Friends with benefit, nimepewa masharti magumu

Friends with benefit, nimepewa masharti magumu

Kama unakufahamu home kwake fanya hima nenda na ikiwezekana muende na mumeo ukaombe msamaha coz tayari anajua mahusiano yenu yakoje then baada ya hapo move on. EPUKA KUUMIZA MOYO WA MTU.
 
nina mume na kaniambia nilikuonya hukunisikia, yamekukuta.
kuna kipindi ilitokea hivyo kwangu bt mme wangu nilipomhadithia hakuniamini akafanya utafiti kwa mda wake akaja gundua hakukua na kinachoendelea, na akanionya si kila mtu ataweza elewa

Nimependa sana kama mumeo naye alikuwa anatambua uhusiano wako na huyo rafki yako, Chakufanya apo huyohuyo mumeo muombe akusaidie kwa huyo mke wa friend wako atamuelewa.vema kuliko ww uende kumueleza mwenyewe
 
yaani kama ungekua hekima kidogo ulipoambiwa na mkewe kuwa "anatamani mumewe ampende kama anavyokupenda wewe" ungekata mawasiliano. Ila hukuona shida? unacheza na mume wa mtu!? halafu hujielewi wewe mwenyewe unampenda sema tu hujajigundua!
 
Sorry but wewe ni mpumbavu sana....marriage is a relationship between wife and husband, you have destroyed that relationship kisha eti unahitaji psychologist wa kukushauri.....you are only alive because it is illegal to kill you.

no need to be hostile
 
Mume wangu kuwa na rafiki wa kike hiyo hapana tena hadi anitambulishe thubutuuuu huyo mwanammke ana moyo kweli........ ila nawe weka mipaka ujue huyo friend ni mume mtu usisahau
 
Iachie time tu...muda ukipita atarudi kwenye orijino position. Ila ku fasti traki hio hali inabidi wewe usifanye mawasiliano na huyo called friend with benefit
 
Wewe Suprise ni Mwanamke Mpumbavu (am sorry kwa kusema hivyo) huyo unayemuita mumeo mchunguze vizuri kama hana michepuko basi huenda siyo rizki. Hakuna mwanaume asiyekuwa na wivu kwa mkewe anayechati ujinga na mume wa mtu mwingine. Ungekuwa mke wangu ningekusambaratisha kabisa. Anyway kaa mbali na ndoa za wenzako msamaha hauna maana waachie maisha yao ganga maisha yako period!
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana anamegwa na inawezekana hamegwi pia!!!
Ni ngumu sana kuipima ila kwa mazoea ya wengi hapa kuna au kumegana moja kwa moja au ilitokea na kwa sababu fulani wakaacha na sasa ni marafiki ila nani yuko tayari kuonja sumu kwa kulamba???!!!

Umehaeibu we piga kimya acha mawasiliano waachie wenyewe huyo friend wako atabeba msalaba wake.
Mumeo atakuwa ---- sana kama ataenda kukuombea msamaha!!!
 
I wouldn't wanna lose my male friends under any circumstances. But if their relationships are affected I would back off.
 
pole suprise kwa yaliyokukuta. watu mnamponda suprise akati hiyo ni hali ya kawaida, huyo bidada ana hisia negative sana kwa mmewe au hamwamini mumewe? kama wewe suprise umeshamweleza ukweli na hakuelewi...baasi achana nae waache na mumewe we endelea na maisha yako, kama ni marafiki mbona wapo wengine sio lazima uwe nae huyo na kuendelea kusababisha wasiwasi usio na maana, waachie ndoa yao hiyo waendelee na maisha yao.
 
dah....yani kila mtu amekulaumu,kwa jinsi ulivyoharibu,kiukweli hata ukiipeleka popote hakuna atakaekuelew kuwa ulikuwa na nia nzur,cha msingi tulia,kwanza,take time,uone upepo ukoje,ukipata chance omba radhi na ahidi kufuta namba,na kutowasiliana tena na mume ya watu,tena ubadili line na ukomee,haipendezi!!
 
Natamani niachane na hawa watu ila kiukweli nashindwa, nahitaji ushauri hasa wa mwana saikolojia aliyebobea, sipendi kuumiza wanawake wenzangu lakini hawanielewi,nami siwalaumu nakiri nakosea kwa sababu mume anauma jamani.

Ni hivi sijui hata nianzie wapi ila nahisi nimemuumiza mwanamke mwenzangu kwa hisia .nasema kwa hisia sababu cjafanya kila anachonihisi nimefanya kwa mmewe sema tu ushahidi haujatosha kua upande wangu.

Nimezoea kuwaita frends with benefit, sasa mmoja wa hao friends zangu ameoa, nimezoeana nae kupita kiasi inshort i feel happy being with him(naomba niweke kwenye mabano sijashiriki nae since nijuane nae coz hicho hakijasababisha urafiki wetu, tunasaidiana sana naweza sema ananisaidia kuliko mimi nimsaidiavyo, ananipa kampani ya kutosha kila mazingira yakiruhusu.

Kiukweli ni rafiki yangu ambaye yupo moyoni naweza sema .

Last wiki katika kuchat akatuma message, nimekumis mpenzi wangu nowadays majukum ya familia yanatubana ila tujitahidi tukipata nafasi tuonane. Utaniambia mda wako.on ma way home.

mkewe anafaham uwepo wangu kama rafiki wa mmewe bt i wonder y imemuumiza kipindi hiki amemwambia mme wake basi awe anakuja kwangu daily kwake basia ye atatafuta atakayemthamini.

Niwarudishe nyuma kuna kipindi alinipigia simu akaniambia dada natamani mme wangu angenipenda kama anavyokupenda wewe, kiukweli naumia natamani anielewe uhusiano wangu na mmewe ukoje ila pia upande wa pili nahisi ni mkosaji.


Sasa ugomvi kwao umekua siku ya tano sasa, mme wake kaniomba nifanye juu chini nimtafute mkewe nimwambie juu ya hilo atusamehe. Nimeamua kumfuta huyu frend with benefit kichwani mwangu ingawa pia itanichukua mda kukubaliana na ukweli.


Naomba mawazo nifanyaje bi dada aweze kutusamehe na kurudisha moyo kwa mmewe.
friends with benefit maana take ni marafiki ambao wanasaidiana kimwili as in sex ila hawana feelings zozote baina yao
 
duhh u have sinned mdada fanya kumtafuta afu uongee nae openly anamoyo na binadamu tumeumbiwa kusamehe pia huenda akakuskia.licha ya ni mwanamke mwenzio jitahidi atakuelewa
 
dada,tafuta wako uwe nae benet,achana na mume wa mtu,unajua ana mke na unajua wanaume ni dhaifu kiasi gani,usiharibu mahusiano ya watu ndani,laana itakua juu yako,acha kabisa,eti ushauri,mhhh
 
Tafuta wa kwako achana na Mme wa MTU!
 
Back
Top Bottom