Freeman Mbowe na Mr.II Sugu wafanya kweli Iringa!

Freeman Mbowe na Mr.II Sugu wafanya kweli Iringa!

Nadhani watu wengi sana bado hawajamfahamu vizuri Kamanda Mr II wa ukweli na nii maana yake kisiasa kwa vijana pindi apandapo jukwaani.

Jana Mh. Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM pamoja na Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini walifanya kweli katika mji wa Manispaa ya Iringa.

Shughuli hii inafuatia kuwapo kwa Uchaguzi mdogo katika kata tatu za Kitanzini, Gangilonga na Kihesa zilizopo hapa mjini.

Katika Mkutano ule Mbowe alinukuliwa akisema kuwa Kinachotea sasa SI MPANGO MZIMA TU BALI NI MPANGO WA MUNGU, Kwamba kumekuwepo njama za kutaka kukatisha harakati za Kupigania Mabadiliko zifanywazo na Chadema lakini kwa Kudra za Mwenyezi Mungu Harakati zinasonga mbele.

Mbowe pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wanachama wa chama cha mapinduzi wawaunge mkono chadema kwani ndicho chama haswa chenye nia thabiti ya kutaka kuleta mabadiliko kwa maendeleo ya watanzania, Mwenyekiti Mbowe alimalizia kwa Kuwaombea Kura madiwani wake.

Mh. Sugu kama kawaida alifunga mkutano kwa Mistari na kusisitiza kuwa Chadema ni dume la mbegu kweli na kuahidi kudhihirisha hili katika shughuri ya Igunga coz kwa mpango wa chama Muziki rasmi utaanza trh 25 Sept 2011 timu ya Makamanda itakapo wasili rasmi kwa Kazi!
 
Huyo mtu ni Mwita25 ambaye ndiyo philanderer mwenyewe.Thread yoyote ya sugu huyu mtu lazima aweke chuki zake binafsi dhidi ya Sugu!Huwa hana hoja za kupingana na sugu zaidi ya kuleta historia yake ya elimu na jinsi alivyokwenda majuu.Hajui kwamba hiyo ni historia ambayo hata Obama anayo ya kwake lakini la muhimu ni jinsi gani kiongozi anadeliver kwa anaowaongoza baada ya kuwa kiongozi.Watu wote wamtaa huu wanajua kuwa wewe ni mwita25 na bado kuna ID zako zingine nitakwambia siku nyingine.
Kuna ukweli ndani yake maana Mwita25 ndio wale wa THT walio na bifu na SUGU.
 
Mbona kuna mtu humu alituambia kuwa Mbunge wa Njombe Jah People,Mbunge wa Korogwe vijijini Prof Maji Marefu,Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde na Mbunge wa Rorya Lameck Aiko wote kupitia CCM HAWANA FORMAL EDUCATION ikiwa na maana kuwa hawajasoma hata darasa la kwanza!

Ile thread ina ongea ukweli au inawachafua tu hawa wabunge mtz mwenzangu philanderer?

wape wape heeee vidonge vyao wakimeza wakitema ni shauri yao
 
Mbona kuna mtu humu jamvini huwa anasema eti Sugu alipata division four mtihani wa form four sasa hii thread ina ukweli gani?
rais kibaki wa kenya ni rais wa kwanza afrika muhitimu wa chuo kikuu lakini angalia upupu alioufanya kung'ang'ania madaraka,Daudi Balali alifaulu vizuri sana but cheki madudu yake,haijalishi ulipata nini shule,whats matter ni kuwa umeachieve nini baada ya hapo.
 
...duuuh!...........naona una-manyisya kweli kweli shemeji.......!
 
rais kibaki wa kenya ni rais wa kwanza afrika muhitimu wa chuo kikuu lakini angalia upupu alioufanya kung'ang'ania madaraka,Daudi Balali alifaulu vizuri sana but cheki madudu yake,haijalishi ulipata nini shule,whats matter ni kuwa umeachieve nini baada ya hapo.

Acha kufanya kila mtu humu jamvini ana akili za kuku! Kibaki ni Raisi wa kwanza Afrika mhitimu wa chuo kikuu? Una uhakika unachokinena kweli?
 
Mhh magamba kwa kujitetea eti sugu ana div 4 mbona huyo lusinde ,prof maji marefu elimu zao ndogo sana,cha kushangaza magamba yalimtosa phil. Mangula kuwa mwenyetiki yakampa jah people huko mkoani iringa,huyu naye ni kituko cha mwaka.kihistoria george washngton hakupata formal education yoyote ile but ndiye baba wa taifa la marekani
 
Mbona kuna mtu humu jamvini huwa anasema eti Sugu alipata division four mtihani wa form four sasa hii thread ina ukweli gani?

