Ni upogo wa kufikiri kudhani kwamba Mkoa wa Mtwara wote ni Pwani. Kwa taarifa tu ni kuwa Masasi ni bara kuliko hata Same au Mikumi. Umbali wa Mtwara (Mji/Manispaa)hadi Masasi ni sawa au mbali kuliko Dar-Moro, sembuse huko Lupaso zaidi ya Kilometa 270 kutoka mjini, huko Culture za pwani hamna kabisa. Tunashauri Tembeeni tu hata hapa Tanzania, yapo ya kujifunza kuliko kukariri au kutegemea story za Vijiweni.
Hivyo in brief, ukisikia Mtwara ni Pwani basi tambua ni Mtwara Manispaa na Vijijini tu. Nje ya hapo ni Bara kabisa, namanisha Newala, Masasi, Tandahimba, Nanyumbu, Nannyamba na Ndanda, hao hata bahari hawaijui inafananaje, labda kwa waliowahi kutembelea Mjini Mtwara, na ofcourse tamaduni ziko tofauti kabisa!