From Madame B to Mung Chris...

From Madame B to Mung Chris...

Kwako Mung Chris kipenzi cha moyo wangu na tiba ya maradhi yangu sugu.
Ni siku, wiki, na hatimaye imetimu miezi mitatu tangu tuanze safari ya penzi letu tamu na lisilochuja hapa duniani tulilolianzisha hapa Jamii forums tarehe kama ya leo.
Na pia nakumbuka jinsi tulivyosumbuana hapa Jamii Forums kule Pm kila siku.
Usijali....(ile ilikuwa mitego yangu kukupima kiasi cha upendo wangu kwako).

Hakika sikutaraji kama nitaweza kupata mwenza wa kuweza kunituliza na kufanya niweze kuwa kiumbe kipya katika safari hii ya penzi tamu.

Sijutii kukupenda
Sijutii uamuzi wangu
Sijutii kuchaguliwa na wewe
Sijutii vile binadamu wanasema nini kunihusu mimi au wewe.
Ila kwangu utabaki kuwa mpenzi na baba bora wa mtoto wetu mtarajiwa.

Natamani nimalize hii ng'we salama ili niweze kupakata katoto kako kalikochanganya damu ya Kisambaa na Kichaga.
Nakupenda leo
Nitakupenda kesho na
Nitakupenda milele daima.
Labda mmoja wetu afariki.

Kila mmoja ana mapungufu yake, hakuna aliyekamilika kwa 100%
Kama kuna sehemu naendelea kukukosea naomba uwe muwazi na uniambie ukweli.
Hatuhitaji kuishia njiani.

Asante kaka mkuu Maxence Melo kwa kuanzisha mtandao huu kwani kwa namna moja ama nyingine imechangia mimi kumpata mwenza wangu Mung Chris.

Pia natoa rai kwa wale tuliokuwa tunasumbuana Pm,
Nimetwaliwa....natawaliwa.
Nagharamiwa sasa hv.

Ila baba Mung Chris punguza wivu, wabantu wa mizigo ndio asili yetu.
Utagombana na wangapi baba?
Cha muhimu ni kutunza heshima ya penzi na pendo letu.
Ila nami itabidi nipunguze manjonjo....kha!!!!

Nakupenda sana.
Can't wait kuvaa ring...
Soon najua inakuja.
I love you, no matter how and what!!!
Madame B.
2018
Hongera sana mdogowangu Madame B
Mung Chris ni kaka mzuri - VERIFIED!
Karibuni chamani wapendwa
Mniletee kadi Pm au whatsapp nitawachangia michango yote
Nikiwepo Tz nitahudhuria kama nitaalikwa!
I wish u all nothing but the best
LOVE IS A GOOD THING - Muhimu ni Kuvumiliana
PS:
Kitchen Party Kungwi nakuletea bure ukitaka!

Mmebakia Smart911 na wifi mahondaw nasubiri KADI ABI!?
Honey Njoo tuwachangie wapendwa wetu 50thebe
 
Asante sana Extrovert.
Usijali, tumeshajuana na tunafit kila mahala.
Kwahilo sitawaangusha watu wa humu.

Asante sana na hutasikia lolote baya toka kwetu.
Ntafurahi sana mambo yakiwa mazuri always. Nawaombea wepesi katika safari yenu zingatia sana kutumia neno samahani na asante katika siku zote za maisha yenu bila kusahau kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika nyakati zote.
 
Ntafurahi sana mambo yakiwa mazuri always. Nawaombea wepesi katika safari yenu zingatia sana kutumia neno samahani na asante katika siku zote za maisha yenu bila kusahau kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika nyakati zote.
Usijali.
Mambo yataenda mazuri na wala hutasikia lolote baya na la kukweza juu yetu.

Asante tena na tena.
Naahidi kutimiza yote uliyosema.
 
Hongera sana mdogowangu Madame B
Mung Chris ni kaka mzuri - VERIFIED!
Karibuni chamani wapendwa
Mniletee kadi Pm au whatsapp nitawachangia michango yote
Nikiwepo Tz nitahudhuria kama nitaalikwa!
I wish u all nothing but the best
LOVE IS A GOOD THING - Muhimu ni Kuvumiliana
PS:
Kitchen Party Kungwi nakuletea bure ukitaka!

Mmebakia Smart911 na wifi mahondaw nasubiri KADI ABI!?
Honey Njoo tuwachangie wapendwa wetu 50thebe
Hahahahah
Usijali mwayaaaaa Money Penny....hapa penzi ni miaka laki na usheee.
Hakuna wa kututenganisha katu.
Na hatotokea nakuapia kwa hilo.

Kadi tutakupa, muhimu afya na uzima uwepo.
Asante kwa kutukaribisha chamani.
Hatutawaangushaaa
 
Mie kitasa, yeye ufunguo.
Kitasa kimepata ufunguo.

Asante shost mwaya.
Maana kwa hali ile kumpata wa kunivumilia makasheshe yangu hapa jukwaani isingewezekena.
Ila jamaa ndo kajitosa mzimamzima na maisha yanasonga kabisa.

Asante kipenzi.
Wewe nitakuweka kamati ya michango ya harusi pale January.
Sasa kwakua umepata kiboko yako haunifundishi tena ile kitu nami nimnogeshe shemeji ako?
 
Sasa kwakua umepata kiboko yako haunifundishi tena ile kitu nami nimnogeshe shemeji ako?
Hahahhhahah
Huyu hatumii.
Naweza kukupa tekniki kumbe ajae hataki.

Ila nitakuja kukufundisha kwa ajili ya akiba ya yeyote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom