Freemason wanywa damu ya gadafi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Freemason wanywa damu ya gadafi

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Aug 10, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  FREEMASONS ni jamii ya siri (secret society) inayotisha duniani, njama zao za kuitawala dunia ifikapo Desemba 2012 ni tisa, kumi ni unyama wa kutisha waliomfanyia aliyekuwa Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi.

  Memba wa Freemasons hususan wale
  wanaomuabudu Shetani, Lucifer (Jini Mkuu), wanadaiwa kumchana Gaddafi kifuani, wakaikinga damu yake na kuihifadhi kwenye glasi kabla ya kuitumia katika kafara nzito.

  Mtandao mmoja wa kidini umeandika kuwa damu ya Gaddafi, ilichanganywa na ya mbuzi aliyechinjwa ili kutolewa kafara katika kuadhimisha kukamatwa, kuteswa na hatimaye kuuawa kwa Gaddafi.

  Katika habari hiyo, ilielezwa kuwa Freemasons walichukua kiasi kidogo cha damu ya Gaddafi na kuimimina kwenye ile ya mbuzi ambayo ndiyo ilikuwa nyingi na kuhifadhiwa kwenye chombo kimoja.
  [​IMG]
  Habari zinafafanua kwamba baadhi ya Freemasons walikunywa, wengine walilamba na kunawa katika kusherehekea kuingiza mizizi yao ndani ya nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta (Libya).

  Hata hivyo, kati ya wafuasi waliohudhuria kafara hiyo ni idadi ndogo mno waliokunywa damu ya Gaddafi iliyochanganywa na ya mbuzi, kwani wengi walilamba na kunawa, ikiwa ni ishara ya kutambua utukufu wa kiongozi wao, Lucifer.
  [​IMG]
  "Damu iliwekwa kwenye glasi, aliyetaka kunywa, alimimina kidogo kwenye glasi ya peke yake, waliolamba waliingiza vidole na kulamba kisha wakanawa," uliandika mtandao huo.

  Kwa mujibu wa mitandao inayochambua mambo ya Freemasons, jamii hiyo ya siri hupenda damu ndiyo maana maadhimisho yao husindikizwa na kafara ya kuchinja wanyama hususan mbuzi.
  [​IMG]
  Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye ni mnajimu mwenye utaalamu mkubwa wa falsafa za Freemasons, naye alilithibitishia gazeti hili kuwa jamii hiyo hupenda damu kwa sababu humfurahisha kiongozi wao mkuu, Lucifer.

  "Kuchinja na kuona damu kuna maana kubwa mno kwa Freemasons, wanapenda sana damu," alisema Maalim Hassan.
  [​IMG]
  NJAMA NI ILE ILE
  Inaelezwa kuwa Freemasons ipo kwenye mkakati thabiti wa kuitawala dunia kabla ya Desemba 2012, hivyo imekuwa ikiratibu sera zake kwa kuangusha tawala za nchi mbalimbali ambazo viongozi wake wameshindwa kuendana na matakwa yake kama ilivyokuwa kwa Gaddafi.

  Maalim Hassan aliliambia Uwazi: "Freemasons inapambana kutwaa mamlaka ya nchi tajiri kama Libya, inawaondosha viongozi ambao hawaendani na matakwa yao. Shabaha ya Freemasons pia ni kupambana na Uislam pamoja na Ukristo.
  [​IMG]
  "Ipo wazi kuwa lengo lao ni kuitawala dunia, kwa hiyo wanasimamia kuona hilo linawezekana kwa kuhakikisha Uislam na Ukristo unaishiwa nguvu na Shetani anashinda hapa duniani," alisema Maalim Hassan ambaye ni mrithi wa kazi za marehemu Sheikh Yahya.

  Aliongeza: "Mkakati mkubwa zaidi ni kuhakikisha dunia inaabudu Dini ya Shetani, wanataka kila mtu awe chini ya mamlaka ya Jini Mkuu, Lucifer. Dunia nzima itawaliwe na serikali moja na iwe na sarafu moja."
  [​IMG]
  AFRIKA MASHARIKI YACHIMBWA
  Kuangushwa kwa Gaddafi siyo suala la mzaha kwa Afrika, kwani inadaiwa kuwa Freemasons kupitia Jeshi la Kujihami la Nchi za Magharibi (Nato), inatekeleza sera zake kwa vitendo kwa nchi ambazo viongozi wake wameshindwa kukidhi matakwa yao.

  Inaelezwa kuwa Freemasons hawapendi nchi kuungana na kubainisha kuwa ndiyo maana wameanza kuichimba Jumuiya ya Afrika Mashariki na ili kuidhoofisha, wameingiza agizo la kukubali ndoa za jinsi moja.
  [​IMG]
  Habari zinasema kuwa Serikali ya Uingereza imekuwa ya kwanza kutumiwa na Freemasons katika kuhakikisha nchi zote zinazounda Jumuiya ya Madola zinapitisha sheria zinazokinzana na maandiko matakatifu yanayoaminiwa na waumini wa Dini za Kiislam na Kikristo.

  Imeelezwa kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki nguzo yake ni Tanzania, Kenya na Uganda ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola, hivyo agizo la ndoa za jinsi moja lengo lake ni kuzigawa kati ya zile zitakazokubali na zitakazokataa ili mwisho wake ziwe na mfarakano.
  [​IMG]
  Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (Saut), Profesa Mwesiga Baregu, alizungumza kupitia runinga moja hivi karibuni kuwa anguko la Gaddafi Libya ni ishara mbaya kwa vyama vikongwe kama Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Alisema, nchi za magharibi hazipendi kuona vyama vikongwe vikishika madaraka kwa muda mrefu, kama ilivyo kwa CCM ambacho kinaongoza nchi tangu uhuru (Tanganyika mwaka 1961, Zanzibar 1964), kikiwa ni mtoto aliyezaliwa baada ya Tanu na ASP kuungana.
  [​IMG]
  Angalizo hilo la Baregu, linatishia pia amani ya utawala wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na chama chake cha National Resistance Movement (NRM), kwani yupo madarakani kwa miaka 25 sasa (alianza kutawala Januari 26, 1986).

  Rais wa Kenya, Mwai Kibaki na chama chake cha People National Unit (PNU) ndiyo anapona kwenye angalizo hilo, kwani kuna mabadiliko makubwa ya vyama tawala nchini kwake, katika mihula miwili kati ya mwaka 2002 na 2012, tayari vimeshaongoza viwili. (Mwaka 2002 hadi 2007, chama tawala kilikuwa Narc).

  VITA YA IMANI
  Maandiko yanasema kuwa nyakati za mwisho kutakuwa na tishio la dunia kutawaliwa na Dini ya Shetani ambapo zama hizo zikifika kutakuwa na mfumo utakaozuia mtu yeyote kupata huduma za kijamii mpaka awe mwanachama na atatambulika kwa chapa 666.
  [​IMG]
  Habari zaidi zinaeleza kuwa Freemasons wanatumia njia mbalimbali kuhakikisha ulimwengu mzima hakuna anayeamini dini za Mungu na wanapambana kuhakikisha hata Yesu (Nabii Isa) atakaporejea akute hakuna aliye tayari kukombolewa.

  Katika kuhakikisha wanapambana na nguvu ya Yesu, Freemasons wamekuwa wakitumia damu ndiyo maana hutoa kafara kwa kuchinja wanyama hasa mbuzi au kondoo wenye pembe zinazotengeneza alama ya V kwa imani kwamba huwaongezea nguvu ya kuishika dunia.

  juma: FREEMASON WANYWA DAMU YA GADAFI
   

  Attached Files:

 2. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  duh....kama ndio hivyo tumekwisha sasa
   
 3. Wazo Langu

  Wazo Langu JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 1,344
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 280
  Kuitajataja Frimasoni ndio tunaipandisha chati.
  Natamani kila mtu alisahahu hilo neno jamani maana hadi watoto wadogo wanalijua
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mambo ya kawaida tu usiogope Muogope Mwenyeezi Mungu FreeMason hawawezi kumshinda Mwenyeezi Mungu wa pekee ndio wa kumuogopa mkuu Boflo
   
 5. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Mkuu una shida gani na Freemason??

  waliomuua Gaddafi si watu wake mwenyewe na ilikua live pictures?? maana una kama threads zaidi ya tano unahangaika nao

  wamekuchukulia mke?
   
 6. Davie S.M

  Davie S.M JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ni Upuuuzi ...