Masaburi yk! Div four ya Mr Sugu inaingiaje ktk thread hii,Kamuulize Lusinde mjinga mwenzio darasa la vii feriya aliyejichagulia kifo baada ya uchaguzi wa Igunga!....**
 
Acha kufanya kila mtu humu jamvini ana akili za kuku! Kibaki ni Raisi wa kwanza Afrika mhitimu wa chuo kikuu? Una uhakika unachokinena kweli?
Ninachojua mimi kibaki ni mwafirika wa kwanza kupata first class huko UK
 
Jana Mh. Freeman Mbowe ... akisema kuwa Kinachotea sasa SI MPANGO MZIMA TU BALI NI MPANGO WA MUNGU,
Alirudia sana maneno hayo Igunga, akisema CHADEMA wanafanya kazi ya Mungu.

Again, poor campaign advisement, CHADEMA kimepachikwa label ya chama cha kidini, haisaidii kuvua taswira hiyo kama kila hotuba ya Mwenyekiti inasisitiza anafanya "kazi ya Mungu, CHADEMA ni mpango wa Mungu." Kuna fumbo hapo? Mpango wa Mungu upi, wenye inclinations za kidini au wachambuzi wengine watajiuliza.

Ninaamini kabisa Dr. Slaa na JK waligawana kura za baadhi ya wananchi kwa misingi ya dini. Udini wa wananchi, sina hakika kama ulipaliliwa na CHADEMA na CCM wenyewe, sidhani, lakini udini wa wananchi uliathiri CHADEMA uchaguzi wa mwaka jana.

Mwenyekiti Mbowe, achana na mipango ya Mungu na kazi za Mungu. Tunaomba msisitizo wa mipango wa CHADEMA.
 
Makamanda nawaaminia kinoma..na ukweli wa mambo ya Chadema upo live...Sasa wanaokataa na wakataee.. kila kona CCM wamebanwa masaburi...mh
 
Mbona kuna mtu humu jamvini huwa anasema eti Sugu alipata division four mtihani wa form four sasa hii thread ina ukweli gani?

Unafahamu serikali yako ya CCM imeuza madini yote, ikiwa haitoshi, imewaachia wawekezaji kumwaga maji yenye sumu kwenye mito na haya ndio madhara yake kwa akina mama na wananchi wengine wa mkoa wa Mara??
kilaza!!!
2.JPG
 
Tena maelfu ya Watanzania tupo nyuma ya CHADEMA maana CCM ni chama mfu jamani
 
Jana Mh. Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM pamoja na Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini walifanya kweli katika mji wa Manispaa ya Iringa.

Shughuli hii inafuatia kuwapo kwa Uchaguzi mdogo katika kata tatu za Kitanzini, Gangilonga na Kihesa zilizopo hapa mjini.

Katika Mkutano ule Mbowe alinukuliwa akisema kuwa Kinachotea sasa SI MPANGO MZIMA TU BALI NI MPANGO WA MUNGU, Kwamba kumekuwepo njama za kutaka kukatisha harakati za Kupigania Mabadiliko zifanywazo na Chadema lakini kwa Kudra za Mwenyezi Mungu Harakati zinasonga mbele.

Mbowe pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wanachama wa chama cha mapinduzi wawaunge mkono chadema kwani ndicho chama haswa chenye nia thabiti ya kutaka kuleta mabadiliko kwa maendeleo ya watanzania, Mwenyekiti Mbowe alimalizia kwa Kuwaombea Kura madiwani wake.

Mh. Sugu kama kawaida alifunga mkutano kwa Mistari na kusisitiza kuwa Chadema ni dume la mbegu kweli na kuahidi kudhihirisha hili katika shughuri ya Igunga coz kwa mpango wa chama Muziki rasmi utaanza trh 25 Sept 2011 timu ya Makamanda itakapo wasili rasmi kwa Kazi!

Ha ha ha ha ah....Da nasikia raha sana,hii spidi ya CDM very encouraging!!! Well done CDM,pamoja sana!!!
 
Ni kweli mikutano yote ilifana,Mh chiku obwai,akawaambia wanamama waache kuhongwa elfu tano tano na CCM ili kumchagua diwani,kwani kufanya hivyo ni kudhalilisha utu wao kwani wakifanya kazi wanaweza kupata zaidi ya hiyo.
 
Back
Top Bottom