Freeman Mbowe: Nawaletea Katibu Mkuu Makini

Freeman Mbowe: Nawaletea Katibu Mkuu Makini

viongozi wa chadema mtakuwa mmebugi sana kuchagua huyu jamaa. tunajua hili litakuwa chaguo la Lowasa tuu. kweli sasa tutaamini chama kimeuzwa.haiwezekank ccm walewale waongoze upinzani. over our dead body
Huna akili kwa 100% nini maana ya upinzani?
 
Mkuu ndani ya ccm hakuna kitu kinaitwa aibu

Lakini kweli hawa jamaa hawana mshipa wa aibu. Maana hata suala la Uchaguzi wa meya Dar wanataka kutuibia kama vile teja anavyoiba mchana akidhani haonekani.
 
Lakini kweli hawa jamaa hawana mshipa wa aibu. Maana hata suala la Uchaguzi wa meya Dar wanataka kutuibia kama vile teja anavyoiba mchana akidhani haonekani.
Mkuu wa meya wa dsm hapo ccm wamesanda,hawapati chochote maana namba haina longolongo wala haiitaji kupekuwa kwenye dictionary
 
Mkuu wa meya wa dsm hapo ccm wamesanda,hawapati chochote maana namba haina longolongo wala haiitaji kupekuwa kwenye dictionary[/
QUOTE]

Teh teh teh. Muhimu ni kwamba Ukawa wanatakiwa kuwa makini sana. Maana hawa jamaa wanawakamata kamata wabunge na madiwa na kesi za kubambika.

Wanaweza wakatimia hii kama mbinu ya kuwapunguzia Ukawa idadi.
 
Mlikuwa mnaiga eeh mimi sio mfuasi wa siasa chafu nabishana kwa hoja hamuwezi kuwa mnafuata mkumbo wakisema mkeo mzinifu nawe unasema ndio! Wakisema tulikuwa tunatania nawe unakubali pia!!! Huo ni utoto
Nyie mlioiga mpaka magwanda ya Makamanda mkifikiri na nyie mtaitwa makananda lakini jina lenu limebaki pale pale magamba full
 
Demokrasia iko wapi? Kwanini mbowe ndio ateue mtu, na kuna wa kumpinga kweli? Kwanini wasiachie wanachama wajitose kugombea na wapigiwe kura. Atachagua mchaga na wachaga wote cdm watamkubali bila tabu yeyote.
Tunafuata katiba siyo mtu
 
Kwa taarifa nilizonazo za uwakika ni kwamba aliyekuwa mbunge wa Kahama James Lembeli ndio katibu Mkuu mtarajiwa. Kwa hili naomba niwapongeze watani zangu kwa kupata jembe.

Kwa hakika James Lembeli ana uwezo kama Dr. Salaa na pengine ana uwezo mkubwa kuliko Dr. Slaa....
Nita kuwa tomaso Katika hili kwani mkuu una PHD ya uongo uli ahidi umma wa watanzania hapa hapa JF kuwa muitaliano ata fanya press jumatatu tarehe 07/03/2016 mpaka muda huu hatuja wahi kumsikia na wala wewe hujawahi kukabusha?kwa kifupi wewe ni muongo wala Habari yako haina Sifa ya kujadiliwa hapa JF
 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amevunja ukimya na kusema atawasilisha jina makini la mrithi wa nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa jana, baada ya kumalizika kikao cha kwanza cha Kamati Kuu, Mbowe alisema sifa za kiongozi anayepaswa kushika wadhifa huo zinafahamika.

Alisema wajumbe na wanachama wa Chadema watarajie kumpokea mtu makini ambaye jina lake atalipendekeza kisha kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza Kuu kesho.
“Sifa za Katibu Mkuu zinajulikana, nawaomba wanachama na wajumbe kutulia, jina watakutana nalo ukumbuni muda ukifika… nina imani litakuwa jina la mtu makini,” alisema.

Mbowe alisema chama hicho kinakutana kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka jana, hivyo wana mambo mengi ya kujadili, ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati mipya ya kuwafikia wafuasi wao.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimesema kitamtambulisha Katibu Mkuu mpya rasmi Jumapili wakati wa mkutano wa hadhara utakaofanyika viwanja wa Furahisha jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene, alisema majina mawili yatawasilishwa katika Baraza Kuu litakalokaa usiku wa Jumamosi kwa ajili ya kupitisha jina moja.

Alisema majina yatakayowasilishwa hayatakuwa na uhusiano au urafiki wowote na Mwenyekiti Mbowe.

“Tayari viongozi wa kitaifa wamewasili Mwanza, Sekretarieti imekutana kwa ajili ya kuandaa ajenda ambazo zitajadiliwa na Kamati Kuu yenye wajumbe 36.

“Siku inayofuata Baraza Kuu litakaa usiku kwa ajili kumpata Katibu Mkuu, hii ni nafasi nyeti sana ndiyo maana hata wenzetu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanafuatilia kwa ukaribu kujua nani atapewa mikoba ya Dr Slaa.
apo umechemka vyanzo vyako vimeanza kuchakaa mkuu
 
TUSINGILIE KAZI ZA WAGANGA TUKAGEUKA KUWA WAPIGA RAMLI TUVUTE SUBIRI NITAWEKA HAPA JINA
 
Hujui kitu wewe msukule kula pumba!
1457719762940.jpg
 
Back
Top Bottom