Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
This is a very logical but biased analysis. Hofu hii ya tuzo kuchafuka kutokana na jina la mwenye tuzo kuchafuka ipo; ndio maana taasisi nyingi huchagua majina ya hayati katika tuzo. Lakini tunaweza pia kumpima mtu kwa muda aliyoishi mpaka wakati huo maamuzi yanapofanyika.
Naamini vijana wa Mikoa mingine wanapaswa kuiga mfano huu wa Mkoa wa Kinondoni ambao Mwenyekiti Mbowe ni mmoja wa wakazi wake mathalani mkoa wa Mara unaweza kuanzisha Tuzo ya Ujasiri ya Chacha Wangwe.
JJ
JJ hapo nilipoweka redi ni statements mbili zinazokinzana. Mwanajamvi hapo juu alishauri ni bora tuzo ikapewa jina la almarhum kwa sababu ni mtu aliyemaliza kazi yake. Naamini hapo chadema mnao watu wengi wakiwemo waasisi wa chama waliofanya kazi kubwa kukifikisha chama hapo kilipo na wengine bado wapo wanafanya kazi nzuri(bado tunakumbuka vizuri namna wazee hao walivyotumia busara wakati wa uchaguzi wenu mwezi septemba) na wapo wengine wametangulia mbele ya haki. Kwahiyo mngeweza kumtumia mmoja wapo kwenye hiyo tuzo. Wasiwasi wa wadau ni kuonekana mnamtukuza sana mbowe, mnafanya yale mambo ya zidumu fikra za mwenyekiti.
Kwakuwa umemtaja almarhum kamanda Chacha Wangwe basi nadhani katika mtazamo huo huo mfikirie kubadilisha jina la hiyo tuzo, na mimi nadhani hakuna ubaya wowote mkiita kwa jina la Chacha Wangwe. Sio lazima ifanywe na watu wa mkoa wa mara, kwakuwa Chacha Wangwe alikuwa kiongozi wa kitaifa katika chama chenu na alichangia kwa kiasi kikubwa ustawi na kushamiri kwa chadema wilayani Tarime na mkoaa mara kwa ujumla.
Kama mkiendelea kusisitiza na kuhimiza utoaji wa tuzo kwa kuangalia mahali mtu alikozaliwa, jihadhari sana msije mkaonekana wakabila!!!