UTAPELI KWA KIGEZO CHA AJIRA
Na Malisa GJ.
Mnamo mwezi uliopita kuna organisation inajiita REBORN INTERNATIONAL walitangaza nafasi za kazi kwa malipo ya Tsh 4,530,000/= kwa miezi mitatu kwa position ya Civic and Voters Education Officers concerning with Tanzania Referundum Support Project.
Nasikia jana wameanza kujibu walioomba na kuwaambia wamefanikiwa kupata nafasi hizo na kuwaambia kwamba wa scan vyeti vyao na kuvituma kwa mwanasheria wao vikiambatana na Tsh 51,500/= as a verification fee inayotumwa kwenye namba walizoweka ama kwenye akaunti ya Twiga Bancorp Bank.
PLEASE AND PLEASE WENZANGU MNAIBIWA SO MSITUME HIZO PESA.
Kwanza hao Reborn ni NGO haiwezi kutangaza nafasi za maafisa wa kuandikisha wapiga kura. Nafasi hizo ni serikali tu iwezayo kuajiri chini ya wizara na idara zake. Mara nyingi waalimu ndio wamekua wakitumika.
Pili, Hao REABORN hawana ofisi popote Tanzania. Ofisi walizotaja kwenye tangazo lao la ajira kuwa zipo Mikocheni si kweli, mbona hawajaweka phisical adress kama ilivyo kwa ofisi nyingi nchini?
Halafu kwanini akaunti namba ni ya mtu binafsi? Yani organization kubwa inayoweza kulipa mil.4 kwa mtu mmoja inakosa akaunti hadi watumie ya mtu binafsi? Jiulize mara mbili, usikubali kutapeliwa kijinga.
Watu wengi wanatumia tatizo la ajira kujinufaisha. Kama ni wakweli kwanini wasiruhusu mtu averify vyeti vyake mahakamani kama ilivyo utaratibu wa siku zote?
Au kwanini wasikukate hela kwenye malipo yako wakamlipa huyo mwanasheria wao akaverify vyeti halafu wakati wa kuja kulipwa ukaambiwa kiasi fulani kilikatwa kumlipa mwanasheria?
Plz and plz wandugu msijaribu kutapeliwa kijinga hivi. Mtu mwenye nia ya kweli ya kukupa kazi hawezi kuhitaji hela. Na kama atahitaji sio kabla ya kuajiriwa. Atahakikisha umepata kazi kwanza ndio umpe hela. Ukiona mtu yeyote anayetaka hela kabla ya kazi huyo ni TAPELI..
Wameona vijana wengi hawana ajira na kwa dau walilotangaza (japo si kubwa sana) lakini vijana wengi watakimbilia maana wamechoka kutembeza bahasha za kaki maofisini.
So usikubali kutuma.. Na kama umeshatuma kunywa maji mengi ushushe hasira kisha upige kimya, maana ushatapeliwa. Kama bado hujatuma mshukuru Mungu then jipange upya, kazi zipo na utafanikiwa tu siku moja.
Foward ujumbe huu kwa wengine ili kusaidia wengine walio kwenye mchakato wa kutuma.