  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
 7. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Je na Gaddafi alikunywa damu yao? Maana mie sikuelewi elewi unachomaanisha. Hizi habari za Freemason waachie akina Shingongo na njaa na ujuha wao wawaibie majuha wenzao. JF siyo saizi ya habari kama hizi ambazo ni vigumu kuzithibitisha hasa ikizingatiwa kuwa glasi iliyowekwa hapa ni ya mvinyo. Hata mimi ningeipata ningeinywa mradi isiwe damu ya Gaddafi mbuzi wala binadamu mwingine. Muacheni Gaddafi apotee huko jangwani walipomtupa mwenda zake. Au unamaanisha Freemason ni walibya wote waliomsulubu Gaddafi baada ya kuwasulubu muda mrefu? Kama hao basi sawa maana naye alikunywa damu yao kwa miaka zaidi ya arobaini.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Sarkozy na Gaddafi wakisalimiana kwa ishara za Freemason. Mkuu Father of All
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wanga kwetu Tanzania kila siku wanakunywa damu na wanakula nyama za watu. Au hujui hilo?
   
 10. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  the dry root has lost it compeletety

  sijui nani anamuwasha... huko nyuma hakua hivyo
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Ina maana uboflo unaletwa na hawa jamaa kumbe?
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  tatizo ni namna ya kuthibitisha kama kweli hayo yanafanyika. Wengine hatuamini katika hayo...
   
 13. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,111
  Likes Received: 10,468
  Trophy Points: 280
  Nimeshindwa hata kucomment... mtu ambaye anapoteza muda wake kuongelea freemason huwa namuona kama hana akili timamu..
   
 14. Mourinho

  Mourinho JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Guys freemasonly ni secret brotherhood, being secretly ndio essence ya existance yao.Kutokana na maendeleo ya teknolojia cku hiz hadi vitabu vyao vipo kwenye mitandao BUT agenda zao na mipango yao ni siri kubwa hata young masons wa degree tatu kama kina Jay Z hawazijui na information zozote zinazotoka nje mpaka mbongo kama wewe unazpata zina aim ya kumislead(conseal) na sio kureveal. You hv been fooled kama unaamin kwamba 12/12/2012 ndio wataestablish new world order. Wanachoplan mimi na wewe hatujui and probably we wont its only few "illuminated ones" wanaojua wat wil happen and when and believe it o not hakuna istitution which is safe from the illuminati including religion!
   
 15. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  au wanamtaka yeye mwenyewe. fremason fremason atuache bana kama yeye sio si ahubiri yake kama ana dini safi? na atende kwa kadiri ya dini na mafundisho sio kukalia kututajataja hapa
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ana mahangaiko tu na dunia yake mwenyewe anayoitia najisi
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Asiyeamini anabaki na kuwa haamini na aneamini anabaki kuwa anaamini, ndio binaadam tulivyo.

  Kama hizi habari za kupikwa kipikwa, eti freemason wanakunywa damu ya Gaddafi, ni kitu haiingii akilini. Ili iweje?

  Ma photoshop yanatumika na vijana wanapoteza muda kuyaungaunga hayo mambo, yote ni ukosefu wa kazi za kufanya, hawa vijana wanayoleta na kushadidia haya wanaonesha wako idle muda mrefu na wanakosa ubunifu ndio matokeo yake nyuzi kama hii.
   
 18. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Believe this you'll believe anything!
   
 19. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mbona maelezo yanaendana na muslim brotherhood zaidi kuliko freemanson? ingawaje mimi sikubali uwepo wa freemanson ambayo kwa maoni yangu mimi binafsi ni uzushi tu na upuuzi wa watu wenye itikadi danganyifu, lakini kwa uhakika na bila ubishi walioziangusha serkali za libya, egypt, tunisia, mali na wale wanaotafuta kuiondoa serkali ya syria madarakani wote ni muslim brotherhood! hawa ndo wenye katiba yenye azimio la kuitawala dunia nzima under one global caliphate. Yawezekana mtoa hoja hajui chochote kuhusu muslim brotherhood au anajua lakini anafanya propaganda kuhadaa watu ili wasije wakazishtukie mbinu za muslim brotherhood zinaendelea hapa tanzania na kwingineko duniani kote.
   
 20. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #20
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbuzi Mzee jiandae, zamu yako yaja.
   
Loading...