Freeman Mbowe: Majipu matatu haya hapa

Freeman Mbowe: Majipu matatu haya hapa

sasa anataja hayo majipu anataka nani ayatumbue wakati magufuli hamtambui/ ampe lowassa kazi hiyo
 
Hizi kauli na mijadala yake vinazidi kuthibitisha tulivyo watu tusio na mwelekeo kabisa. Kuna mdau hapa alieleza hali halisi ya nchi ilivyokuwa na ilivyo na kutoa wazo la kuleta tume ya ukweli na maridhiano (truth and reconciliation commission).

Wale wanaoamini kuwa ni suala la kutumbua majipu "machache" tu halafu mambo yanabaki shwari basi wadai mahakama ya mafisadi ianzishwe haraka ili waone hao mafisadi papa "wachache" wakifungwa haraka sana.

Ni ajabu sana kushabikia utumbuaji wa majipu halafu usitarajie marais waliopita baada ya Nyerere wasiguswe. Hii ni pamoja na wazito wengine ambao baadhi wana nyadhfa serikalini na bungeni. Na wengine wakiwa nje kama EL. Ukiwa mkweli, lazima wote hao uwachukulie hatua za kisheria.

Dili zote kubwa za kifisadi zimekuwa zikipangwa ikulu. Someni makala na vitabu kama cha Andrew Feinstein (The Shadow World) muone data na mikakati ya akina "nyoka wa makengeza" wakisuka vitu vya uhakika. Usipowatumbua hao unabakia kuwa mbabaishaji. Ni ajabu kuwa Nyerere aliwapigia watu kampeni huku akishangaa ni biashara gani inayowafanya wakanyagane kuingia mjengoni.
 
Hayo ni majipu kwelikweli lakini Katiba.....

Kwa Sefue sijui lakini haya mawili yaliyouza raslimali za nchi hii kwa mrahaba wa aslimia 3 yalistahili kuhukumiwa ila katiba hii wanayoikumbatia

Tena mbaya zaidi Lubuva anang'ang'ana aipitishe (poor Tz yangu)
 
sasa anataja hayo majipu anataka nani ayatumbue wakati magufuli hamtambui/ ampe lowassa kazi hiyo

Bahati mbaya umejaa ushabiki. Ni kweli Magufuli hawezi kuyagusa lakini taasisi zetu xilitakiwa ziwe na nguvu kwa wote e.g. Angalia mahakama za Africa kusini hata watawala wanashtakiwa huko na kuhukumiwa
 
Zote zikisikia ccm ni ile ile zinanyamaza
 
Na wanaoshabikia CCM na utawala huu huwa najiuliza kama ni hamnazo au ni kufaidika na ushabiki huo. Mambo yako wazi wasomi wa nchi hii waisaidie nchi historia isije kuwahukumu
Njaa mbaya sana ndio ilimsaliti haya Yesu
 
Mbowe naye ni jipu linalosubiri kutumbuliwa Hai

Wakudadavua;
Hivi kweli wewe ni wa kudadavua?? Usiende nje ya mada. Mbowe kasema; hao aliowataja ndiyo majipu yanayotakiwa kutumbua haraka. Sasa ka weye unataka naye atumbuliwe, kwanza basi mwambiye JPM ayatumbue hayo yalio tajwa, akimaliza umkumbushe hilo lako. Huo ndo utaratibu. Tukiufuata utaratibu wako, nadhani tutaishia kushitakia ka watoto, kuwa ukinisema nami ntakusemea.
 
Kutaja majina tu hata wehu wanaweza.

Hata ile orodha ya Mwembeyanga ambayo hamtaki hata kuisikia kwa sasa nayo mliropoka hivi hivi.
Hata ambayo yanatumbuliwa inaonesha Aidha yamegota muda wa utumishi, hayapendwi kwenye chama au yalikuwa mlengo wa Lowassa

Majipu yenyewe yanakula bata yaliyoingia mikataba mibovu ya gesi na madini.
 
Wakudadavua;
Hivi kweli wewe ni wa kudadavua?? Usiende nje ya mada. Mbowe kasema; hao aliowataja ndiyo majipu yanayotakiwa kutumbua haraka. Sasa ka weye unataka naye atumbuliwe, kwanza basi mwambiye JPM ayatumbue hayo yalio tajwa, akimaliza umkumbushe hilo lako. Huo ndo utaratibu. Tukiufuata utaratibu wako, nadhani tutaishia kushitakia ka watoto, kuwa ukinisema nami ntakusemea.
Atumbue na aliyeuza nyumba za serekali kwa bei chee
 
Mbowe naye ni jipu linalosubiri kutumbuliwa Hai
Mtumbue kwanza aliyeuza nyumba za serekali kwa bei chee aliye tengeneza barabara za lami zenye uwezo sawa na Big G, aliyejigawia Mgodi wa makaa ya mawee kwa bei chee aliye binafsisha bank zetu kwa bei yakutupa aliyekua anatalii nchi za njee kuliko alivyokua anakwenda kwao
 
Yeye mwenyewe Mbowe anasubiri kutumbuliwa. Alipewa uongozi mwaka 2004, alipaswa kukabidhi uongozi kwa mwingine mwaka 2014, leo hii 2016 anawanyooshea vidole wengine, wakati kutumbuliwa kunamhusu pia.
Kama Mbowe ni jipu, haiondoi hao aliowataja. Ikithibitika watumbuliwe tu, maana PM alisema namnukuu maneno yake-Wakati wa Kutumbua Majipu, Hatutamuonea Mtu,mwisho wa kunukuu.

Hivyo kila anaestahiki jipu atumbuliwe tu!

Ila falsafa hii ya jipu sijaipata kinagabaga lengo ni nini?!:-
1. Kuondoa wabadhirifu
2. Kuwashtaki Wabadhirifu
3.Kuondoa wazembe
4. Kuunda Team Mpya

Au hasa ni nini?
 
Back
Top Bottom