi likijidai tu na wakijificha chini ya mwevuli wa CCM lakini hamna kitu walikuwa na malengo yao na si kuendesha nchi ,wamepigwa na chini ,hata huku Bara mnajua kuwa Zanzibar hakuna CCM.
Mwiba, hawa wanaowaliza nyinyi kila siku hapa kwenu Zanzibar ni kina nani kama sio CCM?,
Kama kweli Zanzibar hakuna CCM, waliopo madarakani ambao wataendelea na kuendelea na kuendelea ni kina nani?,
October hiyo inakuja, Maalim kashalabishwa asali, anasubiri kuchonga mzinga, na pia ameingia kwenye ule urembo wa mtego wa makamo wa kwanza, penye urembo ndio penye ulimbo, mkishanasa kwenye uliombo hiyo October, msianze kulioa lia ohh CCM hivi, CCM vile!.
 
Pasco, utulivu ulio kutana nao hautokani wapiga kura kujitokeza kwa uchache? nafikili kuna jumla ya watu laki nne waliojiandikisha kupiga kura leo. Je hawa wote wametimiza lengo la kipiga kura?

Kibunango, you are one of the people who amaze me by your diversity judging from your contributions!! Sasa mtu mwenye akili kama wewe kitu gani kinakuvutia kukaa na kushirikiana na wakina Makamba! Au NJAA?
 
Donge kura zishahesabiwa, Wilaya ya Kaskazini B nako tayari (huku wamepiga kura ya HAPANA) na ni maskani kwa Shamhuna... Kituo cha Mahonda kura za NDIYO ni 442, za HAPANA ni 467, 29 zimeharibika.
 
Kumbe kazi ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo inaweza kumalizwa ndani ya siku moja, iweje sasa kwenye uchaguzi mkuu "wanahesabu kura" wiki nzima?
 
Vituo vyote vishamaliza kuhesabu kura, majumuisho ndo yanasubiriwa.

Wasimamizi kwa asilimia kubwa walikuwa ni wanawake katika vituo vingi, kuna kituo ambapo kura za HAPANA zimekuwa 107 na NDIYO zikawa 87 zikaharibika 9 na kura hizo zikahesabiwa kwa dakika 15!
 
nataka hapana washinde! ili tuondoe kabisa ccm kote nchi nzima!, maana ndiyo wakishinda Maalim atakuwa na wakati mgumu! sasa huku Maalim kule Slaa,kazi ipo!
 
Mwiba, hawa wanaowaliza nyinyi kila siku hapa kwenu Zanzibar ni kina nani kama sio CCM?,
Kama kweli Zanzibar hakuna CCM, waliopo madarakani ambao wataendelea na kuendelea na kuendelea ni kina nani?

Pasco jaribu kumuelewa Mwiba. Inawezekana ana maana kuwa CCM hakuna Zanzibar na hao wanaowaliza ni ASP Masalia.WanaCCM wamekwenda kupiga kura ya ndiyo.
 
nataka hapana washinde! ili tuondoe kabisa ccm kote nchi nzima!, maana ndiyo wakishinda Maalim atakuwa na wakati mgumu! sasa huku Maalim kule Slaa,kazi ipo!
Kwa hesabu za haraka haraka NDIYO watashinda. Zanzibar inatawaliwa na sehemu mbili Pemba na Unguja, na mgawanyo wa wapiga kura ni angalau 50-50. Sasa ukianza kusikia unguja kuna mixed results basi jua Ndiyo imeshinda kwa kuwa Pemba kuna uhakika wa kura zote kuwa za Ndiyo.
 
Kumbe kazi ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo inaweza kumalizwa ndani ya siku moja, iweje sasa kwenye uchaguzi mkuu "wanahesabu kura" wiki nzima?

Strategy huwa ni kusubiri hamasa ipungue kabla ya kubinua meza ya kuhesabia kura. Ukitangaza haraka bila ya kujiandaa kwa vikosi vya usalama ni kwamba maandamano. Matokeo yatatangazwa haraka pale tu mshindi wa kweli anakuwa yupo upande wa CCM, kama hizi kura maoni ambazo zina baraka za CCM
 
Matokeo yanatangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Mhe. Mwinyichande.
Jimbo la Ukuu: 141 Haribika, 4978 Ndiyo Hapana 1622
 
Jimbo la Kiembe Samaki
Ndiyo 1668
Hapana 1086
Haribika 56
 
Jimbo la Dole
Ndiyo-2429
Hapana-2527
Haribika-145
Dole wamepiga Hapana!
 
Jimbo la Kikwajuni
Ndiy0 -3339
Hapana -2131
Haribika -99
Kikwajuni wamepiga kura ya ndiyo.
 
Jamaa wametangaza matokeo zaidi ni kesho saa 4:00 asubuhi.

Hapa ndipo ZEC inaponichosha kabisa!, kura zimamaliza kupigwa saa 10:00 jioni. By saa 11:00 wamemaliza kuhesabu kote, hapa katuletea majimbo matano tuu, mengine mpaka kesho saa 4 asubuhi, jamani this is a joke kama sio kichekesho!
 
Kwa hesabu za haraka haraka NDIYO watashinda. Zanzibar inatawaliwa na sehemu mbili Pemba na Unguja, na mgawanyo wa wapiga kura ni angalau 50-50. Sasa ukianza kusikia unguja kuna mixed results basi jua Ndiyo imeshinda kwa kuwa Pemba kuna uhakika wa kura zote kuwa za Ndiyo.

Luten;
kwa jinsi nijuavyo siasa za Pemba,sidhani kama jimbo la Mkanyageni hasa vijiji vinavyozunguka mitaa ya Chokocho,kule kwenye jimbo la Gando au hata baadhi ya majimbo ya Wete hasa kuzunguka mji wa Chakechake wanaweza wakakubali "NDIYO" kwenye kura hii hasa kipengele cha kumpa aliyeshindwa uongozi ndani ya serikali ya ZNZ,kule bado wana amini kuwa ni CCM tu ndiyo inapaswa kuongoza na hata wabunge na wawakilishi wa CUF huwa kura hazipishani kihivyo!

Tutegemee pia kura za"HAPANA"kutoka katika majimbo baadhi kule Pemba ndugu yangu Luten!
 
Samahani wakuu zangu nimeingia katikati pasipo kufuatilia mwanzo wa hizi kura za maoni..Ningependa kujua NDIYO inasimamia nini na HAPANA inasimamia nini..
 
Malafyale unguja kwenye ngome ya CCM ambao wengi wake walikuwa wanapinga lakini matokeo hadi sasa NDIYO inaongoza itakuwa Pemba kwenye ngome ya CUF ambayo wengi wanaunga mkono. Ni hesabu ndogo sana hiyo kujua what will happen but tomorrow is just around the corner Wait and See.
 
Samahani wakuu zangu nimeingia katikati pasipo kufuatilia mwanzo wa hizi kura za maoni..Ningependa kujua NDIYO inasimamia nini na HAPANA inasimamia nini..
NDIYO kukubali serikali ya mseto Zanzibar na
HAPANA kupinga serikali ya mseto
 
Back
Top Bottom