GE2025 CCM: Kuongoza Kura za Maoni haimaanishi umeteuliwa

GE2025 CCM: Kuongoza Kura za Maoni haimaanishi umeteuliwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,217
Reaction score
3,796
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo kimehitimisha zoezi la kura za maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea wa nafasi ya Ubunge katika majimbo ya Ubungo na Kibamba, huku Prof. Kitila Alexander Mkumbo na Anjellah Kairuki wakiibuka vinara wa kinyang’anyiro hicho

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo, Henry Mwenge amesema kuwa wakazi wa wilaya hiyo wameonesha ukomavu wa kidemokrasia kwa kushiriki zoezi hilo kwa amani na utulivu, huku akisisitiza kuwa matokeo hayo ni maoni ya wanachama tu, si ushindi wa moja kwa moja kwani “vikao vya juu vya chama vitakutana ili kujiridhisha”

Katika Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo ameongoza kwa kura 3,613 kati ya kura halali 4,992, akionesha kuwa bado ana uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wanachama wa chama hicho. Kitila, ambaye amemaliza muda wake kama Mbunge wa Ubungo, anatazamwa kwa jicho la matumaini na wengi wanaomshabikia kuendelea na kazi ya uwakilishi bungeni

Kwa upande wa Jimbo la Kibamba, Anjellah Kairuki ameibuka kidedea kwa kupata kura 4,655 na hivyo kumuweka katika nafasi nzuri ya kupitishwa kuwania tena kiti hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025




Chanzo: Jambo TV​
 
Naam, si jambo geni
 
Uchaguzi huu wa 2025 ni rahisi zaidi kuonesha madhaifu ya CCM kuliko ya upinzani. Hivyo wateule wa CCM wasidhani wameshavuka
 
CCM wanaleta mambo gani tena, kama wamechuja na kuleta majina machache ya kupigiwa kura kwanini wakatae kupitisha aliyeongoza?
 
Back
Top Bottom