Ninamfahamu Richard na kumuheshimu kama mwandishi mwenye juhudi, nimesoma baadhi ya maandishi yake na huwa napenda msimamo wake sio mtu wa kuburuzwa. Nampongeza kwa juhudu zake za kufika huko alikoenda. Lakini naona article hii ameitoa wakati ikiwa bado haijaiva, yaani ni hadithi ya safari yake ya Goma badala ya habari ya kuboresha kile kinachozungumzwa. Mimi kama mwl, tena wa creative writing, hii habari inakosa majibu mengi tu, kwa mfano, nini hasa alichokua anaki investigate? na nini source yake ya verification maana haiwezi kuwa report za mazungumzo yake na M23 as if ndio the gospel truth. Halafu nafikiri kilichosemwa kingeweza kufanyika kwa nusu ya kurasa zilizotumika, of course hii kazi ilitakiwa iwe edited, sema kwa kuwa shirika lake halina magwiji, nafikiri waandishi mahiri wa lugha hii kama Jenerali Ulimwengu, Atilio Tagalile na Hilal Sued wangepewa kui polish, japo wangemrudisha field, lakini angetoka na kiboko ya kazi, nawashauri pia waandishi hawa wasiogope kuwatumia wasomi wenzao kusomeana kazi, mimi watu hawa wamenisaidia sana kuboresha kazi zangu za kizungu, maana ni wataalamu wa hasa, Kazi tofauti Richard big up